Ubunge na u-RC, u-DC au DED kipi zaidi?

luirhu

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
800
412
Kufuatia kauli ya mhe. Rais Magufuli kuwa kuna baadhi ya viongozi wana tamaa ya kuto kuridhika na walicho nacho haswa ma RC, DC Na ma DED kutaka nyadhifa ZA juu zaidi ni fundisho tosha Kwa walio sikua, kweli hata mimi nasema hiyo ni tamaa na siku zote mtaka yote hukosa yote.

Kuna watanzania wengi tu hawana kazi wewe Mungu amekujaalia umeupata ukuu wa mkoa au wilaya au ukurugenzi bado tena unataka ukawazibie wenzako kwenye nafasi ya ubunge duh!! Hii ni tamaa ya fisi!! Na chini ya awamu ya Rais Magufuli mtachezea kichapo! Na kama tabia hii ikiachwa ikajengeka Kwa kigezo cha demokrasia kila mkuu wa mkoa, wilaya au Mkurugenzi watakuwa wanajijenga Kwa malengo ya kugombea ubunge badala ya kutumikia wananchi, asante JPM Kwa kuliona jambo hilo Na kulikemea wenye masikio wameelewa.

Nafasi mnazo teuliwa Na Mh Rais sio za kujiimarisha Na kujijenga kisiasa bila ni nafasi ya kutumikia wananchi Kwa nguvu zako zote, utendaji wako mzuri ndio mtaji wako wa badae, tunaamini kila jambo anapanga Mungu.
 
bilashaka ubunge utakuwa mtamu zaidi kwa wenye kupenda maslahi ya fedha, ndio maana wana siasa wanapambana kufa na kupona.
lkn safari hii tuchague viongozi waadilifu hao ndio watakao tuletea maendelea,
wachumia tumbo safari hi basi..
 
Wanadai ukipata ubunge kuna nafasi kubwa ya kuwa naibu au waziri so utavaa kofia mbili kwa wakati mmoja na mishahara unakula kote kote(ubunge&uwaziri).
 
Mi naona mkuu wa mkoa Dar es salam aliwaamuru waunge wote a wako bungeni wakamatwee hivyo ni zaidi ya ubunge.
 
kuna hatari kubwa ya kupeleka wabunge wenye njaa/wachumia tumbo..na hao ndio walio wengi, ukimuona yupo tayari kutoa rushwa...ujue huyo ni moto wa kuotea mbali.
yatupaswa tuwe makini sana ktk kuchagua viongozi sahihi na haswa wenye uchungu na shauku ya kutuletea maendeleo
 
Vyeo vya kuteuliwa ni kamd vile vya kuandikwa kwa pensel, ajira yako inategemea Bosi kaamkaje?

Ukiwa Mbunge una uhakika wa miaka 5 labda litokee sijui balaa gani!

Amor Makala yupo wapi
 
Uroho wa na uchu wa madaraka ni moja kati ya vitu vinavyo litesa bara la Afrika Tamzania ikiwemo. Wanasiasa wanahamgaika kutafuta uongozi kwajili ya kujineemeaha wao na familia zao badala ya kufikiria masikini wasio jua hatuna yao ya kesho,
Kila mmoja anuwania ubunge kwa udi Na uvumba .......
 
Kufuatia kauli ya mhe. Rais Magufuli kuwa kuna baadhi ya viongozi wana tamaa ya kuto kuridhika na walicho nacho haswa ma RC, DC Na ma DED kutaka nyadhifa ZA juu zaidi ni fundisho tosha Kwa walio sikua, kweli hata mimi nasema hiyo ni tamaa na siku zote mtaka yote hukosa yote.

Kuna watanzania wengi tu hawana kazi wewe Mungu amekujaalia umeupata ukuu wa mkoa au wilaya au ukurugenzi bado tena unataka ukawazibie wenzako kwenye nafasi ya ubunge duh!! Hii ni tamaa ya fisi!! Na chini ya awamu ya Rais Magufuli mtachezea kichapo! Na kama tabia hii ikiachwa ikajengeka Kwa kigezo cha demokrasia kila mkuu wa mkoa, wilaya au Mkurugenzi watakuwa wanajijenga Kwa malengo ya kugombea ubunge badala ya kutumikia wananchi, asante JPM Kwa kuliona jambo hilo Na kulikemea wenye masikio wameelewa.

Nafasi mnazo teuliwa Na Mh Rais sio za kujiimarisha Na kujijenga kisiasa bila ni nafasi ya kutumikia wananchi Kwa nguvu zako zote, utendaji wako mzuri ndio mtaji wako wa badae, tunaamini kila jambo anapanga Mungu.
UBUNGE UNALIPA ZAIDI
 
kuna haja serikari kurekebisha mafao wanayopata wabunge, maana maslahi manono anayoyapata mbunge yanaondoa kabisa lengo la mbunge kuwa mtumishi wa wananchi badala yake kila anaye gombea ubunge anatamaa ya kunufaika either na mafao au kuupata uwaziri.
hii inajenga tamaa kubwa sana kwa wana siasa kujinufaisha,
ikiwezekana mbuge asilipwe mishahara miwili yaani ya ubunge na uwaziri hii pia itaondoa tamaa kwa kila mtu kuutaka ubunge
 
Kwa masilahi ya pesa / uchumi ubunge uko juu sana, unalipa zaidi. Kwa masilahi ya mamlaka hivyo vingine ulivyotaja viko juu ya ubunge.
 
Back
Top Bottom