Uchafu...uchafu wa big brother africa (bba)

Mbavu mbili

JF-Expert Member
Apr 25, 2011
1,456
872
Binafsi sioni umuhimu wa kuwepo BBA, Shindano lililojizolea umaarufu mkubwa barani Afrika na Duniani kwa ujumla.
Hofu yangu ni kwamba namna ambavyo mambo yanaendeshwa ndani ya jumba hilo ni Kuudhalilisha utamaduni wa mtu mweusi, utu wake, na nchi atokako mshiriki husika.
mathalani
?Washiriki wamekuwa wakioneshwa Nusu uchi kama siyo uchi kabisa,
?Wakikaribia kufanya ngono,kama siyo kufanya kabisa.
?Sijajua kinachoshindaniwa na washiriki ni kipi? Kuonesha namna waafrika tunavyoweza kuishi.kama wazungu?...Au ni nini?
Shindano hili hurushwa LIVE bila kuficha jambo lolote...
SWALI LANGU....
Tunamfundisha nini na kujenga vipi maadili ya Watoto tunaowalea?
Binafsi shindano linanikera kwani Halina tija na limeshindwa kuutangaza vilivyo utamaduni wa nchi husika badala yake wahusika wamekuwa muda mwingi WAKINGONOKA TU...
HUU NI MTAZAMO WANGU TU...
 
Kiongozi wakati concern yako iko sahihi juu ya utamaduni wa mwafrika kupotoshwa ni makosa kama umeruhusu wanao kuangalia channel 198 maana its not meant for under age.

Wakionyesha kwenye local channels mara nyingi picha zinakuwa zimehaririwa.

This is what they call free market, sell anything so long as the demand is there! Tumlaum nani??
 
Nynaya yangu mwenye umri wa 101 years aliwahi kuniambia kabla ya World War i watu wengi tu walikuwa wakienda uchi kabisa au nusu uchi.
Nguo kama tuzijuavyo leo hazina mika hata 150 tangu tuanze kuzivaa.

Hii aibu ya mtu kwenda uchi ni matokeo ya kuchamnganya mambo.

Wazungu waliotuletea na kutufundisha kuvaa nguo wao ndo kwanza wanatembea uchi.

Ngoma nyingi za utamaduni Tanzania zinaelezea zaidi ngono,kigoli chuma, kijana mzuri wa kuvutia mademu wote na jinsi ya kufanya tendo la ngono.

Kushindwa kuona kuona utamaduni wa Mtanzania katika sura yake halisi kunatokana na kutafsiri utamaduni wa Mtanzania kwa kutumia kigezo cha imani ya dini za kuja( Dini zilizoletwa na wageni)

Wazungu wakikumbatiana na kusakana Zero Distance poa.

WaTZ tukikata viuno vya kufa mtu matusi, tukivaa vibwaya matusi, tukionyesha makalio yetu matusi.

Jmabo lolote lile linaweza kuwa Tusi inategemea tu linasemwaje.

Neno Kunduchi, Makunduchi kama jina la mji si tusi. Lakini likitumiwa katika sentensi fulani ni tusi

Hebu ondoa hilo kunduchi lako!

Watu siku hizi wakienda pwani kazi kutembea makunduchi hata aibu hawana!


Ushauri.
Ukiona mambo yanakwenda kinyume na imani yako mpya ambayo babu wa babu wa babu yako haijui badili channel. TV yako ina Channel 1 tu??
 
Watanzania inatuuma baada ya kupeleka wale dada zetu wakamegwa lakini tulivyokuwa tuna wamega hatukuona tatizo.....lol
 
Mkuu wenye akili hatuangalii huo upuuzi kuna chanel nyingi unaweza kuangalia mambo yanayo jenga, na hujalazimishwa kuangalio hio kitu, au unafanya sitaki nataka unachungulia af unashindwa kuhamisha
 
Unalalamika nini ndugu? Very simple ondoa interest na hakikisha imezimwa. Mie binafsi hata siwajui washiriki na sina haja hata ya kujua nini kinaendelea. Huo muda wa BBA nitafanya kazi nyingine-simple.
 
Post kama hii imepitwa na wakati, anyway muleta mada ameongeza idadi ya post. Hapa tz watu wanamegana kila mahali na kila wakati harafu mtu anajifanya kushangaa as if muwakulishi weti hajawahi ku*****a. Uliza waliosoma Tumaini university 2years ago watakueleza maisha halisi ya mmoja wa wawakilishi wetu alivyokuwa.
 
Unajua maana ya ile nembo inayotumika? nembo ya jicho?, it is one of gods being worshiped by Freemasons, they are behind the whole thing, ndiyo wanaotoa hata zawadi, it is all about to praise and glorify Satan.
 
Binafsi sioni umuhimu wa kuwepo BBA, Shindano lililojizolea umaarufu mkubwa barani Afrika na Duniani kwa ujumla.
Hofu yangu ni kwamba namna ambavyo mambo yanaendeshwa ndani ya jumba hilo ni Kuudhalilisha utamaduni wa mtu mweusi, utu wake, na nchi atokako mshiriki husika.
mathalani
?Washiriki wamekuwa wakioneshwa Nusu uchi kama siyo uchi kabisa,
?Wakikaribia kufanya ngono,kama siyo kufanya kabisa.
?Sijajua kinachoshindaniwa na washiriki ni kipi? Kuonesha namna waafrika tunavyoweza kuishi.kama wazungu?...Au ni nini?
Shindano hili hurushwa LIVE bila kuficha jambo lolote...
SWALI LANGU....
Tunamfundisha nini na kujenga vipi maadili ya Watoto tunaowalea?
Binafsi shindano linanikera kwani Halina tija na limeshindwa kuutangaza vilivyo utamaduni wa nchi husika badala yake wahusika wamekuwa muda mwingi WAKINGONOKA TU...
HUU NI MTAZAMO WANGU TU...

Ni channel gani jamani nitathmini viwango vya maadili?
 
Hizi thread za kuponda BBA zimezidi, Mods naomba muwe mnazipotezea juu kwa juu
 
I think we should send comments to BBA, telling them to change the content of this program...kwa sababu inapoelekea hata watazamaji itakosa, kwanza inabore coz mambo ni yaleyale kila siku, watu waende pale kile ambacho ni interesting ni ngono tu hamna kingine ni ujinga ujinga! more creativity should be based on an African realities.
 
Mwajifanya mwaahangaa je hao wanaojiuza mchana kweupe unawachukuliaje. Mnajifanya wastarabu mbele za macho ya watu. Kumbe nanyie mwayafanya
 
ila kwel hakuna maana BBA ni uchafu 2uu

Serikali lazima ingilie hilo swala mbona kwenye nchi nyingine kipindi kichafu kama bba hata watu wazima hawaruhusiwi kuangalia mfano iran huwezi onyeshaza upuzi kama huu kwa utetezi kwamba hili ni soko huria
 
hakuna cha kulalamika hapo, sii lazima kuangalia na kuhusu watoto kipindi hicho kina parental guide sasa iweje usemee watoto hapo? huku umangani kuna kipindi kinaitwa SEX EDUCATION VS PONOGRAPHY kinaonyesha maungo ya wanafunzi au watu wanaojitolea wananfunzi kuwasoma live na kuuliza maswali kushusu maumbile yao wakiwa uchi, pia kuna VIPINDI VINAVOUWIANA NA bba WATU WANAKULA NGONO LIVE na vinaonyeshwa hata mchana, cha kushangaza nin nn?? kujificha ficha kwetu ndiko kunakoharibu watoto wetu manake wanajua vingi kuliko tuwadhaniavo.Kusema DSTV inaonekana ulimwenguni kote sio kweli man Europe kuNA CANAL DIGITAL haina hizo channel za MNET.
 
Usemayo ni kweli, lkn najua wapo watakao kupinga, na wengine pia watasema BBA haina tatizo lolote, kweli hiki ni kizazi cha majaribio........
 
Back
Top Bottom