Ubunge wa Mh. Kagasheki mashakani Bukoba Mjini

Ubunge wa Mh. Kagasheki mashakani Bukoba Mjini

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,793
Reaction score
7,173
Wana JF,

Hali ya mbunge wa Bukoba mjini ni mbaya sana baada ya wakazi wa mji huu kuanza kumkataa rasmi kwa kuwa ameshindwa kazi ya kuliongoza jimbo hilo.

Awali palikuwepo migogoro mingi iliyohusisha Madiwani na Meya wa Jiji ambayo ilimalizika kwa meya kujihuzuru kwa kulazimishwa na waziri mkuu, hata hivyo vurugu za chini chini hazikuisha kiasi kwamba zimeleta athari kubwa katika kuendeleza mji huu. baadhi ya shughuli za maendeleo zimekwama sana ukilinganisha na juhudi za mbunge wa awali bwana Rwakatare ambaye alikuwa kipenzi cha wengi lakini CCM wakaweka nguvu kubwa kulirudisha jimbo hili hadi kwa kupigwa mabomu. Katika hali isiyo ya kawaida mbunge huyu anaonekana mchapa kazi sana serikalini kabla ya kuachishwa uwaziri lakini jimboni kwake ni butu, hali ambayo wengi wamemkumbuka sana Bw. Rwakatare.

Sehemu nyingi za mji ni chafu kupindukia, yaani ukifika bukoba mjini huwezi kuamini kuwa ndiko kunatoka mshomile ambao wanazaniwa kuwa ndio wastaarabu na wanajipenda sana. Kufifia kwa maendeleo ni pamoja na kufuka kwa migogoro ya wana ccm wapenda madaraka huku hawawezi kazi, wakipewa kazi wanatanguliza ten per sent jambo ambalo linawafanya wakandarasi kutengeneza barabara mbovu, mitaro mibovu na madaraja feki.

Ona sasa stand ya kutisha ya mji huu
attachment.php

 

Attachments

  • bukoba.jpg
    bukoba.jpg
    50.5 KB · Views: 6,745
Ukifika tu stand badala ya kukumbana na wamachinga unakumbana na senene. Bora Lwakatare arudi.
 
Siku zake zinahesabika sana pamoja njama zake nyingi za kuhonga makundi mengi yakiwemo ya akina mama na wazee huku akiwatishia waziwazi wale watakaojitokeza kumpinga kwenye chama chake,tunampa pole kubwa kwani wapiga kura ndo sie na kamwe hatokaa arudi hapo,miaka 5 aliyokaa kwa kuleta ushoga na mabishano ya wao kwa wao inatosha, dawa yao ni Ukawa wafanye juu chini kutupa MTU mwenye vision ili wapiga kura tumalizie kazi ...hawa wazee wakalee wajukuu na siasa zao za kilocal.Tunataka viongozi wa kuwaongoza watu kutumia rasirimali zao kujiendeleza na so viongozi was kwenda kuchuma na kuleta ili kuwaaminisha wananchi wasiwaze kwingineko,na kibaya zaidi sahivi ameanza tena kurumbana na watendaji wa manispaa badala ya kukaa nao walau wamsaidie hapa na pale
 
Yaani kwa sasa wazee mwisho hamjuju mjini hakuwafai
 
Ukichangia na hii meli walioichakaza serekali walikula hela alafu matengenezo hakuna
Ccm hawawezi kupata kura bk
 
Tatzo si Kagasheki: tatzo ni Ukawa hawana mtu mwenye ushawishi wa kulirudsha hili jmbo! Rwakatare kachokwa mpk yy kachoka! Jimbo liko nje nje kwa Ukawa lakn uzembe wa Ukawa ndo utasababsha Kagasheki arud tena!
 
Yaani kwa sasa wazee mwisho hamjuju mjini hakuwafai

Hamjuju ni soon ndugu yangu breki ikikugomea pale utatamani Israeli akuchukue fasta.Kwani vip ile stand ya kyakailabwa imefikia hatua gani?
 
Ukichangia na hii meli walioichakaza serekali walikula hela alafu matengenezo hakuna
Ccm hawawezi kupata kura bk

Marire hebu msome Black fire naona comment yake ina mantiki ama wewe unaichukuliaje mkuu?
 
Kiukweli Bukoba ni wilaya inayostahili kuwa na hadhi fulani lakini haitendewi haki
 
Kiukweli Bukoba ni wilaya inayostahili kuwa na hadhi fulani lakini haitendewi haki

Ndo hivyo mkuu ila daima ukweli haufichiki,fitina za CCM ni nyingi mno katika hili lakini Siku moja yaweza kuwa kubwa kupita muongo mzima
 
Yomaweee kubakisii yaani stand haijawekewa lami, aaah delete hao ccm fasta
 
Yaani stand imekuwa ya watu wa boda boda badala ya mabasi ile ya kyamirwo ni hadithi

11037776_10153130534094693_3021568554152694940_n.jpg


Meri nayo taabani ccm ni lazima ku-delete kabisa

10614306_10152597592699693_8164024353418616207_n.jpg10614306_10152597592699693_8164024353418616207_n.jpg10614306_10152597592699693_8164024353418616207_n.jpg
 
4B.jpg


Huyu ndiye Meneja kampaini wa kagasheki kwa mwaka huu wa 2015.Anaitwa Jumanne Bingwa. huyu ni dk tano mbili,anatumia viroba kama hana akili nzuri,anatembea na vichu na nyembe. ndiye msemaji wake mkuu na ndiye anampangia mipango ya jimbo bukoba pole sana-HAPO CHINI MTAZAME KWENYE KIKWAPA MKOO WA KUSHOTO
DSC04196.JPG
 
Mwaka huu akiiba na sisi tutaiba..Lwakatare ni MTU mwenye maono ya kutupa bukoba tuitakayo.
Mungu atampigania na kila mwana Bukoba mweye akili timamu am support Rwakatare.
 
Tunataka mtu was kujua namna ya kuzitengeneza beach za mwambao was ziwa kwa ajiri ya kuweka vivutio vya uchumi na utalii,mahoteli, n.k,mtu wa kukiona kisiwa cha Musira kama fursa ya kiuchumi kukifanya kivutio kikubwa na kuwashawishi wenye pesa kupeleka miundombinu pale ili pawe kama Brunei,mwenye maono ya kujua kwamba tayari pale ni kiungo cha mikoa baki na nchi za upande huo kwahiyo kuweka mambo yanayoendana na muingiliano huo wa masoko ...haya yote yamewashinda CCM kwa zaidi ya miaka 50 na hakika hawayawezi tens,tunahitaji vijana kutoka Ukawa wayatatue haya
 
Back
Top Bottom