Ubovu wa product ya Mo ukwaju

kuna zao huko mbeleni litakuja kuwa almasi nishanunua shamba nimepanda vyema,subira yavuta kheri
 
Hiyo MO ni flavoured drink sio ukwaju halisi...
ndo mana hata bei ni kidogo cheap...!!

Ila bakhera kuanzia embe, ukwaju, chungwa na nanasi anakamua mwenyewe just anaongeza CMC tu kwa baadhi ya juice kuifanya juice iwe nzito...
Vinywaji karibu vyote vya mo huwa anaingiza nchini mchanganyiko ulio tayari, yeye ni kuuweka tu kwenye chupa!! Hana kiwanda hapa!! Na ndio maana huwa unaona yana radha ya ajabu ajabu tu
 
Kwenye mambo ya biashara kuna vitu wanaita #FollowFast

Yaani ukiona mpinzani wako ( Hususani Wanaoitwa Smart Money ) anafanya kitu na kimepokelewa vyema.

Cha Kufanya Ni Kukopi Fasta Iwezekanavyo.

Mabingwa Na Mbinu Hii Ni wachina na wamefanikiwa sana.

Kama Unaogopa Sana Ushindani Dunia Hii Kama Magufuli, Then You Better Quit.

Kitakachokutofautisha Wewe Na Washindani Wako Ni Marketing, Formulation Na Branding Tu .

Hata Hao Azam Mbona Walikopi CocaCola Wakata Azam Cola Pamoja Na Malta
 
Hapa kuna simba na yanga! Hyo ni ukwaju mm ninainywa na iko poa! Ww unajua kupima ubora kuliko TBS na TFDA?
 
Mi nimependa huu ukwaju wa Mo kuliko wa Azam. Ajabu wanaolalamika hakuna aliesema alishindwa kumaliza after some few sips.Kama umekunywa kichupa chots basi ukwaju huu uko sawa kwa walengwa😃
 
kwahio ulitaka same quality for half the price ?, You get what you pay for...

Copy and Originality..., wote hao wanacopy in this day and age, vitu vichache sana ni original under the sun.... issue za beverages sio Azam wala Mo ambao ni waanzilishi.....
 
Hapa kuna simba na yanga! Hyo ni ukwaju mm ninainywa na iko poa! Ww unajua kupima ubora kuliko TBS na TFDA?

Sina ushabiki wakipumbavu kabisa mpk kuleta kwenye chakula , kwani TFDA na TBS wanapima ubora au radha Tuanzie apo kwanza?

Ukweli acha usemwe MO hana ubunifu nikukopy kila kitu na anakopi katika low quality , wewe unakunywa coz ni mshabiki wa simba ila habari unayo ukimaliza kunywa uo wa Mo , pitisha na wa Azam afu kaa chini tafakati jipige kifuani ukisema mimi ni mjinga
 
Mimi niliacha zamani sana kutumia bidhaa za MO, kuna juisi ilikuwa na jina PRIDE wakati imeingizwa sokoni ilikuwa ikikaa muda fulani inajichuja, chini rangi nyingi juu Maji matupu, kuanzia hapo sijawahi kuamini tena bidhaa zake, hata Maji ya maisha au masafi nayo yalikuwa yakikaa siku chache tu yanabadilika rangi, totally bidhaa zake zinachakachuliwa sana.
 
Hakuna kitu kipya duniani vitu vyote viliwai kuwepo ila vinafanyiwa ubunifu na ndipo apo tunaita creativity na kuadd value ila Mo anachofanya ni kukopy na kupaste kitu kinacho leta utofauti kati ya mchuuzi na mjasiliamali
Azam ni mjasiliamali ila Mo ni mchuuzi

Usiwe na mtazamo huo unakumbuka issue ya mifuko plastic (Rambo) iliyokuwa na picha za akina Rambo na wengine tulielezwa kuwa haina na ikaamriwa itolewe sokoni kisha ikaeletwa hii ya sasa au hukuwepo kipindi hicho? Pia hii tulioambiwa ina ubora nayo pia imezuiliwa, TBS Ndio walioiruhusu kuingizwa sokoni.
 
Hope december Mungu akipenda nta introduce kitu changu katika market since nimemaliza fanya reserch yake for six month so stay tune

Alafu kingine boss sijasema kwa nia mbaya ila ukweli umuweka mtu wazi najua atapata wasaha wakupitia mawazo ya uzi huu na atajua wapi pakurekebisha
Sina tatizo na bidhaa za Mo ila mimi ni mtu ninaependa vitu vizuri skuzote hivyo sioni aibu kusema kuwa kitu fulani nikibaya na ukweli ni kua BIDHAA HII NI MBAYA kwa mtu aliekunywa Azam ukwaju anaweza toa comment zake na ukweli ni kuwa Azam amewekeza sana na yuko na watu makini katika maswala ya food production

Hivi aliwahi kutoa bidhaa nzuri hata mara moja?
 
Watanzania hatujambo kwenye upingaji na ukosoaji wakati hatujui kitu
 
Azam hatengenezi juice za matunda halisi. Anakamua pulp anauza Kenya
Hiyo MO ni flavoured drink sio ukwaju halisi...
ndo mana hata bei ni kidogo cheap...!!

Ila bakhera kuanzia embe, ukwaju, chungwa na nanasi anakamua mwenyewe just anaongeza CMC tu kwa baadhi ya juice kuifanya juice iwe nzito...
 
Vinywaji karibu vyote vya mo huwa anaingiza nchini mchanganyiko ulio tayari, yeye ni kuuweka tu kwenye chupa!! Hana kiwanda hapa!! Na ndio maana huwa unaona yana radha ya ajabu ajabu tu
Wewe huna akili. Hakuna mtu anaweza fanya huo ujinga. Viwanda vyote vya soda na vinywaji Tz hununua flavours nchi tofauti na kuja tengeneza syrup hapa Tz na kupack.
Muwe hata mnasoma au kutembelea youtube
 
Watanzania ni wavivu na wao siku zote wanamuona MO tu.
Jambo, Afya, Sayona hawa wote wana bidhaa sawa kwa soko lile lile.

Azam yeye katoa ukwaju. Mo katoa Radha ya Ukwaju.
Kama mtu huwezi lipa 600 basi utapata kwa 300.

Umasikini wetu ndio chanzo haya masoda ya hovyo tungekuwa na uwezo wa kununua juice za maana majuice ya kina Azam tusingeyanunu.
Kuna juice zinatoka nje zinauzwa ghali ila watu huzinunua sana kuliko za azam
Kwenye mambo ya biashara kuna vitu wanaita #FollowFast

Yaani ukiona mpinzani wako ( Hususani Wanaoitwa Smart Money ) anafanya kitu na kimepokelewa vyema.

Cha Kufanya Ni Kukopi Fasta Iwezekanavyo.

Mabingwa Na Mbinu Hii Ni wachina na wamefanikiwa sana.

Kama Unaogopa Sana Ushindani Dunia Hii Kama Magufuli, Then You Better Quit.

Kitakachokutofautisha Wewe Na Washindani Wako Ni Marketing, Formulation Na Branding Tu .

Hata Hao Azam Mbona Walikopi CocaCola Wakata Azam Cola Pamoja Na Malta
 
MO hapa amechemka
Habari za muda huu wana bodi.

Moja kwa moja nijikite katika mada leo mchana nimepata kutumia bidhaa hii mpya sokoni kutoka kampuni ya uzalishaji wa vyakula, vinywaji na vitu vingine (inayosimamiwa na Mohamed Dewji)

BEI YA BIDHAA
Bidhaa hii mpya sokoni inaenda kwa bei ya Sh 300 tu pesa taslimu ya kitanzania hivyo kuifanya iweze kupenya ipasavyo kwa watumiaji wengi yaani watu wa market tunasema ametumia penetration pricing strategy kuifanya bidhaa yake ikubalike kwa haraka ili kutengeneza customer base kubwa ukilinganisha na bei ya Azam ukwaju inayouzwa kwa Tsh 600 kwa 500 Tsh.

BIDHAA YENYEWE
Uongo mbaya na nisiwe mnafiki katika sehemu Mo alipofeli na team yake ni katika product hii kwa 100% zipo nyingine pia japo makosa yake sio makubwa sana kama hii,kwanza kabisa ubovu wa bidhaa hii ni

1. Ladha ya bidhaa
Sijajua fomula iliyotumika kutengeneza hii kitu asee yaani haieleweki ni chungu au tamu yani ladha yake ni mbaya kiukweli haielezeki watengeneza juice na lamba lamba wa mtaani wanatengeneza vitu vizuri zaidi ya hii ya Mo mara 200.

2. Muonekano wa bidhaa
Kiukweli bidhaa ya Mo inamuonekano mbaya sana (yaani namaanisha packaging yake imekaa kilocal sana) mithili ya kinywaji pendwa cha vijana wa mtaani au wapiga debe kinachoitwa double kick hivyo kupoteza mvuto na hamu machoni kwa mtumiaji.

UBUNIFU
Kiukweli Nimekuwa insipred sana na vitu Mo anavyofanya japo huwa nakwazika sana pale ninapoona anakosa ubunifu katika bidhaa badala yake anakopi kila kitu kwa mshindani wake Azam.

Mfano: MO PASSION= AZAM JUICE/AZAM COLA, UHAI=MASAFI, AZAM ENERGY DRINK= MO ENERGY, AZAM UKWAJU = MO UKWAJU

Ila pia katika bidhaa za unga na mafuta. Kiukweli MO amekosa watu wa Business Reserch na Marketing walio na weledi wakujua kitu gani soko linaitaji badala ya kusubiri mwingine alipowekeza juhudi zake ndipo na yeye apate wigo wa kukopi watu wa biashara wanasema kwa ufupi sio mtu wa kurisk sana.

Ni mtu anaetegea mpinzani aanzishe jambo yeye aje kukopi ila pia nlitegemea akikopi ideas aje na vitu bora kuliko mshindani wake mfano COCA COLA na PEPSI badala yake jina ndilo linauza kuliko bidhaa yenyewe.

NB: Ubora wa kitu unapimwa na bei pia kwa watu wa segment fulani hivyo kuweka price ndogo sio suruhisho bali kwa watu wengine uchukulia bidhaa kuwa ni mbovu sana.

Nawasilisha wanabodi

View attachment 1249397

MO amechemka sana, hii ukwaju wala si matunda halisi.

Wameweka kemikali nyingi sana ambazo si ukwaju halisi.
 
Back
Top Bottom