Ubunge ubungo: nape vs mnyika=loss | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubunge ubungo: nape vs mnyika=loss

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Raia Fulani, Jul 19, 2010.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nape katangaza kuwania ubunge kupitia jimbo la ubungo. Kati ya wagombea watano wa ccm waliotangaza nia ni wazi kuwa nape atapenyeza na hatimaye kukutana na kijana mwenzie, mnyika kwenye mchuano wa kuwania jimbo la ubungo. Ni wazi kuwa vijana wote wawili wanakubalika. Kwa nini huyu nape asingechagua jimbo jingine kama ilala (ambapo kuna washindani wawili tu ikilinganishwa na majimbo mengine?), segerea, ukonga ama temeke? Kwa nini wanyang'anyane hii nafasi ilhali wote wanahitajika bungeni? Haoni busara za mzee sabodo? Kilichotakiwa ni kuwa mdee akamate kawe, mnyika ubungo na nape kati ya hayo yaliyotajwa juu. Binafsi kwa wakati huu nisingependa kumpoteza mnyika wala nape. Vinginevyo vijana wenzangu msitake tutake kuamini maneno ya cheyo kuwa mjipange kiuchumi na kijamii kwanza ndipo mfikirie ubunge wakati umri umesonga kiasi. Ningependa sana kuwaona wote wawili bungeni Dodoma
   
 2. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu tatizo ni kwamba siasa haiko hivyo...
   
 3. K

  Keil JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Kingi,

  Ukiona mtu ametangaza kuwania Ubunge jimbo fulani ni kwamba anaangalia ni wapi anakubalika zaidi na je uwezekano wa kushinda ukoje. Hayo majimbo mengine uliyoyataja yawezekana Nape hakubaliki na hata akienda kugombea huko haoni kama anaweza kushinda.

  Kwani hujajiuliza ni kwanini Fred Mpendazoe ameamua kugombea jimbo la Dar wakati miaka 5 inayoisha alikuwa anawakilisha Jimbo la Kishapu?

  Waache wachuane, ingawa nina mashaka sana kama jina la Nape linaweza kuvuka kwenye vikao vya chama. Misuguano iliyotokea ndani ya UVCCM na kupelekea kijana kumwaga kila kitu hadharani kuhusu ufisadi wa upangishaji wa Jengo la UVCCM Makao Makuu, ambao unamgusa moja kwa moja EL unaweka mashaka kama kijana anaweza kupenya.
   
 4. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  basi nape akiona akiona anabaniwa aje chadema kwa watu makini. Pia kwa waliotajwa kuwania ubungo kupitia ccm sioni ambaye anaweza kumchalenji mnyika zaidi ya nape. Na kwa jinsi ccm wanavyotaka kushinda kila eneo, watamweka na akifanikiwa kupita watamnywesha maji ya bendera ya chama
   
 5. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  ehivi chama makini ni chadema ? hii ni chai isio na faida yeyote
   
 6. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  mbona watu kama Sabodo hawakutoa shavu kwa vyama kama CUF na wengine? Hapo ujiulize na utapata jibu tu. Ilianza NCCR, kisha CUF, na sasa CHADEMA
   
Loading...