Ubovu wa product ya Mo ukwaju

Kenzpuls

Senior Member
Oct 22, 2019
171
500
Habari za muda huu wana bodi.

Moja kwa moja nijikite katika mada leo mchana nimepata kutumia bidhaa hii mpya sokoni kutoka kampuni ya uzalishaji wa vyakula, vinywaji na vitu vingine (inayosimamiwa na Mohamed Dewji)

BEI YA BIDHAA
Bidhaa hii mpya sokoni inaenda kwa bei ya Sh 300 tu pesa taslimu ya kitanzania hivyo kuifanya iweze kupenya ipasavyo kwa watumiaji wengi yaani watu wa market tunasema ametumia penetration pricing strategy kuifanya bidhaa yake ikubalike kwa haraka ili kutengeneza customer base kubwa ukilinganisha na bei ya Azam ukwaju inayouzwa kwa Tsh 600 kwa 500 Tsh.

BIDHAA YENYEWE
Uongo mbaya na nisiwe mnafiki katika sehemu Mo alipofeli na team yake ni katika product hii kwa 100% zipo nyingine pia japo makosa yake sio makubwa sana kama hii,kwanza kabisa ubovu wa bidhaa hii ni

1. Ladha ya bidhaa
Sijajua fomula iliyotumika kutengeneza hii kitu asee yaani haieleweki ni chungu au tamu yani ladha yake ni mbaya kiukweli haielezeki watengeneza juice na lamba lamba wa mtaani wanatengeneza vitu vizuri zaidi ya hii ya Mo mara 200.

2. Muonekano wa bidhaa
Kiukweli bidhaa ya Mo inamuonekano mbaya sana (yaani namaanisha packaging yake imekaa kilocal sana) mithili ya kinywaji pendwa cha vijana wa mtaani au wapiga debe kinachoitwa double kick hivyo kupoteza mvuto na hamu machoni kwa mtumiaji.

UBUNIFU
Kiukweli Nimekuwa insipred sana na vitu Mo anavyofanya japo huwa nakwazika sana pale ninapoona anakosa ubunifu katika bidhaa badala yake anakopi kila kitu kwa mshindani wake Azam.

Mfano: MO PASSION= AZAM JUICE/AZAM COLA, UHAI=MASAFI, AZAM ENERGY DRINK= MO ENERGY, AZAM UKWAJU = MO UKWAJU

Ila pia katika bidhaa za unga na mafuta. Kiukweli MO amekosa watu wa Business Reserch na Marketing walio na weledi wakujua kitu gani soko linaitaji badala ya kusubiri mwingine alipowekeza juhudi zake ndipo na yeye apate wigo wa kukopi watu wa biashara wanasema kwa ufupi sio mtu wa kurisk sana.

Ni mtu anaetegea mpinzani aanzishe jambo yeye aje kukopi ila pia nlitegemea akikopi ideas aje na vitu bora kuliko mshindani wake mfano COCA COLA na PEPSI badala yake jina ndilo linauza kuliko bidhaa yenyewe.

NB: Ubora wa kitu unapimwa na bei pia kwa watu wa segment fulani hivyo kuweka price ndogo sio suruhisho bali kwa watu wengine uchukulia bidhaa kuwa ni mbovu sana.

Nawasilisha wanabodi

f1d77b5a-e58b-403f-8b91-ba42bf08296d.jpg
 

Kenzpuls

Senior Member
Oct 22, 2019
171
500
Tuanze na ww umebuni nn kizuri apo ulipo na kikajulikana


unamwalibia mwenzako biashara hujui apo adi TBS wamepitamo, Tanzania tunajua kuponda badala ya kuweka mawazo ili aboreshe nn apunguze nn kwa bidhaa.
Hope december Mungu akipenda nta introduce kitu changu katika market since nimemaliza fanya reserch yake for six month so stay tune

Alafu kingine boss sijasema kwa nia mbaya ila ukweli umuweka mtu wazi najua atapata wasaha wakupitia mawazo ya uzi huu na atajua wapi pakurekebisha
Sina tatizo na bidhaa za Mo ila mimi ni mtu ninaependa vitu vizuri skuzote hivyo sioni aibu kusema kuwa kitu fulani nikibaya na ukweli ni kua BIDHAA HII NI MBAYA kwa mtu aliekunywa Azam ukwaju anaweza toa comment zake na ukweli ni kuwa Azam amewekeza sana na yuko na watu makini katika maswala ya food production
 

Kenzpuls

Senior Member
Oct 22, 2019
171
500
Tuanze na ww umebuni nn kizuri apo ulipo na kikajulikana


unamwalibia mwenzako biashara hujui apo adi TBS wamepitamo, Tanzania tunajua kuponda badala ya kuweka mawazo ili aboreshe nn apunguze nn kwa bidhaa.
Hakuna kitu kipya duniani vitu vyote viliwai kuwepo ila vinafanyiwa ubunifu na ndipo apo tunaita creativity na kuadd value ila Mo anachofanya ni kukopy na kupaste kitu kinacho leta utofauti kati ya mchuuzi na mjasiliamali
Azam ni mjasiliamali ila Mo ni mchuuzi
 

Deceiver

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
3,347
2,000
Kwenye ubora Mo hamkuti uncle Bakhresa. Anza na unga wa chapati wa mo. Ni hovyooo
Maji yake masafi mfuniko haufunguki vzr
Ukitaka kujichubua mikono au hata uso tumia sabuni ya unga ya Mo.
Ukitaka ujijazie sumu mwilini na kupungukiwa nguvu za kiume kunywa juice za Mo.
 

mo shyner

Senior Member
Aug 23, 2015
116
250
Kwenye ubora Mo hamkuti uncle Bakhresa. Anza na unga wa chapati wa mo. Ni hovyooo
Maji yake masafi mfuniko haufunguki vzr
Ukitaka kujichubua mikono au hata uso tumia sabuni ya unga ya Mo.
Ukitaka ujijazie sumu mwilini na kupungukiwa nguvu za kiume kunywa juice za Mo.
Utakuwa Jambo na Vijambo sio bure!
 

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
May 11, 2015
22,984
2,000
Hivi karibuni nimeona kabadili mifuniko ya maji yake kuwa mieusi yaani ipo kiganga ganga.

Maji ya Masafi yapo sokoni muda sasa ila hata wenyewe wameshindwa kujua yapo kwa sababu gani, leo unakuta maji yamefunikwa na mfuniko wa blue, kesho orange keshokutwa mifuniko mieusi unawaza hivi kampuni inafanya majaribio ya urembo wa chupa au ni nini!

Tazama Hill Water wamekuja na bidhaa bomba sana kuanzia kwenye maji yenyewe na vibebeo (chupa) yaani unakuwa comfortable kubeba chupa ya Hill popote kwa namna ilivyo katika umbo zuri na material magumu. Ila Uhai Drinking Water na Masafi Drinking water vibebeo vyao ni hovyo kweli.

Siwezi kuzungumzia bidhaa nyingine za Mo ila kwa biashara ya ushindani na utekaji soko ni wazi Azam anajua anachofanya ila huyu Mo na bidhaa zake kwangu naona ni bidhaa zisizo na ubora KWANGU.

Hajui kupangilia bidhaa zake.
 

Lyamber

JF-Expert Member
Jul 24, 2012
9,851
2,000
Tuanze na ww umebuni nn kizuri apo ulipo na kikajulikana


unamwalibia mwenzako biashara hujui apo adi TBS wamepitamo, Tanzania tunajua kuponda badala ya kuweka mawazo ili aboreshe nn apunguze nn kwa bidhaa.
Ajabu ni kwamba wewe mwenyewe pia unaponda
 
Top Bottom