Mr Bean.
Senior Member
- Jan 25, 2015
- 185
- 128
Habari zenu wadau,
Nimekuwa na wasiwasi wa ubora na uthamani wa haya madawati mbayo naweza kuthubutu pia kuyaita ya mwendo kasi kwa jinsi yanavyotengenezwa. Jambo kubwa ni katika ubora wa madawati yenyewe.
Kuna maeneo madawati haya yamekuwa yakitengenezwa usiku kucha na mchana kutwa ili kuhofia kutokamilika kwa wakati. Watendaji kwa kuhofia kutumbuliwa wamekuwa wakiwashurutisha mafundi waliopewa tenda ya kutengeneza madawati hayo kufanya haraka.
Hali inayopelekea na itakayo sababisha mengi ya madawati hayo kutokuwa na ubora stahiki. Na sina uhakika kama wahandisi wa manisipaa husika wanahusika na ukaguzi wa madawati hayo au la?
Hasa ukizingatia mengi ya madawati hayo sasa yanatengenezwa kwa kutumia chuma maarufu kama Square Pipes na Mbao. Chondechonde mnaotengeneza hayo madawati yenu ya mwendo kasi zingatieni ubora msije mkatuvunjia viuno ndugu zetu.
Nawasilisha.