Uboreshaji mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji nchini ulivyolenga kutatua tatizo la ajira

Chee4

Member
May 17, 2021
35
125
Historia inaonyesha nchi nyingi zilifanikiwa kuvunja mzunguko wa utegemezi kwa kuanzisha viwanda vya kuzalisha bidhaa mbalimbali.

Serikali ya Awamu ya Tano ilijenga msingi mzuri wa Sekta ya Viwanda kwa kuja na sera ya “Tanzania ya Viwanda” ambayo hadi sasa Serikali ya Awamu ya Sita inapita mule mule kwa kuboresha mazingira ya uwekezaji, na ndio sababu kubwa ya kaulimbiu - KAZI IENDELEE.

Mama yetu, Rais Samia Suluhu Hassan anatambua umuhimu wa kukuza Sekta ya Uwekezaji ili kuongeza fursa za Kiuchumi kwa Wananchi na ndio maana tumeshuhudia akikutana na Viongozi mbalimbali wakiwemo Marais wa Nchi Jirani ili kufanikisha azma yake hiyo.

Katika kila hotuba yake haachi kugusia suala la kuboresha mazingira ya Biashara na Uwekezaji. Kwa mfano, Wakati akifungua kiwanda cha Ushonaji cha Jeshi la Polisi, Kurasini - Dar es Salaam, alisisistiza Wananchi na Taasisi za Serikali kuongeza juhudi katika uwekezaji wa viwanda ili kupunguza gharama ya kuagiza bidhaa kutoka nje ya Nchi.

Uanzishwaji wa viwanda utatengeneza ajira kwa Wananchi kwani viwanda vinapoongeza Uzalishaji vinakuwa na uwezo wa kuajri watu wengi. Pia viwanda huchochea mageuzi ya mfumo wa uchumi katika sekta ya kilimo, na kuwapa manufaa ya moja kwa moja wakulima wa Nchi yetu, ambao ndio idadi kubwa ya Watanzania.

Hivyo basi uanzishwaji wa viwanda na kupanuka kwa viwanda hivyo kutaiongezea Serikali mapato na kuwa na uwezo wa kuhudumia wananchi wake kwa kuwapatia elimu bure, maji safi na barabara nzuri n.k

Mwisho, jana Bungeni Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa mikakati ya ujenzi wa viwanda ndiyo jibu sahihi la kupunguza tatizo la ajira.
 
Back
Top Bottom