fikirikwanza
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 7,452
- 3,065
Ukiangalia kwa kina unagundua ni ubinafsi mkubwa ambao unafanyika bila kujali maslahi ya taifa. Maslahi ya taifa ni kitu chochote ambacho kinakuja kwanza ama kabla ya maslahi ya mtu, kikundi au chama.
Ukimuuliza mwana CCM kama Nape na wengine wengi nyuma yake, utasikia hawako tayari kuona CCM inakufa, hata kuona inaachia ngazi kiserikali. Hapa unapata mawazo mengi sana, kuwa nani aliwaambia na kuwasadikisha kuwa CCM lazima iwepo na lazima ishike dola kila uchaguzi??? kuna ubaya gani CCM after 50years ya kuongoza tanzania ikasema inaachia ngazi, ukiangalia hali ya uchumi wa nchi hii, ukaangalia mihimili ya uchumi kuwa ni siasa safi, watu, uongozi bora na ardhi, unagundua kuwa watu makini ndani ya CCM wangeomba CCM iachie serikali ili kupata fursa ya kujifunza wapi walikosea na wapi walifanya vizuri. ni suala la akili na hekima tu hapa, kila mtz analalamika uchumi na maisha duni sasa kama kiongozi unajitathmini harafu unachuka hatua za kuachia ngazi.
ukitoa ubinafsi wa viongozi na viongozi nyemelezi, utauona ukweli kuwa CCM kwa hali ilivyo sasa inapaswa kwa heshima kubwa kujiweka pembeni ili watu wengine na mawazo mengine yaweze kufanyiwa kazi. Ubinafsi wa kutaka kutawala milele, ubinafsi wa kufanya nchi kama aina fulani ya biashara. Viongozi wakubwa wanataka wawalisishe wadogo tena mbaya zaidi wenye uhusiano wa damu madaraka ya nchi ambayo hapo awali tuliwapa wao madaraka kwa jitihada zao sio za watoto na familia zao kwa ujumla.
Leo hii watoto wa vigogo wa zamani ndo viongozi wetu katika serikali, chama na mashirika ya umma. orodha ni ndefu na inajulikana kwa kila mtu.
Ubinafisi huu utaiua CCM kifo kibaya sana, kuna watu wanaamini kuwa kuna mgogoro mkubwa ndani ya CCM kugombea madaraka, nami pia naamini hivyo; Kuna kambi ya Lowassa, Membe, Sitta etc. Hawa watu hawawezi kukubaliana kutokana na faida binafsi na ubinafsi. Chama kimepoteza mvuto kwa raia wa tz hata wanawake ambao ndo walikibeba sana kwenye chaguzi za hivi karibuni, chama kimepoteza mvuto kwa wazee (suala la mafao yao) na wakulima (bei za mazao ya biashara kama pamba etc) ambao pia walikuwa nyuma yake kwa miaka nenda rudi.
Hali hii ya kutokubaliana na ukweli kuwa kivumacho hakidumu, hakuna mwenye hati miliki ya ikulu ya dar es salaam, hakuna mwenye hati miliki ya jimbo lolote TZ au halmshauri yoyote ndo itapelekea CCM kufa na pengine kuacha nchi ktk hali ya mmomonyoko mkali. Tukubali hali ya kutokukubali kuacha madaraka ilianza na ipo ndani ya CCM kwa muda mrefu. fikiria utitili wa majimbo ya uchaguzi hata kama hakuna tija kwa wananchi kwa lengo moja tu la kupatiana sehemu ya madaraka ili kila mwanaCCM mafia apate jimbo. Tumeshuhudia majimbo yakigawanywa bila sababu halisi (real reasons) japo sababu nzuri (good reasons) juu ya jambo hilo hutolewa. ubinafsi na uroho wa madaraka umefanya wilaya kuongezeka hata kama hatuna fedha za kuhudumia wilaya na mikoa hiyo.
Wakati technolojia inapanda na uwezo wa mtu mmoja kuhudumia sehemu kubwa zaidi kwa njia ya teknolojia unakuwa mkubwa, ambapo tulipaswa kupunguza hata wilaya na mikoa yetu, sisi tunaongeza kwa faida ya wachache. kwa hili ndo kodi zinaongezeka hata bila kujali vipato vya watanzania, kwa hili nani alaumiwe??? sio ubinafsi huu???
Ubinafsi huu utaiua CCM na kuiacha nchi ikiwa taabani.
Nawasilisha