Majs
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 232
- 520
HALMASHAURI ya Manispaa ya Ubungo imeanza kuzifungia rasmi shule zote binafsi ambazo hazijasajiliwa katika kata ya Kwembe huku ikibaini kuwepo kwa shule takriban 100 ambazo hazijafuata utaratibu.
Ofisa Elimu wa Manispaa hiyo, Chausiku Masegenya akiambatana na timu ya wataalamu kutoka idara yake pamoja na idara ya ujenzi tayari wamezifungia shule sita ambazo zimekuwa zikiendelea kutoa huduma licha ya kuwa hazijasajiliwa.
Katika kutekeleza kazi hiyo, iliyoanzia Kata ya Kwembe shule zilizofungwa ni pamoja na Child Future Success Day Care, Tumaini Nursery School, Life shine Nursery and Primary School, King David Nursery School, Joycare Nursery na Mwao Nursery.
Chausiku akiwa katika hatua hiyo, Mwalimu Mkuu wa shule ya Mwao Nursery (ambaye hakutaka kutaja jina lake) alidai kuwa shule yake ina usajili na alipotakiwa kutoa vielelezo vya usajili wa shule hakutoa hivyo ilimlazimu Ofisa Elimu kuifunga hadi hapo atakapowasilisha taarifa za usajili.
Akitoa taarifa ya jumla kuhusu hatua hiyo ya kufungia shule, Chausiku alisema kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, John Kayombo hawezi kuendelea kufumbia macho suala la watu binafsi kufungua shule bila kufuata kanuni na taratibu za kisheria za kuanzisha shule.