Simba Mwepesi
Member
- Nov 17, 2022
- 19
- 11
Habari wanajukwaa. Leo nimekuja mbele yenu kuleta mada ihusiyo ubovu wa Barabara ya mwandege-mkuranga. Barabara hii ni muhimu kwa mikoa ya kusini kutoka Dar.
Kwa kweli barabara hii imejaaa makorongo na mabonde( tunaweza hata kufugia samaki). Kadhia tunayopata wasafiri wa njia hiyo ni kubwa..
Magari madogo upitaji wake ni mgumu kwa kweli hasa kipande Cha pale madafu mpaka vikindu. Mbunge wa mkuranga hii barabara hupitagi kweli?? Ninawaza kwa sauti, maana hata uzibwaji wa haya mashimo ulipofanyika mara ya mwisho ulifanyika kwa magumashi ndio maana haikupita hata wiki mbili mashimo yakarudi Tena.
Mkandarasi wa Barabara hii hauoni mashimo Yale yameongezeka? Kama barabara kubwa hali Iko hivyo. Je huko ndanindani Kama kazole, kitangwi, lugadwu etc Hali ikoje??? Maoni yangu ni haya, kwanza,mkandarasi tumia vifaa vizito kutengeneza barabara hii maana magari ya mizigo yanayopita hapa sio ya mchezomchezo.
Pili, ujenzi wa Barabara ya kongowe mpaka mbagala ukianza foleni yake itakuwa ni mara sita ya iliyopo kwa sasa,hivyo ni muda wa kutengeneza njia za mkato Kama Ile ya vikindu kutokea mwembe mtengu kupitia lugwadu ili kupunguza kadhia ya foleni.
Tatu, barabara ndio maendeleo, mbunge ipe kipaumbele barabara hii na maendeleo tutayaona, tazama barabara ya ubungo mpaka kimara, zamani ilikuwa ni sumbufu Sana Ila baada ya utanuzi ule, shida zimepungua Sana.
Ni mwendo wa kuteleza na kugusa chalinze. Awamu ijayo ni zamu ya mikoa ya kusini tumewasahau Sana, tuanze na hii barabara ya kuelekea huko mpaka mtwara.