Wewe juha kweli utaendelea kuwa msukule wa Dr Slaa, hauwezi kutetea ukanda na udini uliyopo Chadema hivi umeishajiuliza kwa nini Said Arfi kajiuzulu Chadema kama siyo udini na ukanda.
Ulivyokuwa kauzu umeona aibu kumtaja John Mnyika Mpare kutoka Kaskazini.
Wewe Chadema ni msukule tu ukitaka kujipima jaribu kugombea nafasi na mchaga uone utakavyofukuzwa kama mbwa.
Mkuu
Tulia ukiwa unachangia hoja usiyumbe yumbe kama mnazi ulioko ufukweni.
Mada hapa inahusu ukanda wewe umesha rukia kwenye udini!!!.
Nikiri kwenye orodha nimesahau kumtaja Mnyika ila kumbuka kuwa Mnyika ni Msukuma na si mpare kama unavyosema, lakini kama angekuwa mpare tatizo liko wapi kama angefanya kazi yake vizuri na ufanisi kama anavyo fanya sasa?! Ungemhukumu kwa kuwa ni Mpare kutoka kaskazini?!
Kwa kuwa umegusa kionjo chako kingine cha udini ngoja nikusaidie hapa.
Kwenye top leadership ya chadema iliyokuwa na viongozi sita kabla ya MM na mzee Saidi Arfi kujiuzuru ilikuwa na muonekano huu.
1. Freeman Mbowe - mkristo KKKT (mwenyekiti)
2. Saidi Arfi - Muislamu (Alikuwa makamu kabla ya kujiuzuru)
3. Said Mohamedi- Muislamu (Makamu mwenyekiti Zanzibar)
4. Dr Wilbroad Slaaa - Mkatoliki, Katibu mkuu
5. Zitto Kabwe - Muislamu, (Naibu aliye vuliwa nafasi zake)
6. Hamadi Yusuph - Muislamu (Naibu katibu Zanzibar).
kati ya viongozi sita wa chadema viongozi wawili pekee ndio wakristo.
Hivi viongozi hao wangeamua kupitisha maamuzi wao wenyewe wakikaa kwenye vikao vyao na ku-base kwenye imani zao za kidini nani wangeshinda kwa wingi wa kura?! Yaani waislamu 4 dhidi ya wakristo 2.
Acheni upumbavu, uislamu hautetewi kinafiki kiasi hicho! nilitegemea ungeanza kujiuliza kwa nini moja ya hukumu za dini yetu ni kumtaka kijana wa kiislamu ambaye ni balehe aoe pindi akifikisha miaka 18 lakini bado MM hajaoa mbali na kuwa na mafao na mishahara ya kibunge huku akiwa pia anagusa vilevi haramu kinyume na mafundisho ya dini. Hivi ndio tunatakiwa kuulizana kama unataka kusimamia uislamu sio kuutumia uislamu kueneza chuki kinyume na misingi ya dini yenyewe.