Uchafu unaohatarisha afya za wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchafu unaohatarisha afya za wananchi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ChaMtuMavi, Sep 22, 2009.

 1. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Leo ninakerwa na uchafu unaoimarishwa na viongozi wetu ambao unaathiri afya za wananchi.

  Kuna hii issue ya viongozi wetu (wanasiasa) Kuanzisha shule zao binafsi (private schools). Tunawashukuru kwa jitihada zao; LAKINI.

  Viongozi wanajenga shule bila kuweka system za kukusanya na ku-treat maji taka toka vyooni (sewage). Hii inasikitisha sana.

  1. Kuna shule ya Mbunge wa Songea Mh.John Komba, ipo kule Mbweni Mpiji. Shule ni ya bweni, imezungushiwa wigo wa senyenge. Ina wanafunzi zaidi ya 1000. Maji ya vyooni yanayozalishwa na wanafunzi yamechimbiwa ka-mfereji (open & shallow) nje ya fence ya shule. Maji hayo yanatiririka kuelekea kwenye barabara kuu na kwenye property za wengine jirani, yananuka sana. Wananchi wanalalamika lakini hakuna hatua zinazochukuliwa kisa eti shule ni ya mheshimiwa, ameshafikishiwa malalamiko lakini hakuna kilichofanyika.

  Kwa hali hii Watanzania tutaondokana na uchafu????

  2. Shule nyingine ni ya mam ANNA MKAPA ipo karibu na shule ya Mh. Komba kule Mbweni Mpigi. Yenyewe ipo kwenye mwinuko na imezungushiwa vizuri sana, lakini nayo inatema untreated maji taka nje ya fence, yakielekewa katika makazi ya wananchi.

  Jamani huyu mwananchi atajikomboaje na hali hiii? Ni MJINGA, MASIKINI, pia manamletea MARADHI mpaka kwenye mmakazi yake???? HUU NI UUNGWANA KWELI???

  Viongozi tunawachagua wajipatie pesa na kuanzisha miradi inayowaua wananchi?? Halafu leo utamkemea mwekezaji huko Geita anauwa wananchi kwa taka za sumu majini???

  Vipindupindu, mazalio ya mbu na malaria vitaishaje??

  Sisi wananchi wa eneo hili tumekerwa sana, tumeona tulilete humu ili wanaJamii Forum watusaidie kuchambua hilo. Mji wetu ni mpya, planned na tungependa tuuweke katika hali inayokubalika ki-mazingira lakini viongozi wetu wanatuangusha na kutukatisha tamaa.
   
 2. F

  FOE Member

  #2
  Sep 22, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CV yenyewe ndio kama hivyo tulivyokwishawahi kuiona. Leo hii atajenga shule nzuri kweli? Mifumo ya maji safi maji taka anajua umuhimu wake? Anaweza akawa kainvest pesa nyingi sana kwenye kwaya ya shule hiyo badala ya vitu muhimu. Bado tunakazi kubwa ya kuondoa watu kama hawa bungeni! Tulifikiri mwalimu akiwa na shule itapendeza kumbe ndio worse !!!
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,374
  Likes Received: 3,138
  Trophy Points: 280
  kama watoto wa wakubwa wangekuwa wanasoma shule za kata nadhana hawa viongozi wangekuwa na huruma sana...........hata salva rweyemamu aliyesema kikwete amefanikiwa katika mengi likiwemo la kujenga shule zilizo kamilika kila kitu bado watoto wake hawawezi kusoma hizo shule,hebu fanya utafiti ujue watoto wake wanasoma wapi?
   
 4. H

  Haruna Malima Member

  #4
  Sep 23, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wasimamizi wa shule waliopewa majukumu na serikali ndio tatizo. Wapo wakaguzi wa shule, Halmashauri , manispaa na jiji pia wizara husika: si wasimamizi wazuri. Vyombo vipo usimamizi mbovu. Komba ama Mama Mkapa Hawajui kanuni, vigezo na taratibu ila wanajua sheria Mama tu za kuanzisha shule na kama wame-comply lawama ziende kwa waliopewa majukumu ya kusimamia elimu na facilities zake. Tuanzie hapo.
   
 5. O

  Ogah JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kwanza nikupongeze kwa kuondoa ile avatar yako

  Pili nikupongeze kwa mada nzuri.........

  System ikiwa corrupt ndio matokeo yake.......kuanzia viongozi mpaka watu wanotakiwa kusimamia.........

  Cha kufanya......ni kuwaumbua.....Piga picha weka mtandaoni i.e. magazetini na kwenye internet pia...........

  Pili, kama kuna mtu ana contacts zake azimwage hapa, na watu watawataarifu wahusika..........
   
Loading...