Ubongo wa binadamu na utunzaji wa kumbukumbu

Ubongo wa binadamu na utunzaji wa kumbukumbu

Monstgala

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2009
Posts
1,079
Reaction score
1,037
Kuna mambo ya kuvutia katika jinsi ubongo unavyofanya kazi, ni mengi lakini la utunzaji wa kumbukumbu ni jambo la kushangaza iwapo utafikiria kiundani. Nimeandaa mada hii kugusia hili kwa ufupi na unaweza kuongezea ujuayo au kuuliza swali ili tuchimbe zaidi.

Uwezo wa ubongo wa binadamu katika kutunza kumbukumbu ni wa hali ya juu. Ubongo una neurons karibu bilioni moja na kila neuron inaunda njia takribani elfu moja zinazounga neurons nyingine hivyo kuleta miunganiko zaidi ya trillioni moja. Laiti kama kila neuron ingekuwa inatunza kumbukumbu moja basi tungesema basi ubongo limit yake ya kutunza kumbukumbu ni pale zinapokaribia bilioni moja, lakini sivyo.

Miunganiko hii ya neurons inatengezeza mtandao mkubwa sana wa kupokezana kumbukumbu kwa wakati mmoja na hivyo kufanya uwezo wa kutunza kumbukumbu hizi uwe mkubwa sana kiasi kwamba hauwezi kujaa katika maisha yote ya binadamu hata akiishi miaka mia moja. Hii pia ni kwa sababu neurons katika ubongo zinaendelea kukua katika maisha yote ya binadamu.

Kwa kulinganisha na utunzaji wa kumbukumbu katika computer, uwezo wa ubongo ni sawa na 2.5 petabytes au one million gigabytes. Vifaa vyote tunavyoviona kama latest technological devices kama smart phones, ipads, PCs, GPS devices na vinginevyo vina uwezo wa chini sana wa kutunza kumbukumbu kama vikilinganishwa na ubongo wa mwanadamu. Lakini pia kuna super computers kama K-Fujitsu hii ni exceptional kwa kutunza kumbukumbu ubongo wa binadamu hausogei (sio ufanyaji kazi)

Lakini mbona tunasahau?

Kusahau kule kwa kawaida ni jambo la kawaida la binadamu na lina sababu zake na labda pia umuhimu wake. Kujifunza kwa nini ubongo huruhusu kusahau sio kitu kidogo bali hili ni eneo pana sana la psychology na lina wataalam waliobobea kutambua kwa nini tunasahau.

Kuna theories zake zinazoelezea jambo hili la ajabu la ubongo na zenye nguvu zaidi ni ile ya kufutika kwa kumbukumbu za muda mfupi (Trace decay and displacement) na ile ya kufutika kwa kwa kumbukumbu za muda mrefu. (Interference and lack of consolodation)

Kwa theory ya kwanza (trace decay theory) inaelezea kumbukumbu ina kawaida ya kuacha alama(trace) katika ubongo. Hapa trace inakuwa kwa maana ya mabadiliko fulani ya kikemia au kifizikia ndani ya mishipa ya ufahamu.

Sasa kinachotokea ni kwamba kusahau kunakuja kama matokeo ya asili ya kufutika au kufifia kwa hizi alama za kumbukumbu zilizoachwa. theory hii inapendekeza kuwa kumbukumbu za muda mfupi hutunzwa kwa muda wa sekunde 15 hadi 20 na kama hazikushughulikiwa basi hupotea au kufutika. Utafiti uliofanywa zamani sana na unaojulikana kama Brown-Peterson task unasapoti hii theory.

Theory ya pili (interference and lack of consolidation), hii inapendekeza kuwa baadhi ya kumbukumbu hupambana na kuingiliana ili kupata nafasi katika sehemu zinapotunzwa. Kama kumbukumbuku ya iliyotunzwa mwanzo inafanana na nyingine inayoingia basi kuingiliana kwa kumbukumbu hizi ni dhahiri.

Inaweza kutokea kwamba kumbukumbu iliyotunzwa kabla ina nguvu zaidi na inazuia kumbukumbu mpya isitunzwe (Proactive interference) na pia inaweza kutokea kumbukumbu mpya haipati nafasi kwa kuwa uwezo binafsi wa mtunza kumbukumbu hauwezi kustahimili kumbukumbu mpya.

Vipande vingine vinavyojenga theory ya kwanza na hii ya pili ambayo hasa ni kushindwa kukumbuka au kuvuta kumbukumbu ni kama "Generic cues" pale ambapo mzizi wa kumbukumbu unafanana. "Repression" pale ambapo kumbukumbu inafanyiwa makusudi ifutike pale ambapo kumbukumbu hii ina madhara. Pia hali ya ubongo inaweza kusababisha kupotea kwa kumbumbuku hii ni kutokana na magonwa mbalimbali kama Amnesia, Jipu la ubongoni (Brain tumour) na mengineyo.

Mambo mengine tofauti na utunzaji wa kumbukumbu

Fahamu (neuron impulses) kwenda na kutoka katika ubongo husafiri speed ya kilomita 270 kwa saa. Huu ni mwendo mkali sana ukizingatia kutoka kwenye kidole cha mguu wako kwenda kwenye ubongo ni kama sentimita 160 tu. Lakini kuna aina tofauti za neurons na hivyo speed inatofauitiana katika kila aina baadhi speed hupungua hadi nusu mita kwa sekunde (0.5 meters/sec) au kuongezeka sana hadi mita 120 kwa sekunde (120 meters/sec).

Nishati inayotengenezwa na ubongo wa binadamu ni sawa na ile ya kuwasha balbu ya wati kumi (10 watts). Hii ni hata ukiwa umelala. Hivyo kwa kipindi kirefu cha maisha chukulia taa hii ya watt 10 inawaka. Na ubongo huwa active zaidi pale mtu anapolala tofauti na wengi wanavyodhani kwamba tunapolala basi ubongo hupumzika.

Katika vipimo vya nguvu inayotumika wakati wa mchana ukiwa kazini na majukumu ya kawaida au hata ukiwa unafanya hesabu ngumu bado ni ndogo ikilinganishwa na ile inayotumika ukiwa umelala unaota. Na inasemekana wale watu wenye I.Q kubwa kuwa wanaota ndoto sana kulinganisha na wale wenye I.Q. ndogo.

Binadamu anaota ndoto zaidi ya elfu katika usiku mmoja ila kwa kuwa nyingi ni fupi sana hivyo hazitunzwi katika ubongo na unapoamka huwezi kukumbuka. Hii kitu bado inasumbua vichwa vya wataalamu wa mambo ya ubongo.

Jambo jingine kubwa la uwezo wa ubongo wa binadamu ni kubeba information nyingi sana kwa wakati mmoja. Information hizi zinatokana katika milango yote ya fahamu na zinaweza kuchambuliwa kutafsiriwa, kupangwa, kuitikiwa na kutunzwa kwa wakati mmoja.

Seli mpja ya ubongo wa binadamu ina uwezo wa kushikilia information sawa na kitabu kimoja kizima cha Encyclopedia. Encyclopedia ni kitabu kama kamusi ya tawi la elimu fulani. Encyclopedia ya utamaduni basi itakuwa na summary ya kila kitu kuhusu utamaduni kwa mpangilio wa mfuatano wa herufi (a-z).

Viumbe wengine wenye kumbukumbu kubwa

Kuna baadhi ya viumbe wenye uwezo fulani mkubwa sana katika bongo zao lakini bado hakuna aliyethibitishwa kumzidi mwanadamu.

Ndege wa aina nyingi wana uwezo fulani wa kumbukumbu (spatial memory) ambao huwasaidia kuishi katika mazingira magumu. Mfano njiwa wale wanaoishi mijini wana uwezo wa kukumbuka sura ya binadamu katika details za kushangaza. Ukimtisha njiwa mmoja akakuona vizuri zura yako ukirudi baada ya wiki hata kama umebadili nguo na unatabasamu yule njiwa atakutambua na kuruka mbali haraka. Hivyo hivyo ukimpa chakula na kuonesha huna hatari kwake akikuona sura vizuri hata ukirudi baada ya mwezi njiwa yule atakukumbuka na kuruka karibu yako. Hii ni kwa sababu ubongo wake hutunza kumbukumbu za tabia fulani za uso ambazo zimetofautiana kati ya kila binadamu. Pia kuna sokwe mtu hawa wanajulikana kwa kumbukumbu za aina mbalimbali ikiwemo visual memories.

Wengine ni Sea lion na Tembo, hawa wana kumbuka vizuri sana pale wanapooneshwa kitu alafu kujaribiwa kama watakumbuka hata katika hali ya kuchanganywa sana. Tembo huweza kutambua kundi lake hata likiwa na tembo wengine mia na hamsini atawakumbuka wote. Na pia wengine waonaingia katika list ya uwezo wa hali ya juu wa kukumbuka ni pweza na paka. Ubongo wa pweza hufanya kazi kama ubongo wa binadamu na si viumbe wenzie wa majini. Pweza pia anauwezo wa kutunza kumbukumbu ndefu na fupi na hweza kuziunga katika hali fulani ya hatari hivyo kufanya mambo ambayo hata binadamu angehitaji muda zaidi wa kufanyia mazoezi. Paka huyu tunaishi nae majumbani mwetu na labda tunamdharau tu lakini ni kiumbe mwenye kumbukumbu kali za muda mfupi ambazo zake ni ndefu kuliko za binadamu.

Ukivutiwa na mada hii karibu tujadili...
 
mkuu mada nzuri sana ngoja nikune kichwa kwanza nina maswali kadhaa kuhusu hizi mbongo zetu
 
Mkuu Monstgala/Mgalanjuka shukrani kwako kwa kutuletea elimu adimu na pana mno
mimi mwanafunzi wako mtiifu nashukuru sana
SWALI
je katika ubongo wa binadamu neurons zinafanana idadi ?
kwa lugha nyingine labda nijaribu kujifananisha mimi na Einstein, je neurons tupo sawa ?

.made in mby city.
 
Asante, neurons ni aina ya seli kama zilivyo seli nyingine katika mwili wa kiumbe hai lakini hizi ni special kwa mfumo wa fahamu hivyo muundo na aina ni kwa ajili ya kupokea stimuli na kuzifanyia kazi. Kila mtu ana seli mwilini mwake lakini idadi ya seli si sawa kati ya mtu na mtu na seli mpya zinatengenezwa kila mara. Hii ni sawa pia kwa neurons idadi si sawa na wala wingi au uchache wa neurons katika ubongo sio kigezo cha akili nyingi au akili kidogo. Uwezo wa kufikiri ni complex issue na ni moja ya maeneo yanayofatitiwa sana ingawa kuna gap kubwa bado kutokana na ugumu wa kuutafiti ubongo lakini jinsi teknolojia inavyokuwa mambo mengi yanapata majibu yanayoridhisha.
 
Mkuu Monstgala/Mgalanjuka ahsante sana
bibiangu alishawai nambia kuwa "watu wanaotumia ubongo kwa kiasi kikubwa ndio wanaofanya kila kitu kiwezekane"
hivi hii statement ina ukweli ?
kwani inakuaje baadhi ya watu wanatumia kiasi kikubwa cha ubongo kuliko wengine ?

Kwa urahisi kabisa ni kwamba unaporudia kufanya kitu mara nyingi ndivyo jinsi ubongo zile kumbukumbuku za process ile zinavyozidi kijishikiza katika sehemu zinapotunzwa na vivyo hivyo usiporudia basi kumbukumbu ile inaweza kufutwa/kufutika kwa kuwa inakuwa haina uzito. Mfano unaposikia jina la mtu kwa mara ya kwanza kuna hatari ya kwamba baada ya mwezi usilikumbuke iwapo 1. Hukulitaja mwenyewe baada ya kulisikia (kwa jinsi utakavyojaribu kulitamka au kulirudia ndivyo litakavyotunzwa katika ubongo wako) 2. Jina lile lile halikuwa na connection yoyote ya muhimu kwako 3. Jina lile halikuwa la ajabu au zuri/baya lenye kuvutia kwa namna fulani etc. Mifano hii mitatu ina maana ubongo kwa namna fulani haukuangaika au haukufanya kazi kwa kiasi kikubwa kutunza jina hilo au kulifikiria hivyo matokeao yako ni wewe kulikumbuka kwa urahisi.

Kwa hiyo jinsi ubongo unavyofanya kazi zaidi ndivyo mambomengi yanawezekana hii ni kwa upana zaidi apart from kumemorise vitu.
 
Kuna jamaa moja alipigwa na baseball kichwani toka siku hiyo hadi leo hasahau kitu, anakumbuka tarehe flani hadi hali ya hewa ilivokua siku hiyo na mambo yote aliyoyaona... Brain ya hivi bonge la dili
 
ahsante Mkuu Monstgala/Mgalanjuka
mkuu hivi je informations ukiwa unaziweka/unazitunza ubongoni, ubongo utaweza kubeba ukubwa kiasi gani na kwa mda gani information za encyclopedia fulani ??

.made in mby city.
 
nifanyeje ili niwe na kumbukumbu za mda mrefu

Kwa kawaida kumbukumbu zinashika zaidi pale kitu au tendo linaporudiwa-rudiwa, kinapohusishwa na vitu vingine vilivyo tayari kwenye kumbukumbu zako, au kinapojengewa mazingira fulani yenye tofauti. Ukiondoa hali nyingine ambazo ni exceptional (mfano mtu mwenye kumbukumbu kali naturally/au mtu mwenye ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu) mtu wa kawaida anaweza kusaidia uwezo wake wa kukumbuka kwa ku-exercise yale unayotaka kuyakumbuka. Kama utaijengea mazingira kumbukumbu basi itatunzwa na itakuwa rahisi kuivuta pale unapoihitaji. Yote haya yanafanyika kwa namna nyingi sana tofauti kutegemea na mtu na vigezo vingine vingi.
 
Kuna jamaa moja alipigwa na baseball kichwani toka siku hiyo hadi leo hasahau kitu, anakumbuka tarehe flani hadi hali ya hewa ilivokua siku hiyo na mambo yote aliyoyaona... Brain ya hivi bonge la dili

Sure, kuna cases nyingi za damage ya ubongo ambayo inapelekea hali mbili tofauti either kupoteza kumbukumbu na kuleta athari kwa ufanyaji kazi wa kwa kiwango fulani au kuzidisha ufanyaji kazi wa area fulani either kumbukumbu au kuongezeka kwa kasi ya kufikiri au kurespond kwa stimuli vizuri zaidi. Kuna sababu za kisayansi zinazofafanua hali hii.

Inaweza pia kutokea kwamba mtu baada ya ajali na damage kichwani akapoteza uwezo area fulani na ukaongezeka area nyingine. Kuna baadhi ya wagonjwa wa akili wako strong sana katika area fulani ndogo na wanaweza kuwa juu ya kawaida ila ndio hivyo ukija upande mwingine wanakuwa hawako sawa.
 
Swali langu ni kipi kinasababisha tofauti ya uwezo wa ubongo kati ya mtu na mtu?,mfano akili.
 
karbu mkuu Eiyer

.made in mby city.

Kuna tafiti ambazo zinakataa kuwa ubongo ndio unaotunza kumbukumbu bali ni kifaa cha kuzipata umbukumbu na ndio maana kikipata athari unakuwa na tatizo la kumbukumbu kwa sababu kile ambacho kinakuwezesha kuaccess sehemu ambapo kuna hizo kumbukumbu kim epata tatizo

Hiyo pia inaweza kuwa kinyume chake kwani unaweza kupata tatizo ambalo litaimarisha ubongo wako na kukufanya uwe na uwezo mkubwa wa kuwa na kumbukumbu kwasababu zile zile, kwa maana nyingine hili tunaweza kusema sio tatizo bali ni faida!
 
Ubongo ni ajabu lakutosha

Na ngumu zaidi ni kwamba hakuna kinachoonekana zaidi ya kuobserve activities (za umeme) katika regions mbalimbali za ubongo. Hii ni sawa na kuangalia matokeo ya behaviours fulani na kujaribu kurelate na nadharia tofauti. Lakini kwa sasa stadi za eneo hili zinaadvance sana kwa kuwa na tech inayorahisisha majaribio tofauti.
 
Kuna tafiti ambazo zinakataa kuwa ubongo ndio unaotunza kumbukumbu bali ni kifaa cha kuzipata umbukumbu na ndio maana kikipata athari unakuwa na tatizo la kumbukumbu kwa sababu kile ambacho kinakuwezesha kuaccess sehemu ambapo kuna hizo kumbukumbu kim epata tatizo

Hiyo pia inaweza kuwa kinyume chake kwani unaweza kupata tatizo ambalo litaimarisha ubongo wako na kukufanya uwe na uwezo mkubwa wa kuwa na kumbukumbu kwasababu zile zile, kwa maana nyingine hili tunaweza kusema sio tatizo bali ni faida!

Ni eneo dogo la ubongo linalohusika na utunzaji wa kumbukumbu, sio mfumo wa fahamu wote. Lakini hizo tafiti zinapendekeza ni wapi hasa memories zinatunzwa apart from sehemu ya ubongo?
 
Inaweza kutokea kwamba kumbukumbu iliyotunzwa kabla ina nguvu zaidi na inazuia kumbukumbu mpya isitunzwe (Proactive interference) na pia inaweza kutokea kumbukumbu mpya haipati nafasi kwa kuwa uwezo binafsi wa mtunza kumbukumbu hauwezi kustahimili kumbukumbu mpya. ..
hapa sasa ndipo inakuja kitu kinaitwa Genetics -- koo zingine zinakuwa na tatizo hili la kutotunza kumbukumbu.
 
Ubongo ni ajabu lakutosha
kaka si ubongo tu, system nzima ya mwili wa binadamu ni so complicated kiasi kwamba ukisoma unaweza kuogopa hasa kwa sisi ambao hatukusomea elimu ya viumbe hai.

Kuna siku daktari wa wanawake, alinisimulia namna process ya kujifungua inavyofanyika - aisee niliogopa sana, nikatamani nisingemuuliza!! very complicated - kama process moja itachelewa tu basi unaweza kupoteza mama au mtoto.
 
Back
Top Bottom