Uboreshaji daftari la mpiga kura upo palepale

Uboreshaji daftari la mpiga kura upo palepale

Joined
Apr 4, 2020
Posts
16
Reaction score
7
1586406533702.png


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,(NEC), Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage amesema, utekelezaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili pamoja na uwekaji wazi daftari upo pale pale.

Amesema hayo leo Aprili 8,2020 wakati alitoa mrejesho wa kikao kilichofanyika Machi 23 mwaka huu ambacho pamoja na mambo mengine kilijadili kuhusu mambo hayo mawili. "Tulishauriana na wadau na baada ya mashauriano tutaendelea na mazoezi haya yote mawili kwa kuzingatia athari za virusi vya corona, tumeshanunua vifaa vya kujikinga na ugonjwa huo na kutoa maelekezo kwa watendaji kuzingatia miongozo ya afya."Uwekaji wazi daftari utakwenda sambamba na uboreshaji wa daftari awamu ya pili ambao utaanza rasmi Aprili 17, mwaka huu."
 
Mbunge wa viti maalumu, ndugu Bulembo na mwanae, wanasema tusifanye uchaguzi, bajeti iende kwenye Corona, sasa daftari wanabolesha la nini?
 
Back
Top Bottom