Ubora wa mbao za Mtiki

akili akili

JF-Expert Member
May 5, 2014
1,732
1,095
Wadau, naombeni ushauri hukusu ubora wa mbao za huu mti uitwao Mtiki katika kitengeneza milango ikilinganishwa na mninga au mkongo. Kuna mdau ananishawishi kwamba wenyewe ndio the best, ingawa majority wanapigia chapuo mninga. Ushauri please.
 
mti bora kuliko wote duniani ni mninga, kuna kabati alichonga mzee enzi mimi sijazaliwa na lipo mpaka sasa na mbao zipo imara vile vile anachofanya yeye ni kupiga vanish tu, ni miaka 20+ sasa
 
Hapa ndipo panaponichanganya sasa, maana mwingine ananiambia mkongo ndio mwisho wa habari zote.
 
trust me, mninga ndo mti bora wa miaka yote pia hata gharama yake si mchezo na haupatikani kila nchi, tuna bahati sisi kuwa nao, muulize fundi yoyote atakueleza, hizi mbao nyingi tunazoziona ni mipodo na sio imara
 
mti bora kuliko wote duniani ni mninga, kuna kabati alichonga mzee enzi mimi sijazaliwa na lipo mpaka sasa na mbao zipo imara vile vile anachofanya yeye ni kupiga vanish tu, ni miaka 20+ sasa
mninga unapatikana wapi
 
Kupata mbao za mninga kunahitaji umakini kama wewe hunauelewa wa mbao. Bei ya mninga iko juu ukiringanisha na mtiki. Kwa mimi mtaalam nikiinusa mbao au kuiangalia tu, najua huu ni mti gani.

NB: kama unahitaji mbao bora kabisa tafuta mti wa MNINGA AU MVURE.
 
mti bora kuliko wote duniani ni mninga, kuna kabati alichonga mzee enzi mimi sijazaliwa na lipo mpaka sasa na mbao zipo imara vile vile anachofanya yeye ni kupiga vanish tu, ni miaka 20+ sasa
Mninga si lolote si chochote kwa mtiki. Sema wengi mmekaririshwa tu coz mninga ndo ulianza kutumika kabla ya mtiki.
In terms of durability, kwakweli mtiki ni baba lao hauozi wala haubunguliwi na unang'aa kuliko mninga.
Matumizi makuu ya mtiki ukiachana na samani za ndani, pia hutumika kutengeneza low surface finishings za ndege na meri bila kusahau vyombo vya mziki km spika etc!
 
neno langu sio sheria, mimi naongea kwa uzoefu coz naziona samani za mzee jinsi zilivyo imara mpaka sasa, na hapo zina umri mkubwa kuliko mimi mwenyewe
 
Kupata mbao za mninga kunahitaji umakini kama wewe hunauelewa wa mbao. Bei ya mninga iko juu ukiringanisha na mtiki. Kwa mimi mtaalam nikiinusa mbao au kuiangalia tu, najua huu ni mti gani.

NB: kama unahitaji mbao bora kabisa tafuta mti wa MNINGA AU MVURE.
Nyie wote mmekaririshwa tu na mnaishi kwa mazoea... mbao za mninga, mvule, mkongo/mkomba/mkola zilizoeleka kutumika kutokana na enzi hizo upatikanaji wake ulikuwa rahisi na ni miti iliyokuwa inajiotea ovyo maporini tofauti kabisa na mtiki ambao kiasili haukuwepo Tanganyika. Miti hii ipo kwa wingi bara la asia na ililetwa nchini enzi za mwl Nyerere ikaoteshwa Mtibwa, Lunguza na Kilosa.
Imeanza kuvunwa miaka ya hivi karibuni baada ya kupungua china na india ndo wakajimovuzisha kwetu(shamba la bibi) kujivunia kwa bei ya kutupa.
Ndiyo maana mpaka leo hatuijui thamani ya mtiki.
Natumaini mpaka hapo mmeelewa thamani ya mtiki.
 
neno langu sio sheria, mimi naongea kwa uzoefu coz naziona samani za mzee jinsi zilivyo imara mpaka sasa, na hapo zina umri mkubwa kuliko mimi mwenyewe
Basi mkuu chukua hiyo na uelewe hivyo! mimi ni mdau wa mbao kitambo sana na nimezaliwa kwenye mashamba ya hifadhi za miti.
 
Kupata mbao za mninga kunahitaji umakini kama wewe hunauelewa wa mbao. Bei ya mninga iko juu ukiringanisha na mtiki. Kwa mimi mtaalam nikiinusa mbao au kuiangalia tu, najua huu ni mti gani.

NB: kama unahitaji mbao bora kabisa tafuta mti wa MNINGA AU MVURE.
Teh teh teh! mtiki bei yake ipo juu mkuu kuliko mninga. Labda huko sokoni kwenu hawaitambui thamani ya mtiki!
 
Hata mimi nimeshangaa kuona nimepewa bei ya mlango wa mbao za mtiki ikiwa imezidi mninga na mkongo; sikutarajia kwa kweli
 
Hapo umechukua samani iliyo bora... wazungu wanasema "value for money" huo mlango hauozi na unavumilia humidity. No expansion or contraction in whatever season.
 
Back
Top Bottom