Mcheza Karate
JF-Expert Member
- Jun 30, 2011
- 690
- 350
Kumekuwako na malalamiko mengi ndani ya chama Cha CHADEMA kuwa viongozi wake wamekuwa miungu watu na wmamekifanya chama kuwa ni chama cha kifamilia. Napenda nitoe mifano kadhaa mwisho nitahitimisha na maswali ya tafakuri.
Mwaka 1964, aliyekuwa rais wa chama cha Uganda peoples congress(UPC) bwana Milton Obote aliona kuna kila dalili ya kupingwa ndani ya chama kwa kile kilichodaiwa kuwa alikuwa "mungu mtu" ndani ya chama.
Alichokifanya ktk mkutano mkuu wa chama uliofanyika Guru, Uganda mwaka huo ni kuamuru zichapwe kadi tofauti na zile za kawaida ili wale ambao 'hawamfurahishi' wakose nafasi ya kupiga kura.
Alifanikiwa njama zake hizo na hatimaye akachaguliwa tena kuwa rais na mwisho akaamuru katiba ibadilishwe na yeye awe anamteua katibu mkuu wa chama.
Mwaka 1967 waliokuwa wabunge machachari wa TANU, Eli Anangisye, Mwafitwange na akina Chonge na wenzao walifukuzwa uanachama ndani ya TANU kwa kile tu kilichodaiwa "mwenyekiti" (mwl. Nyerere) na sekretarieti kuu ya TANU kuwaona wabunge hao wanaenda kinyume na "MATAKWA" ya chama.
Dhambi ya kusema tofauti na wanayonena wenzao ikawatafuna wabunge wale.
Mwaka 1997 aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Agustine Mrema aliunda zengwe la maksudi kwa lengo la kutaka kuwa mungu mtu ndani ya chama.
Ktk mkutano wa kamati kuu uliofanyika mjini Tanga tarehe mei 14, 1997 Mrema aliawaomba wajumbe wa mkutano "WAMSAIDIE" kumwondoa katibu mkuu bwana Mabere Marando ktk nafasi yake kwa vile Marando anaunda zengwe akishirikiana na katibu mkuu wa CCM(wakati huo Laurent Gama) ili "WAMMALIZE" bwana Mrema.
Kwa bahati mbaya na aibu kubwa mkutano ule ulivurugika siku ile. Mrema alienda mbali zaidi pale tarehe 7/mei/1997 alipowaita baadhi ya wajumbe kutoka Zanzibar na kuwahonga ili "wamsaidie" kumtoa bwana Marando.
Lakini jinamizi hilo lilikuwa mwendelezo tu kwani miezi michache nyuma bwana Prince Bagenda, katibu mkuu na Mashaka Nindi(chimoto), naibu katibu mkuu walijiuzulu nafasi zao kwa vile "MWENYEKITI ALIKUWA MUNGU MTU".
Miezi michache nyuma NCCR-Mageuzi chini ya "sultani" Wake James Mbatia iliwafukuza uandacha mbunge wa kigoma kusini David Mafulila, mgombea wa urais kupitia chama hicho mwaka 2010 bwana Rungwe Hashim na wenzao kwa vile tu "mwenyekiti" aliamini kuna njama zinafanywa "ili yeye ang'oke na yeye kwa vile ndio mwenye chama akawang'oa wasio na chama".
Ni mwendelezo ule ule wa ubabe wa wenyeviti wa vyama.
Miaka ya 2000 mwanzoni bwana Erasto Tumbo alifukuzwa UDP kwa vile tu alienenda tofauti na "mwenyekiti" wake. Kijana wa watu akaondoka huku akiipenda UDP lakini akimchukia na kumdharau mwenyekiti dikteta.
Miezi michache tena iliyopita bundi huyo alitua CUF, chama ambacho wengi wanaamini kuna usultani mbichi. Mbunge wa Wawi na na aliyewahi kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Hamad Rashidi alifukuzwa uanachama.
Kikubwa kinachoaminiwa Hamad kufukuzwa ni kwenda tofauti na Seif kwa kuonesha nia ya kugombea ukatibu mkuu ili mwaka 2015 agombee urais visiwani.
Seif akamwona Rashid ni adui yake na anahatarisha "USALAMA WAKE" akaunda kazengwe ka kumwondoa mwenzie na akafanikiwa.
Maalim Seif na Hamad rashidi wana historia zinazolingana na ni marafiki wa muda mrefu. Kwani wote walifukuzwa kutoka CCM kwa kile tu walichobainika kuwa ni "vinyonga" .
Leo mwenzake akamfanya kafara. Ama kweli viongozi wa kiafrika ni "walevi".
Sasa niwaulize ndugu zangu kwa mifano hiyo ya juu kuna haja ya kuwalaumu CHADEMA? Kuna haja ya kumlaumu Mbowe au Slaa kuwa ni miungu watu? Kuna haja ya kulaumu kuwa viongozi wa CHADEMA wanapendeleana?
Hizi siasa za umwinyi zimeenea kote barani Afrika. Ni mwendelezo wa kile "wakubwa" wanachoamini ni kulinda nidhamu ndani ya chama.
Je tuendelee kupiga makelele au tuache ikijengwa nidhamu ya chama?
Mimi binafsi sina chama(nitangaze parsonal interest mapema) ila nina kaupenzi kwa mbali na CHADEMA.
Ila kwa hili naomba tujadili kwa kina ili tujiridhishe sote.
Nawasilisha!