siku nzima itaishia hapohapo kwenye foleni,..
Mkiambiwa muachane na private mtumie public transport kwa muda huu ujenzi ukiendelea hamuelewi,.
Hamna wa kulaumiwa hapo!!
Kuweni wavumilivu mpaka hapo mtakapopata suluhu maana hata busara ya kumruhusu mwenzio apite kwanza naona imegonga mwamba kila mtu anajidai ana haraka kuliko mwenzake!!
Unahitaji maombi mkuu!! kwa usafiri upi wa public ambao ni tegemeo dar hii. Watu wote wangependa ku drive ila tu hawana uwezo kwa namna moja au nyingine, usafiri wa public dar ni mateso. mabasi yanajaa sana, foleni ukiwa umesimama muda mrefu, ni mateso tu.
Ungetumia muda wako kuwashauri watu waliopata bahati ya kutoa maamuzi ila hawana uwezo kifikra ili wajenge flyovers na ring and feeder roads ningekusifu.
Ungewashauri kuwa kabla ya kujenga BRT dar wangeanza kuziweka lami njia mbadala kama za makongo hadi goba, goba hadi masana, mbezi mwisho hadi tabata na hata pugu au gmboto, then ndo waendelee na huo mradi wao ambao hata hatuoni utasaidia nini wakazi wa dar.
Barabara hiyo hiyo moja, unang'oa lami nzuri unaweka ingine eti kisa mabasi ambayo hujui ubungo yatapitaje, sijui yatawekewa mabawa yapae?!!!! this is completely not serious!
Na ndo maana hawatuwekei 3D drawings kwenye maungio muhimu kama ubungo kutuonyesha mradi ukiisha kutakuwaje hapo ubungo. wameondoa traffic lights, askari asipokuwepo kidogo tu kunafunga, wameanza kujenga li msingi pale katikati, hata hatujui wana plan ipi!!!
Hivi ubungo kuna mbunge kweli!!! huyu mbunge yeye anaishi wapi ambapo haoni tabu wanayopata wananchi wake hapo ubungo.
Sijui ni lini nchi itawasikiliza wataalam katika kufanya maamuzi.