Ubinafsishaji umetugharimu - Ngasongwa akiri sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubinafsishaji umetugharimu - Ngasongwa akiri sasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Feb 1, 2008.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  SERIKALI imekiri kufanya makosa katika zoezi la kubinafsisha mali za nchi, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limewafanya wageni kumiliki zaidi uchumi.

  Kauli hiyo ilitolewa jana Dar es salam na Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji, Dk. Juma Ngasongwa alipokuwa akizungmza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua semina ya kupata maoni ya kuboresha Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).

  Alisema dhana ya serikali kuendesha zoezi la ubinafsishaji lilikuwa ni kutoa nafasi kwa sekta binafsi iweze kumiliki uchumi wa nchi lakini kwa bahati mbaya hali imekuwa tofauti.

  Alisema uchumi huo hivi sasa unamilikiwa na wageni ambao wanaendesha miradi mikubwa na kuacha asilimia kubwa ya Watanzania wakiwa katika hali mbaya kiuchumi.

  Alisema sekta binafsi inaaminika ndiyo injini ya ukuaji wa maendeleo ya taifa sambamba na kuwa na idadi kubwa ya watu lakini haina uwezo wa kuhimili mikikimiki ya uchumi kutokana na mabadiliko ya kiuchumi duniani.

  "Lengo letu lilikuwa kuwamilikisha uchumi watu waliopo katika sekta binafsi lakini hali imekuwa tofauti, wageni ndiyo wanamiliki, hapa tulikosea," alisema Ngasongwa.
  Alisema kwa kutambua kosa hilo serikali imeamua kushirikiana na NDC, ili Shirika hilo liwe mwekezaji mkubwa hapa nchini na kutoa nafasi kwa wazawa kumiliki uchumi wao.

  "Serikali tuliipunguzia nguvu ya kufanya kazi NDC lakini sasa tunaona kuna umuhimu wa kuipa nguvu kwani bila ya kufanya hivyo mambo yatazidi kuwa magumu kwa wananchi," alisema Ngasongwa.

  Alisema kupitia NDC, serikali ina nia ya kuendeleza miradi ya chuma, uchimbaji wa magadi na makaa ya mawe ambayo ana imani yatanyanyua uchumi wa Tanzania.

  Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Chrisant Mzindakaya, alisema ili shirika hilo liweze kutimiza malengo waliyojiwekea ni vema serikali ikaangalia namna watakavyoiwezesha NDC kimtaji
   
 2. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Japo maelezo aliyo yatoa mheshimiwa yanaonekana mazuri kwa msomaji na yenye mguso, I smell something fishy in it!

  Nahisi hii ni kutaka kutengengeneza njia ya mradi wa magadi ambao watu hawalali kwa ajili yake?

  Lakini pia makaa ya mawe yapi? si ndo hayo Kiwira wapo wanajinoma kwa 85% serikali ikiambulia 15%? Huyu Fisadi Mzindakaya bado tu anataka serikali imchotee mabilioni mengine?

  May be am getting it in the wrong way... but...
   
 3. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2017
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Bado tunasafari ndefu.
   
Loading...