Ubunge Arumeru Mashariki utakuwa mgumu sana

:yawn:
Tuweni na ubinadamu kidogo jamani kha!! Shetani gani huyo? Kweli wenzako wanalia kwa kufariki kwa mpendwa wao wewe unakuja na threads za kutaka jimbo? Mods naomba kwa heshima ya JF hii thread ifutwe.

Wachawi husema kufa kufaana.
 
Siasa za Arumeru Mashariki zitapamba moto leo makanisani. Watu watahakikisha wanaenda makanisani hata kama hawaiendagi ili kuhakiksha kuwa wanafanikisha malengo yao. Lakini kwa vyovyote vile jimbo la Arumeru ni la Joshua Nasary ingawa nina wasiwasi kuwa anaweza akanunuliwa na rangi ya kijani kuwa mgombea wake.
 
Kuna wapambanaji hapa Mbuguni walishaanza maandalizi ya uchaguzi siku kura za 2010 zilipotangazwa kwani kila mmoja alijua Marehemu Sumari hakustahili ushindi. Magamba hawana chao huku, tangu enzi za Talala Mbise tulishawachoka. Wamekuwa wakishinda kwa hila, safari hii hawatoki.
 
Back
Top Bottom