ubingwa wa yanga ulipangwa

fimbombaya

Member
Apr 11, 2011
47
12
kumekuwa na maneno mengi kabla na hata baada ya mechi kati ya yanga na toto africans jumapili kuwa timu hizi ni baba na mwana kiasi cha kupelekea mechi hiyo kutokuwa na ushindani wa dhati hasa kipindi cha pili hali iliyopelekea magoli ya kupeana kufanya ubingwa uende kwa yanga. hebu waliopata kushuhudia mechi hii mtujuze hali halisi ilikuwaje?
 
Ni kweli pambano lilikuwa la upande mmoja. Ila nakuhakikishia Yanga hawakununua bali inawezekana ni Fadhila ya mwana kwa mzazi pambano lao lilimalizika ikabidi wasubiri matokeo ya Dar kati ya Simba na Majimaji kwa dakika. 9 na ushe kwa maana hiyo Timu zote zilichakachua ushindi ila mechi ya Dar ilileta mpaka ugomvi wa dhahiri wa kugombea pesa baina ya wachezaji kwa wachezaji wa timu ya Majimaji waliosalitiana na ugomvi pia ukazuka baina ya benchi la ufundi la timu hiyo lililotofautiana na meneja wa timu hiyo. Stephen mapunda'Garincha' aliekuwa kakabidhiwa'MZIGO' iIi aka malize mchezo mchafu kwa baadhi ya wachezaji muhimu wacheze kinazi mpaka sasa hali si shwari baina ya wachezaji kwa wachezaji na baadhi ya wachezaji na mapunda akiwemo kipa wa kwanza wa timu hiyo Juma Ahmad aliepigwa benchi asidake katika mechi hiyo huku ikitolewa taarifa kuwa ni mgonjwa kumbe ni Mzima ila kulikuwa na Taarifa waliozipata baadhi ya wachezaji wenzake waliokuwa upande wa Mapunda kuwa Kipa huyo Mahiri atasajiliwa Yanga msimu ujao hivyo asipangwe anaweza kuwaharibia Deal ajabu kuwa wengine waliosalia ambao hawakushikishwa kitu kidogo wakacheza kihalali na wakafanikiwa Kukomaa kiaina mpaka benchi likaanza kuwatolea lugha ya matusi uwanjani hasa mapunda baada ya kuona dakika ya 80 bado ngoma inasomeka 3-1, hapo ndio walipoanza kufanyiana Sub za kuwakomoa waliokuwa hawa kuwashirikisha katika Mchezo wao'Mchafu' aibu kweli ungekuwepo uwanjani tena jirani na benchi la Majimaji hutokwenda tena mpirani bora ucheze karata Ndio maana tunaishia katika Raundi za awali kwenye mechi za Kimataifa
 
Mwaka huu tutasikia mengi. Subb ya kipa wa Maji2 ilikuwa utata mtupu. Hakuwa ameumia chochote.
 
Nilikua ccm kirumba. Mambo ni hayohayo. Kiongozi mmoja wa yanga alipewa 'mzigo' awafikishie vijana wa Toto. Akakaa nao hakuufikisha pengine aliamini yanga wangeshinda kwa uwezo. Vijana wa Toto walikomaa kisawa sawa, na huenda wangeamua wangeshinda maana walikua wanaingia mpaka kwenye 18 halafu wanapiga fyongo. Mpaka half time ngoma ilisomeka 0 - 0 huku matokeo ya Dar tunasikia Simba anaongoza bao 2. Ilibidi waulizwe viongozi wa Toto "vp mbona vijana wamekaza?" na endapo wamepata mzigo, waliposema hawakupata mzigo, ilibidi yule kiongozi atafutwe na mzigo ufikishwe. Hata hivyo inadaiwa, mzigo uliokua umeandaliwa toto waliukataa wakidai ni kiduchu, ndipo yanga wakaongeza dau. Ndipo mabao yakaanza kumiminika 'kiajabu' yakianzia mapema tu baada ya kuingia kipindi cha pili (dk 46). Pia kipa mahiri wa Toto aliondolewa dk za mwisho, na kuingizwa kipa ambaye kwa wanaoijua vizuri toto wanamuelezea kuwa kibonde, na akafungwa bao la 3 kizembe sijapata kuona. Pamoja na ushabiki wangu wa Yanga, Sikufurahia kilichotokea uwanjani, na yanga hawakuonesha kiwango chochote. Walionekana kuzidiwa kimchezo. Naweza kutabiri kirahisi tu kwamba endapo mabadiliko makubwa yasipofanyika Yanga haitafika popote klabu bingwa Africa. Soka letu linaporomoka kwa mtindo huu.
 
Jamani hawa watani zetu hakuna mwaka wakashindwa kutoa visingizio. Hebu tuacheni tusherehee ushindi wetu. Kumfunga Majimaji migoli minne hivihivi ushindi haukupangwa. Uliopangwa ni wa Yanga kisa kabeba kombe. Give us a break comeon folks!!!!
 
kumekuwa na maneno mengi kabla na hata baada ya mechi kati ya yanga na toto africans jumapili kuwa timu hizi ni baba na mwana kiasi cha kupelekea mechi hiyo kutokuwa na ushindani wa dhati hasa kipindi cha pili hali iliyopelekea magoli ya kupeana kufanya ubingwa uende kwa yanga. hebu waliopata kushuhudia mechi hii mtujuze hali halisi ilikuwaje?

Mnazi wa mnyama wewe.
 
kwahiyo nyie Simba mwataka ku2ambia hata OKWI 2limnunua au!!?? acheni ushabiki jamani m2ache YANGA na furaha ze2 za knyakua ubingwa.
 
Acheni upuuzi,mpira wa Yanga ulipangweje ukaisha 3-0 dk 9 kabla ya mpira wa Simba na Majimaji kuisha ilhali Magoli yalikuwa yakiendelea kumiminika kwa Majimaji,kwa akili ya kawaida kabisa kama ule Mpira wa Yanga ungekuwa umepangwa lazima Yanga angetengeneza margin ya kutosha ambayo ingewahakikishia hata kama Simba angefunga magoli ya doubledouble asingeweza kuifikia.
Tuwe tuna'reason kidogo siyo tunabwatuka tu.
 
sad lion.jpg

Too sad.
 
Kwa nini mnaonea wivu yanga wewe na wengine wengi waache washerekee ushindi ni wao

YANGA OYEEEEEEEEEEE
 
Back
Top Bottom