Ubunge Mbeya mjini 2015

zulu12

Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
58
Reaction score
11
Jamani mbunge sugu anapendwa sana mbeya na mimi pia nampenda sana ingawa si mkazi wa jimbo hilo ila kuna wasiwasi kwenye mchakato wa 2015 watu wachache wakashindwa kumpa kura yeye na wakampa mtu mwingine ndani ya cdm,wote tunaelewa jimbo la mby mjini ni la chd hata kama watasimamisha kisiki kipambane na ccm basi ccm itashindwa,kwa hiyo sugu kwa muda uliobaki ajitazame kwani watu wanampenda na pia manunguniko yao anayajua so anaweza kujisafisha vizuri.

Hiyo ni hali halisi ya jimboni kwa mr two proud,anapendwa sana sana
 
Be clear, specify your objective[ s].
 
Kuna malalamiko ya hapa na pale ambayo anaweza kuyarekebisha ,kwamba ofisi anafunga muda mrefu na kubandika karatasi nje eti yuko nje kikazi,mtu wa kumsaidia mbunge ni msanii mwenziwe na muda mwingi ofisi inafungwa,na bungeni eti anaongea usaniii tuu hatetei watu wa mbeya ,halafu la yeye kuachia chama mkoa kukijenga yeye akiwa nje zaidi ya mkoa, akitafuta credit za kisiasa kwa viongozi, nadhani akitulia haya mambo yanaweza kunyooshwa tu na yeye mwenyewe bado upepo upo kwake lakini japo manung'uniko yanakwenda kwa kasi ya moto wa upepo
 
Ni muhimu kuwasikiliza wapiga kura wake maana ndiyo mabosi wake.Mimi pia ningefurahi kama wabunge wa kanda hiyo wakashirikiana kueneza chama kwenye kanda yao zaidi na kuhitaji nguvu ya wabunge/viongozi wa chadema mara moja moja tu . Kituo cha M4C kwa kila mbunge kiwe kwenye kanda yake, aende sehemu nyingine tu iwapo kuna nguvu yake inahitajika eneo hilo.
 
Comrade hujaeleweka kwa maslai ya chama taifa na mkoa kwa ujumla liweke sawa hili,ili tukuelewe
 
Wananchi wa Mbeya ni waelewa sana hawawezi kutoa judgement za kijinga. Mh. Sugu anapigania ukombozi wa taifa lote.
 
Be clear, specify your objective[ s].

No evidence no right to say....! Kuna manung'uniko Jimboni kwake yapi yataje basi ili tuchangie na utakuwa umemsaidia Mh. kujua ni wapi wananchi wanatatizo naye...
Sasa mara anapendwa mara atapigwa chini which is which...?
Weka vitu km Great thinker na cyo brabraaaa...!
 
nafikiri katika lengo la msingi mleta mada akasau aliyoyataka kusema akikumbuka atatuelewesha zaidi
 

yani sijui ulitaka kusema nini kwani kama wachache hawata mpa si bado atashinda maana wengi bado watampa.
umesema wanampenda sana, wananungunika'nini? na yeye anayajua yapi?
ukahitimisha na anapendwa sanasana?!!!!!!

labda ungekuwa msaada ungetaja hayo malalamiko ili tujue ili tuchangie otherwise hujasema kitu.
 
au ulikuwa unataka kutuonesha unavyompenda mbunge wako.
 
Embu andika kwa kingreza, inaonekana kiswahili si lugha yako ya asili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…