Ubaguzi unaendelea kuitafuna CHADEMA

Kati ya vitu ambavyo sitakaa nimridhishe au kumsimulia mtu, na hasa mtoto wangu ni kuhusu CCM.

Sina ushabiki wa vyama, ila kwa hiki chama sipendi hata kusikia. Kama ni kichaka, ni kile kisicho pitika hata na sisimizi.
Ndugu.
Hoja yako inaonyesha kama hujitambui au hutambui kile unachokisema.

Ulichofanya hapa katika andiko lako kinaonyesha siyo kupenda tu kuisikia CCM bali pia kutaka wanaJF wachangie mada zinazohusu CCM.

Mleta mada hajataja CCM katika mada yake lakini wewe unaanza kuongelea masuala ya CCM kuonyesha ni jinsi unavyofatilia masuala ya CCM.
 
Kwakifupi nikwamba watanzania wamechoka ccm wanataka chama mbadala nawameshakipata chama chao Mungu alichowaletea Chadema

Mwanahabari Huru
 
Tatizo la kuruhusu watu wengine wafikirie kwa niaba yako.

Siitaji mtu kufikiri kwa niaba yangu kwa ufahamu nilikuwa nao. Huitaji elimu ya pekee kujua mfumo unaoelekea kufa wa ccm.

Hatuwezi kuishi katika ndoto kwa miaka 50 ya uhuru bila kuwa na malengo na mwelekeo chanya. Walio kwenye mfumo huu bado wanaishi katika maoni na wapo kwenye bango la fikra kimaoni.

Mwana falsafa Plato anasema aliye kwenye ulimwengu wa kimaoni bado haufahamu uhalisia wa vitu. Hapa ndipo tunapopata maana ya ujinga, yaani asiyefahamu jambo.

Mtaji mkubwa wa ccm ni wingi wa wajinga. Tunashukuru kwamba kila kukicha idadi ya wajinga inapungua. Hiki ndicho kiyama cha ccm.

Kutoka kwenye mkwamo huu wa fikra tunaitaji "a philosopher king," anayefahamu uhalisia wa vitu. Hili nalo kwa sasa lipo njiani.

Kamwe utawala dhalimu haudumu. Huu ni wakati wa kusoma alama za nyakati. Ni sawa na kifo cha nyani kwamba miti yote huteleza.
 
MwanaDiwani labda huo ubaguzi umesaidia mno kwa CHADEMA kuwapiga CCM easily leo uchaguzi wa marudio Mbezi au?
 
Last edited by a moderator:
Chadema tafuteni mchagga akamrithi ubunge Zitto kigoma

Hawa jamaa hilo wanaliweza pia...hawatabiriki kabisa. Waliwahi kumsimamisha MMASAI agombee Ubunge CHALINZE kwa wakwere na wazaramo, ni kama vile wamechanganyika lakini ndivyo wanavyoendesha chama chao.

Wao kwao sifa ya kuwa kiongozi ni kutoka kasikazini na kuwa mkristo...mimi sio mtu wa kaskazini labda nipitie kwenye ukristo nitapata Kick.
 

Ni kweli angalia matokeo ya marudio uchaguzi wa aerikali za mitaa ya pale mbezi yanonyesha ni jinsi gani ubaguzi unavyo itesa cdm.pooole sana mkuu
 
WAKATI MNAINANGA CHADEMA. SOMA HII..............M
CHADEMA SASA HII NI KUTAFUTA SIFA BHANA. LZM IONYESHE UTU KWA CCM JAPO KIDOGO......

Chama cha Drmokrasia na Maendeleo- CHADEMA kimeisambaratisha vibaya Chama cha Mapinduzi -CCM katika uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa uliofanyika leo katika mtaa wa Kingazi Kwembe Mbezi DSM

Katika matokeo yaliyotangazwa muda huu hapa kituoni Chadema kimepata ushindi wa kimbunga wa kura 500 huku CCM wakiambulia kura 180

Ushindi huu ni aibu kubwa kwa CCM iliyopiga kampeni kufa na kupona kwa kutumia wabunge na baadhi ya mawaziri.

Ni shangwe kuu zimetanda kila mahali huku mamia ya wananchi wakipeperusha bendera za Chadema.
 
Ni kweli angalia matokeo ya marudio uchaguzi wa aerikali za mitaa ya pale mbezi yanonyesha ni jinsi gani ubaguzi unavyo itesa cdm.pooole sana mkuu

we waache wabwabwaje sisi tunazidisha imani kwa chadema.
 
MwanaDiwani labda huo ubaguzi umesaidia mno kwa CHADEMA kuwapiga CCM easily leo uchaguzi wa marudio Mbezi au?
Ndugu,
Hata shetani mpaka sasa yupo hapa duniani na anaendelea kugeuza binadamu pamoja na kwamba Mungu ana uwezo wa kumuondoa katika harakati zake.

Think deeply!
 
MwanaDiwani labda huo ubaguzi umesaidia mno kwa CHADEMA kuwapiga CCM easily leo uchaguzi wa marudio Mbezi au?

Ukizungumzia Mbezi unazungumzia wachaga na vigango vyao.Ndio sawa leo uzungumzie CUF ishinde Kibosho
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli angalia matokeo ya marudio uchaguzi wa aerikali za mitaa ya pale mbezi yanonyesha ni jinsi gani ubaguzi unavyo itesa cdm.pooole sana mkuu
Hata shetani anawatesa sana kila siku wana wa Mungu lakini hii haina maana kuwa Mungu hayupo.

Tafakari!
 
Ukizungumzia Mbezi unazungumzia wachaga na vigango vyao.Ndio sawa leo uzungumzie CUF ishinde Kibosho

Vipi kule sumbawanga nakwenyewe kuna wachaga wengi kama mbezi?vipi liwale nakwenyewe kuna wachaga wengi?vipi mtwara kuna wachaga wengi?vipi tandahimba kuna wachaga wengi?vipi nachingwea kuna wachaga wengi?punguza ndoto zako hizo na ukubali dawa ikuingie vema
 
We mjinga kwani watu wa sumbawaga na mbezi ni wachaga,hizo propaganda za ccm tumeshazizooeaa,walizusha adi udini ,
 
Huu unafiki wa CHEDEMA wakusema eti wanafanya maamuzi magumu wakuwatimua wanachama wenye msimamo kinzani ni woga tu...kumbe wanajificha kwenye kivuli cha woga, woga wa kunyang'anywa madaraka, woga wa viongozi wa kupingwa ama kushindwa kwa hoja
 
Ukizungumzia Mbezi unazungumzia wachaga na vigango vyao.Ndio sawa leo uzungumzie CUF ishinde Kibosho

With due respect
Kyela hamna wachaga na CHADEMA ikashinda kuongoza mamlaka ya mji mdogo kutoka vitongoji 2 mwaka 2009 hadi 28 mwaka huu

Nadhani kuna mwamko fulani umewaingia watz au una wazo gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…