Ubadilishaji wa Fedha za Sarafu: Tafadhali Banki Kuu simamieni !

Bandiwe

JF-Expert Member
Oct 19, 2013
9,530
3,556
Imekuwa kawaida sasa ukienda Banki nyingi ni shida kupata fedha za sarafu na wakati huo huo ni shida kuziwasilisha kwa ajili ya kuweka (depositing)
Kituo cha ITV kiliwahi kutoa coverage ya Kijana mmoja akisumbuliwa kukubaliwa kuzihifadhi hizo Fedha katika Banki mbali mbali. Hilo pia limesababisha vijana kuamua kufanya biashara ya kuuza 'chenji' ili kuwapunguzia usumbufu watu wa Dala Dala.

Ninachotaka kukionyesha hapa, kwa sasa kuna mfumuko wa bei unao sababishwa na ukosefu (au usumbufu wa kuzipata) wa fedha za sarafu, hivyo Maduka - haswa ya Supermarket ndogo ndogo au za kati na Bar na Migahawa wameamua kurahisisha malipo katika kuepuka adha ya usumbufu wa 'chenji'.
Bidhaa zozote zinazohitaji bei itakayo sababisha uhitaji wa sarafu (chenji) njia rahisi ni kurahisisha hesabu iliyo karibu.
Kwa mfano: kama bei ilitakiwa iwe Tsh 1,300/=, basi inaongezwa mpaka Tsh 1,500/=, ile ya Tsh 1,800/= inapelekwa mpaka Tsh 2,000/= mbaya zaidi bidhaa ya kuuza Tsh 1,600/= inaweza kurushwa mpaka Tsh 2,000/=

Nashauri Banki Kuu iagize kila Bank ifungue huduma ya kutoa na kupoke fedha za Sarafu ili kudhibiti hali hii !
Itakuwa inashangaza sana kwa Banki kuu kudai inadhibiti mfumuko wa bei wakati huo huo hali hii ikiendelea.

Nawasilisha.
 
Sisi branch yetu tuna sarafu nyingi sana.kuna had I vifuko vya laki 2.5. Had 1mil kiroba.ubaya hakuna atakaekubali umpe.ila ukitaka utapewa.ZIPO nyingi tu.
 
Sarafu ya sh.500 ni dili saivi! Huwezi kuona mtaani na ukiona ujue imetoka bank na soon inaenda kupotea
Sarafu ya sh.500 ni dili saivi! Huwezi kuona mtaani na ukiona ujue imetoka bank na soon inaenda kupotea
Sarafu ya sh.500 ni dili saivi! Huwezi kuona mtaani na ukiona ujue imetoka bank na soon inaenda kupotea
Sarafu ya sh.500 ni dili saivi! Huwezi kuona mtaani na ukiona ujue imetoka bank na soon inaenda kupotea
Inapotelea wapi mkuu??
 
Ni kweli kabisa vitu vinakadiriwa kwa bei za kigawo cha mia tano. Suala lingine la kuangaliwa ni uchakaaji mbaya wa fedha za noti hasa sh 500 na 2000. Kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wa maduka nk ni kawaida kupokea noti nyingi kile kikamba cha mstari kinachomoka au pamechanika. Sijui kama benki kuu wanaliona hili tatizo la hao watengezaji wa hela.
 
Back
Top Bottom