UBAGUZI: Dunia imeipa kisogo YEMENI, why?

blessings

JF-Expert Member
Jul 9, 2012
7,428
7,092
Kwa nini jumuiya za kimataifa zimeipa kisogo Yemeni ikiwa katika machafuko ya kuuliwa wananchi wasio na hatia kwa muda sasa, lakini juzi Sudan Kusini wamepeana kidogo za Chembe, dunia nzima imelipuka kutaka kuingilia kati si UN, AU, IGAD, EAC lakini humsikii kiumbe yeyote pale Yemeni au Syria. WHY?
 
Unajua pale kuna shida kubwa sana ya kidini kati ya shia na suni.shia wana kikundi chao cha houth kinachopigana kuipinga serikali.lakini kumbuka kuwa ali-abdullah saleh anapambana kurejea mamlakani.kuhusiana na malighafi ni kweli yemen ni nchi hoi hivyo wakuu wa dunia hawaangaiki nako kivile.
 
Shia kawa rafiki mwingine kimaslahi wa marekani ckuiz....

Umaarufu wa masuni kuwa rafiki na amerika umepungua baada yakushinda dola nyingi za kisunni kama sadam , gardafi, afghanistan na kwingineko....,
Wanapigwa masunni wenye nguvu kwa msaada wa mashia....!!
Iran kaekwa kipolo tu.... Ngoja waishe nguvu masunni wageukiwe.....!!!

Uwa mnawaamiibi waamerika...., ivi hamuwajui au....!!!
 
Kwa nini jumuiya za kimataifa zimeipa kisogo Yemeni ikiwa katika machafuko ya kuuliwa wananchi wasio na hatia kwa muda sasa, lakini juzi Sudan Kusini wamepeana kidogo za Chembe, dunia nzima imelipuka kutaka kuingilia kati si UN, AU, IGAD, EAC lakini humsikii kiumbe yeyote pale Yemeni au Syria. WHY?

Yemen imezubaa mno.
 
Siasa za uarabuni kuzielewa inatakiwa uwe unashinda Aljazeera kidogo na BBC na RT na CNN CCTV na international forum za nchi mbalimbali ikiwemo uarabuni na website mbali mbali za kiislam Na kuwahoji infor wakina salim kikeke ndio utapata jibu kwa kuunganisha dot. Lakini mwisho wa siku lazima utaangukia Kwenye Islamic idealogy na Colonial Interest.
 
Watasema ni USA au Israel
Kuna mwingine (uliza Zaire,Somali,Iraq,Afghan,Libya,SS,Syria zipo wapi?)

Punde tusibiri... ila Mwenyeezi Mungu apishe mbali TAIFA la TZ !!

Maana siku TZ itakapoanza kuEXPORT gesi, mafuta, graphite in metamorphic rocks na madini adimu !!! basi juwa cheche na taharuki za waasi zitahusika....
chanzo cha machafuko huanzishwa na Rockfela (kama mnamjua vile)!! Historiya imeProve....

Hoshea
ustadhijuma
blessings
Rob Art
Jindal Singh
 
Kwa nini jumuiya za kimataifa zimeipa kisogo Yemeni ikiwa katika machafuko ya kuuliwa wananchi wasio na hatia kwa muda sasa, lakini juzi Sudan Kusini wamepeana kidogo za Chembe, dunia nzima imelipuka kutaka kuingilia kati si UN, AU, IGAD, EAC lakini humsikii kiumbe yeyote pale Yemeni au Syria. WHY?

Blessings Kama kawaida yako(KKY) ya udini.
Sio kweli kwamba Yemen Na Syria zimesuswa Na ulimwengu.Yemen wako wa Irani Na Wasaudi.WaIran wanasaidiwa na NKorea Na Urusi.Wasaudi wanasaidiwa Na WaMerikani Na NATO.Sema tu chuki zako Na Waarabu.
 
mmoja kati ya ndugu aliyekuwa anasoma dini Yemen,aliniambia,hayo mataifa yamekaa kimya kwa sababu wanaouliwa Kule ni wasunni,lau wao ndo wangefanya hayo mauaji,basis wangegaiwa jina LA ugaidi,na kutafutiwa mbinu ya kuwasambaratisha"mwisho wa kunukuu
 
Back
Top Bottom