Ubovu wa barabara Kahama

Ubovu wa barabara Kahama

Kama ilivyo ada 'siasa ni maisha na maisha ni siasa'

Kauli hii ni kweli over 50% siasa inaamua vitu vingi sana, kuanzia bei za bidhaa, kodi, miundombinu, utendaji nk...

Nimetafuta namna nzuri ya kueleza kero za Kahama nimeona sipatiwi majibu, moja ya njia nimejaribu kutumia sanduku la maoni pale Kahama Municipal lakini hakuna majibu yoyote.

1. Kahama barabara ni mbovu
Barabara ya Phantom - Mjini - mataa(kupanda na kushuka) - junction ya polisi - Kishimba secondary nk. hizi barabara ni kibovu sana kila mwaka marekebisho sasa hivi kuna vilaka na mashimo ya kutosha, utadhani ni rough road.

2. Barabara zote za rough road (mkazo barabara ya mama Farida, Mungula - Nyandekwa-..., Dodoma mwisho wa rami - Kilago -....)

3. Hivi pale Lumambo hakuna namna barabara ikawa designed round about/keep reft, au zikawekwa taa za kuongoza magari?.

4. Kuna tuta kubwa pale lumambo lakini hakuna alama yoyote ya kuonesha kuwa kuna tuta wala tuta.

Mkurugenzi, Mkuu wa wilaya, Tanroad na watendaji wengine kama mtaona bandiko hili jitahidini kufanya marekebisho, hali si shwari.

Machepele Tanzania
Kahama.
Kahama Yangu hii yaani Acha tuu.

1) Kokote Duniani huwezi kujipodoa halafu ndio uende ukaoge. Au kwa akina mama apoge ka-poda mashallah, halafu akatemebee kwenye Mvua bila mwamvuli.

Sasa sisi Kahama kwa sababu za kutaka kupata teuzi na kuridhisha mamlaka za uteuzi bali sio kuwahudumia watu wa Kahama; viongozi wengi katika.manispaa yetu kazi yao kubwa ni kutupakia Mji poda bila kutuosha kwanza au kutununulia mwamvuli.

Mji huu hauna miundombinu yoyote ya ya kushughulika na uondoaji wa maji katikati ya Mji, (storm water drainage) Matokeo yake kwa sehemu kubwa ni athari ya kukosa miundombinu ya kuyaondoa maji mjini.

Sasa ninangoja siku ya kuweka miundombinu hiyo watayapeleka wapi maana Majengo chini ya Sokola ndiko maji mengi yalikuwa yakielekezwa nako kumejaa ujenzi. Mungu Atusaidie.

2) Kahama ni wazee kwa kukata Kona na ni mji ambao kisiasa (kwa sababu umekwisha kujulikana una watu wenye bongo hafifu wengi) unatumika kuhadaa watu ili kupata kura tuu. Hakuna lengo la msingi la kuujenga.

Huwezi ukaipa Kahama mradi wa kujenga barabara wa TACTIC ilhali unajua Mji hauna mfumo wa maji taka. Lengo ni nini hasa. Kwamba kesho uanze kuzichimba barabara mpya ili kupitisha mfumo wa majitaka?!

Au zisipoharibika kwa sababu hiyo ya ujenzi wa mfumo wa majitaka basi ziendelee kujengwa juu ya uji wa tope la kinyesi?! Maana mji mzima umejaa maji ya bafuni na chooni; tumeamua kuyapanda kila kiwanja utadhani yanaota, halafu uongeze na maji ya Mvua; ni kuchezea fedha ukiniuliza.

Ila kwa kuwa itawapa kura na kuwabakiza kwenye teuzi zao wanakwenda kujenga anyways na mkurugenzi wao kiburi.

3) Kahama imekuwa haraka sana katika miji mingi Nchini na Afrika Mashariki....lakini serikali imeshindwa kung'amua haraka aina ya watumishi wanaotakiwa kuihudumia wanapaswa kubadilika.

Ni mji ambao kiutendaji bado unajitafuta kwa maana ya utamaduni wake. Ni wakati ambao serikali ilipaswa kupelekwa watu wenye weledi mkubwa na exposed enough ili watie chachu ya mabadiliko ya kitabia kwa watumishi na watawala.

Ila kwa Sasa imejaa wapiga dili na wao maeneo kuharibika wala haiwatishi. Kwa maana wamefikia ukomo wa utatuzi wa changamoto za Mji. Kazi kwao ni kubwa mno kuliko uwezo wa Leo na wa kesho.

Mungu Atunusuru.
 
Back
Top Bottom