Ubadhilfu katika halmashauri za wilaya unaofanywa na wakurugenzi wa halmashauri ni moja ya mafanikio

Mussa Loth

Member
Apr 13, 2012
10
3
MAELEZO YA KATIBU MKUU
OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
(OWM-TAMISEMI)
Katika kipindi cha miaka 50 iliyopita, baadhi ya mafanikio yaliyopatikana
ni pamoja na:-
• Kuweka misingi na kuongeza kasi ya kupeleka madaraka kwa wananchi
kwa maana ya madaraka ya kisiasa, madaraka ya kusimamia watumishi,
madaraka ya kusimamia fedha na mabadiliko ya mahusiano kati ya
Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kupitia Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo
wa Serikali za Mitaa
• Kujenga misingi ya Utawala Bora katika ngazi ya Serikali za Mitaa na
kueleweka kwa wananchi kiasi cha kuanza kujua haki na wajibu wao na
Halmashauri kutambua umuhimu wa kuwajibika kwa wananchi na ulazima
wa kuwa wazi katika kuendesha shughuli za Halmashauri.
• Kutokana na elimu ya uraia kuhusu wajibu na umuhimu wa wananchi
kushiriki katika shughuli za maendeleo, ari yao katika kutekeleza shughuli
zinazohusu maendeleo yao ikiwa ni pamoja na Mpango wa Maendeleo ya
· Kuongezeka kwa raslimali fedha zinazopelekwa katika Mamlaka ya
Serikali za Mitaa kwa kuzingatia vigezo vya usawa na hivyo kuimarisha
viwango vya utoaji huduma
Source: http://www.tanzania.go.tz/wizara/tamisemi.pdf
Maoni yangu.
Hivi karibuni imethibitika kuwa Halmashauri nyingi ambazo zilipelekewa fedha za miradi zimetafunwa na wenye meno na kwa mujibu wa taarifa ya miaka 50 iliyotolewa KM-TAMISEMI, taarifa hii inaashiria nini kwa Umma wa watanzania kuhusu taarifa za serikali?
Kwa mujibu wa sheria za Tanzania wabunge ni madiwani pia, je madudu yaliyo na yanayofanywa na wakurugenzi wa halmashauri wabunge walipaswa kuyaona wakiwa bungeni?
mambo haya ya ubaadhilifu wa fedha za umma yalipaswa kuonwa na wakaguzi wa ndani kwanza kabla ya CAG au chombo kingine chochote je, kuna haja ya kuwachukulia hatua wakaguzi hawa kwa kutowajibika au kwa kushirikiana kuficha na kula fedha za umma na watuhumiwa.
Nini kifanyike?
 
Tuna hasara kubwa kwa serikali iliyoko madarakani.
Hawana maana hata kidogo ya kuwepo kwao!
Iliyo ni mabadiliko tu!

Uone kama Tanzania haijawa kama Ulaya ya Afrika.
 
We acha tu. Kuna mtu alijiuzulu uhasibu bada ya ya kushinikizwa atie saini katika karatasi blank ambapo pesa iliyosomwa bungeni katika bajeti, wilayani mhasibu hakuona hata senti! Alafu unaambiwa anguka hapo.....!NCHI CHI HII INAHITAJI TU MABADILIKO YA SERIKALI YOTE.
 
Back
Top Bottom