Ubora wa Yanga uko hapa..

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,517
Najiepusha kuzungumzia matokeo ya leo pale Kwa Mkapa. Kwa Yanga hii, Simba haifui dafu. Simba walipotoka sare mbili na Al Ahly nilisema kuwa walikutana vibonde watupu. Wababe wa AFL wanacheza baadaye: Wydad v Mamelodi

Ilipotoka ratiba kuonesha kuwa Yanga amepangiwa mechi nne 'ngumu' mfululizo za Azam, Singida BS, Simba na Coastal Union wengi wasiofahamu uimara wa Yanga hii walipatwa na uoga.

Lakini, hadi leo hii Yanga wameshakusanya alama tisa kwa kushinda mechi tatu mfululizo dhidi ya Azam, Singida BS na leo amekandwa Simba. Sasa amebaki Coastal Union. Yanga yaweza kuzoa alama zote 12 katika mechi nne hizi.

Yanga hii ni hatari...ni kiboko. Hata wapinzani kwenye klabu bingwa wanakaa mkao wa kula..wanakaa kwa uoga na tahadhari kubwa. Yanga hii ina morali kubwa hasa kipindi cha pili.

Yanga iko vizuri. Simba wajipange sana...labda kama derby ingechezeshwa na....
 
Mkuu bado hujausema ubora wa yanga.

Kwangu naona yanga wana nguvu kubwa saana pale katikati.. Unapocheza na yanga, wana wachezaji watano ambao kiasili ni viungo, unahitaji ukabaji wa hali ya juu na nidhamu kubwa mnoo kuwadhibiti, pacome, maxi na azizi kimsingi ni viungo kabisa, kwenye mfumo wanaonekana kama mawinga kiuhalisia si mawinga.
 
Hata Tatu angekuwa refa bado kipigo kingekuwepo .

Ile mechi ya tanga simba walibebwa na kila mtu aliona maamuzi yalikuwa poor.

refa wa leo amejitahidi .

Simba waliingia kifaza hasa yule msemaji wao uchwara anayewapa sifa zisizostahili eti anasema ana mkaribisha gamondi Kwenye mazoezi hivi anapima anavyozungumza au anakuwa amelewa??
 
Waambie warudiane hata usiku huu waone kama simba anamuweza Yanga.
Simba alipopigwa kitu akapmba kichomolewe ili apate kujamba ile mechi ya ngap ya jamii ilileta picha haiwezi kushinda mechi yoyote Tena.

Walipigwa mbili kavu zote zikawa ofside, huku wakiendelea kudondosha miuno na kupoteza mpira kila wakiumiliki. Hata walitaka kesho, tutaenda hukohuko boko
 
Mkuu bado hujausema ubora wa yanga.

Kwangu naona yanga wana nguvu kubwa saana pale katikati.. Unapocheza na yanga, wana wachezaji watano ambao kiasili ni viungo, unahitaji ukabaji wa hali ya juu na nidhamu kubwa mnoo kuwadhibiti, pacome, maxi na azizi kimsingi ni viungo kabisa, kwenye mfumo wanaonekana kama mawinga kiuhalisia si mawinga.
Upo sahihi kabisa na engine ya Yanga ni Aucho. Huyu ndiye roho ya Yanga.
 
Back
Top Bottom