Ubepari utakufa duniani. Tusiusogelee!

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,264
Reaction score
17,561
Huwezi kumiliki utajiri mwingi katikati ya watu wengi masikini ukabaki salama. Ni swala la muda tu iko siku watakunyang'anya kutegemea na hali yao itakavyoendelea kuwa bora au mbaya zaidi. Kama hali ya wengi kiuchumi itaendelea kuboreka watakuheshimu kwa utajiri wako, lakini kama hali zao zikizidi kuwa mbaya utajiri wako utageuka kuwa laana kwako. Utakosa usingizi, watauchukua na wanaweza kukuua pia. Maana njaa haizoeleki hata kidogo.

Wananchi wa nchi za Magharibi sasa wameanza kuuona ubaya wa ubepari, hawataki tena haki, demokrasia na uhuru wa kutukana, bali wanataka haki ya kula chakula, matibabu, elimu, malazi na malipo ya haki kwa wote.

Wananchi wa Magharibi wameshaanza kuwapora mali na kuwanyima kura matajiri na wanaokumbatia ubepari mkali. Wameshaanza kutamani mifumo ya kijamaa kama ile ya Uchina, Urusi, Korea, Tanzania, Cuba na Ulaya mashariki ambako hakuna anaekosa mahali pa kulala, chakula, elimu, matibabu, na mavazi hata kama ni maskini wa kutupwa.

Nyerere na Karume walikuwa na maono ya kutoka kwa Mungu moja kwa moja kuuchagua ujamaa na kujitegemea. Hata kama tunaona Tanzania tuna amani na utulivu kidogo kuliko mataifa mengine Afrika basi ni kutokana na ujamaa na kujitegemea. Mfumo ambao unamhakikishia kila mtu kupata ardhi, chakula, elimu, matibabu, malazi, mavazi na usafiri kwa bei nafuu. Ardhi ni mali ya serikali hivyo kila mtu yuko huru kwenda kupata ardhi na kuishi kokote ilimradi tu asivunje sheria na taratibu za nchi na za kule anakohamia.

Vyama vyote vya siasa vinavyotaka kubadilishana na CCM katika kuiongoza nchi hii lazima viikubali misingi waliyoiacha Nyerere na Karume. Vingine wananchi wataipatia baraka zote CCM kuvizuia kwenda Ikulu hata ikibidi kwa kutumia nguvu vyama vyote vinavyohisi Nyerere na Karume walikosea sana kutujengea mfumo huu wa ujamaa na kujitegema, aina ya muungano, utawala wa mikoa na umiliki wa ardhi. Vyama vya siasa vishindane kwenye mambo mengine lakini sio kwenye hii misingi.

Sisi watanzania lazima tuwe wakali na ikibidi kumkemea na muondoa kiongozi wa umma aliyejilimbikizia mali; tuzichukue na kuzirejesha kwa umma mali hizo.


View: https://youtu.be/d_jI6d9LsXo?si=-hZ5pSka6150ScOD
 
Tatizo si kuwa na utajiri, bali ni namna utajiri huo unavyopatikana na kutumika. Ubepari usio na mipaka una mapungufu yake, lakini pia ujamaa hauwezi kuwa suluhisho la kila tatizo. Taifa linahitaji haki, fursa sawa, uwajibikaji na mfumo unaompa kila mtu nafasi ya kujikwamua kiuchumi. Tusipambane na utajiri, tupambane na umasikini na mifumo inayozalisha dhuluma.
 
Bila katiba mpya hiyo nguvu ya kuwabananisha mafisadi nani anayo?
Hapo nakukubalia, katiba yetu inakosa kipengele cha kumwadhibu vikali aliyekula rushwa na kutumia vibaya rasilimali za umma kwa manufaa yake.. Hicho ni kipengele muhimu kwenye ujamaa na kujitegemea.
 
Una maana Tanzania ya kina Kikwete, Samia, Rostam, Mo, SSB, nk ni ya kijamaa?
 
Acha kutisha watu mkuu.
Yaani pesa ya kwangu then nipate laana Kwasababu ya watu kuwa maskini Sasa Kwani Mimi ndy nimewapatia huo umaskini?
Kama mungu ndy anae toa utajiri na yeye ndy anaetoa umaskini Sasa shida Iko wapi hapo ya wao kuwa maskini?
 
Acha kutisha watu mkuu.
Yaani pesa ya kwangu then nipate laana Kwasababu ya watu kuwa maskini Sasa Kwani Mimi ndy nimewapatia huo umaskini?
Kama mungu ndy anae toa utajiri na yeye ndy anaetoa umaskini Sasa shida Iko wapi hapo ya wao kuwa maskini?
Hakikisha waliokuzunguuka wanakuwa wanufaika wa utajiri wako, vinginevyo kazi unayo, utalala usingizi wa mang'amng'am.

Pale kwangu mm wale vijana watu wanaowaita vibaka na masela ni sehemu ya maisha yangu. kazi za kupakia takataka, kukatia miti, kuogesha mbwa, kufagia banda, nk wanafanya wao. ninawakumua wananikwamua tunakwamuana na kusonga mbele pamoja. Bangi zao mm hazinihusu kabisa, sijawahi kuibiwa hata sight mirror wala fyekeo.
 
Bongo ni vichekesho. Mashuleni tunafundishwa uongo na chuki
Mfumo wa ubepari hauna muda mrefu utaanguka. Mitaala ya shule ielekee uelekeo huo. Matajiri wanaiba uchaguzi kwa kudhani wagombea kwa fedha nyingi sana.

Pale Uingereza kuna kavuguvugu ka kuukataa ufalme. Hawakatangazi lakini Siku kakipata nguvu nitawajulisha.
 
Tanzania kuna ujamaa gani? Umetumwa? China yenyewe usha achana na ujamaa
 
Ubepari hauzi kufa, ukisema ufe maana ake uchumi wa dunia umekufa.
 
Tanzania kuna ujamaa gani? Umetumwa? China yenyewe usha achana na ujamaa
Hii nafuu unayoiona hapa kwetu inaletwa na mambo yafuatayo:
1. Ardhi yetu kumilikiwa kijamaa. Hakuna mtanzania bila kujali kabila lake au dini atakosa ardhi hadi pale ardhi yote nchini itakapoisha. Sera hii inasababisha kila mtu aweze kujenga kijumba, kufuga, kulima, na kufanya shughuli zake kwa gharama ndogo.

2. Huduma za elimu na afya kutolewa kijamaa. Shule na vituo vya afya/zahanati ziko kila kijiji, kata, tarafa na wilaya.

3. Wanachi kujizalishia chakula chao wao wenyewe mashamabani: Hii ndiyo turufu yetu Tanzania. bei za vyakula iko chini kwasababu wananchi wengi wanajizalishia chakula chao na kuuza ziada ili kupata mahitaji mengine. The higher the supply the lower the price. Mishahara yetu ni midogo sana lakini bei ya chakula ni ndogo zaidi.

Serikali lazima ipime ardhi ya kilimo ambayo haitaruhusiwa kugeuzwa makazi hata kama watu wataongezeka namna gani. Ardhi ya kilimo na ufugaji isibadilishwe matumizi. Na serikali iendelee kutoa ruzuku na utaalam kwa wakulima wadogo vijijini ili wavune mazao mengi kwenye eneo dogo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…