mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,789
- 7,181
- Thread starter
- #21
Tunataka mtu was kujua namna ya kuzitengeneza beach za mwambao was ziwa kwa ajiri ya kuweka vivutio vya uchumi na utalii,mahoteli, n.k,mtu wa kukiona kisiwa cha Musira kama fursa ya kiuchumi kukifanya kivutio kikubwa na kuwashawishi wenye pesa kupeleka miundombinu pale ili pawe kama Brunei,mwenye maono ya kujua kwamba tayari pale ni kiungo cha mikoa baki na nchi za upande huo kwahiyo kuweka mambo yanayoendana na muingiliano huo wa masoko ...haya yote yamewashinda CCM kwa zaidi ya miaka 50 na hakika hawayawezi tens,tunahitaji vijana kutoka Ukawa wayatatue haya
Hakuna kitu kinaniuma kuona mji wa BK uko vile , zamani kulikuwepo mpaka suti made in BUKOBA zinauzwa bei gari, Tangu IDD AMINI ajambie mji huu tukaingia kwenye vita serikali ilitupa kule. Kila mara marais wanakuja kuangalia sanamu la mayunga kama nembo ya ukombozi kutoka nduli Amini lakini kufikiria kuwa BK ni mji wa kihistoria hakuna.
Tuna beach safi, lakini wawekezaji kwenye utalii hakuna. Naona angalau vijana wetu wakina JAMKO na Bukoba wadau angalau wanaitangaza, tuwape nguvu. Mtoeni mbunge huyu hana ubunifu wakati alikuwa wizara nyeti ya utalii