Watanzania tuna ulimbukeni sana na neno "ubinafsishaji" na halafu upungufu ulioko katika lugha yetu ya kiswahili, ndipo tunapozidi kuchanganyikiwa. Katika kiingereza kuna maneno State Ownership (Parastatal), Public Ownership na Private Ownership. Katika Kiswahili tuna "Mali ya Umma" na "Mali ya Binafsi", kwa hiyo hapo ndipo tunapokorogekewa sana, kwa sababu tunaamini kuwa ni ama mali ya umma kama ilivyo Tanesco au ni mali binafsi kama ilivyo IPP. Tulliingia katika soko la kubinafsisha mali za umma bila kujua tofauti baina ya State Ownership na Public Ownership na ndiyo maana tukaruka grupu hilo na kuishia kwenye Private Ownership kuwa ndiyo maana ya "Ubinashaji." Tuna ugonjwa wa ubinafsi sana leo, kwani process yote ilienda kibinafsi. Kila siku utasikia tunamtafuta mwekezaji anunue shirika fulani halafu process yote ya ununuzi inafanywa siri.
Wakati Kenya walipobinsfaidha Kenya Airways, waliitoa kwenye state ownership na kuiweka kwenye public ownership, na kwa hiyo hakuna mtu anayedai kuwa KQ ni mali yake binafsi. Na kweli KQ imekuwa ni mfano mkubwa sana wa mafanikio ya public ownership. Lakini Tanzania utashangaa hakuna enterprise yoyote ambayo kweli ni public, zote ama ni private au ni State Owned.
Sasa sijui ndugu yangu alikuwa ana maana ya kuifanya TANESCO kuwa Private, au kuwa Public au ubaki kuwa State owned. Makampuni makubwa karibu yote ya nchi zilizoendelea ni Public owned; ni machache sana ambayo ni private, na ni kiduchu sana ambayo ni State Owned isipokuwa huko China ambapo bado makampuni mengi ni state owend ingawa wamekuwa waki-transition kuyafanya kuwa public owned.