Ubadhirifu na ufisadi CHAURU

galama

New Member
Sep 9, 2012
1
0
Wakulima wa kilimo cha mpunga, kupitia chama chao cha CHAURU huko Ruvu mkoa wa Pwani wametendewa unyama mkubwa na viongozi wa chama hicho baada ya kukusanya pesa zao zikiwa ni gharama za kuendeshea kilimo hicho cha umwagiliaji, viongozi wameingia mitini na pesa hizo na kuwaacha wakulima hao wengine hawakupewa mashamba waliyoyalipia, huduma ya maji kwa waliolima haikutolewa kwa wakulima na mwisho wakulima hao hawakuvuna kitu toka kwenye mashamba hayo. Inashangaza sana kuona kwamba pamoja na vitendo hivi vya viongozi hao waliokosa aibu hata chembe wameshindwa kutoa maelezo yoyote juu ya hasara hii.

Wakulima tunaomba msaada wa serikali katika hili ikiwa ni pamoja na kutuletea mkaguzi wa nje kuja kukagua mapato na matumizi ya chama. Pili tunaomba tupatiwe wataalam wa kilimo kwani chama kina wababaishaji tu. Tatu hatuutaki uongozi uliopo madarakani kwani wapo kujinufaisha wao tu. Nne wawajibishwe kwa hasara waliosababisha.

Uongozi umekithiri kwa rushwa kwani kuna baadhi ya viongozi wakubwa serikalini wanalimiwa bure ili kuwanyamazisha wasiseme kuhusu maovu yanayotendeka pale. Viongozi wa Ushirika Mkoa na wilaya wamewekwa mfukoni na mwenyekiti kwani wanashirikiana kula fedha za ruzuku.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom