DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania umetuma salamu za pole kwa familia na jamii kwa ujumla ambazo zimepoteza wapendwa wao kutokana na matukio yaliyotokea wakati wa uchaguzi.
Kupitia taarifa iliyotolewa leo, ubalozi huo umeeleza kuwa unaenzi maisha ya wote waliotangulia mbele ya haki, pamoja na wale wanaoendelea kuuguza majeraha ya kimwili na kiakili katika kipindi hiki kigumu.
Aidha, ubalozi umetoa wito wa kuendelea kujenga maridhiano na umoja wa kitaifa kupitia uelewano na uwajibikaji wa pamoja, ili kuimarisha misingi ya haki na amani kwa Watanzania wote.
Kwa heshima ya waliopoteza maisha, ubalozi wa Denmark umesimama kwa dakika moja leo kuwaomboleza.