Ubabe wa CHADEMA na historia ya ujenzi wa nidhamu ndani ya vyama

Mcheza Karate

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
690
350
Kumekuwako na malalamiko mengi ndani ya chama Cha CHADEMA kuwa viongozi wake wamekuwa miungu watu na wmamekifanya chama kuwa ni chama cha kifamilia. Napenda nitoe mifano kadhaa mwisho nitahitimisha na maswali ya tafakuri.

Mwaka 1964, aliyekuwa rais wa chama cha Uganda peoples congress(UPC) bwana Milton Obote aliona kuna kila dalili ya kupingwa ndani ya chama kwa kile kilichodaiwa kuwa alikuwa "mungu mtu" ndani ya chama.

Alichokifanya ktk mkutano mkuu wa chama uliofanyika Guru, Uganda mwaka huo ni kuamuru zichapwe kadi tofauti na zile za kawaida ili wale ambao 'hawamfurahishi' wakose nafasi ya kupiga kura.

Alifanikiwa njama zake hizo na hatimaye akachaguliwa tena kuwa rais na mwisho akaamuru katiba ibadilishwe na yeye awe anamteua katibu mkuu wa chama.

Mwaka 1967 waliokuwa wabunge machachari wa TANU, Eli Anangisye, Mwafitwange na akina Chonge na wenzao walifukuzwa uanachama ndani ya TANU kwa kile tu kilichodaiwa "mwenyekiti" (mwl. Nyerere) na sekretarieti kuu ya TANU kuwaona wabunge hao wanaenda kinyume na "MATAKWA" ya chama.

Dhambi ya kusema tofauti na wanayonena wenzao ikawatafuna wabunge wale.

Mwaka 1997 aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Agustine Mrema aliunda zengwe la maksudi kwa lengo la kutaka kuwa mungu mtu ndani ya chama.

Ktk mkutano wa kamati kuu uliofanyika mjini Tanga tarehe mei 14, 1997 Mrema aliawaomba wajumbe wa mkutano "WAMSAIDIE" kumwondoa katibu mkuu bwana Mabere Marando ktk nafasi yake kwa vile Marando anaunda zengwe akishirikiana na katibu mkuu wa CCM(wakati huo Laurent Gama) ili "WAMMALIZE" bwana Mrema.

Kwa bahati mbaya na aibu kubwa mkutano ule ulivurugika siku ile. Mrema alienda mbali zaidi pale tarehe 7/mei/1997 alipowaita baadhi ya wajumbe kutoka Zanzibar na kuwahonga ili "wamsaidie" kumtoa bwana Marando.

Lakini jinamizi hilo lilikuwa mwendelezo tu kwani miezi michache nyuma bwana Prince Bagenda, katibu mkuu na Mashaka Nindi(chimoto), naibu katibu mkuu walijiuzulu nafasi zao kwa vile "MWENYEKITI ALIKUWA MUNGU MTU".

Miezi michache nyuma NCCR-Mageuzi chini ya "sultani" Wake James Mbatia iliwafukuza uandacha mbunge wa kigoma kusini David Mafulila, mgombea wa urais kupitia chama hicho mwaka 2010 bwana Rungwe Hashim na wenzao kwa vile tu "mwenyekiti" aliamini kuna njama zinafanywa "ili yeye ang'oke na yeye kwa vile ndio mwenye chama akawang'oa wasio na chama".

Ni mwendelezo ule ule wa ubabe wa wenyeviti wa vyama.

Miaka ya 2000 mwanzoni bwana Erasto Tumbo alifukuzwa UDP kwa vile tu alienenda tofauti na "mwenyekiti" wake. Kijana wa watu akaondoka huku akiipenda UDP lakini akimchukia na kumdharau mwenyekiti dikteta.

Miezi michache tena iliyopita bundi huyo alitua CUF, chama ambacho wengi wanaamini kuna usultani mbichi. Mbunge wa Wawi na na aliyewahi kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Hamad Rashidi alifukuzwa uanachama.

Kikubwa kinachoaminiwa Hamad kufukuzwa ni kwenda tofauti na Seif kwa kuonesha nia ya kugombea ukatibu mkuu ili mwaka 2015 agombee urais visiwani.

Seif akamwona Rashid ni adui yake na anahatarisha "USALAMA WAKE" akaunda kazengwe ka kumwondoa mwenzie na akafanikiwa.

Maalim Seif na Hamad rashidi wana historia zinazolingana na ni marafiki wa muda mrefu. Kwani wote walifukuzwa kutoka CCM kwa kile tu walichobainika kuwa ni "vinyonga" .

Leo mwenzake akamfanya kafara. Ama kweli viongozi wa kiafrika ni "walevi".

Sasa niwaulize ndugu zangu kwa mifano hiyo ya juu kuna haja ya kuwalaumu CHADEMA? Kuna haja ya kumlaumu Mbowe au Slaa kuwa ni miungu watu? Kuna haja ya kulaumu kuwa viongozi wa CHADEMA wanapendeleana?

Hizi siasa za umwinyi zimeenea kote barani Afrika. Ni mwendelezo wa kile "wakubwa" wanachoamini ni kulinda nidhamu ndani ya chama.

Je tuendelee kupiga makelele au tuache ikijengwa nidhamu ya chama?

Mimi binafsi sina chama(nitangaze parsonal interest mapema) ila nina kaupenzi kwa mbali na CHADEMA.

Ila kwa hili naomba tujadili kwa kina ili tujiridhishe sote.

Nawasilisha!
 
kichwa cha habari na habari havifanani sawasawa.Nilitegemea utaeleza kwa kina na kwa mifano ya wazi kwamba ni kivipi chadema ni wababe lakini nimesoma kwa makini maandiko yako sijaona unakothibitisha au walau kuonesha ubabe wa CHADEMA.Nilichoona ni wewe Kumtaja Mbowe na Slaa na kudai ni miungu watu lakini hujasema wamefanya je!.sijui unaweza kuweka wazi kinachokukera inawezekana una jambo la muhimu na hapo ndipo watu watakapojadili "facts" zaidi ya hapo tegemea "emotions".

Mwaka 1967 waliokuwa wabunge machachari wa TANU, Eli Anangisye, Mwafitwange na akina Chonge na wenzao walifukuzwa uanachama ndani ya TANU kwa kile tu kilichodaiwa "mwenyekiti" (mwl. Nyerere) na sekretarieti kuu ya TANU kuwaona wabunge hao wanaenda kinyume na "MATAKWA" ya chama.
kwa maoni yako mtu akienda kinyume na matakwa ya chama unashauri afanywe nini?

Sasa niwaulize ndugu zangu kwa mifano hiyo ya juu kuna haja ya kuwalaumu CHADEMA? Kuna haja ya kumlaumu Mbowe au Slaa kuwa ni miungu watu? Kuna haja ya kulaumu kuwa viongozi wa CHADEMA wanapendeleana?
Hali hiyo ikithibitika kitaalam wanapaswa kulaumiwa.
 
ndio niko njiani naenda mwenzangu si ulishachukua?

uswaz.jpg
 
Katika cdm hakuna ubabe bali uwajibikaji na uwajibishwaji pale inapobainika kuna msaliti katika kazi ya ukombozi wa taifa hili.
 
Mfano mwingine ni jinsi ambavyo Mwenyekiti wa sasa wa CCM, mara baada ya kupata Urais na uenyekiti wa CCM alivyowaengua viongozi wa CCM ambao hawakuwa wanamtandao!

Alianzia na Katibu Mkuu Mzee Philip Mangula na kumweka mwanamtandao Yusuf Makamba, list ni ndefu sana.
 
asante kwa kuongeza mifano HAI
 
Kumekuwako na malalamiko mengi ndani ya chama Cha CHADEMA kuwa viongozi wake wamekuwa miungu watu na wmamekifanya chama kuwa ni chama cha kifamilia. Napenda nitoe mifano kadhaa mwisho nitahitimisha na maswali ya tafakuri.

Mwaka 1964, aliyekuwa rais wa chama cha Uganda peoples congress(UPC) bwana Milton Obote aliona kuna kila dalili ya kupingwa ndani ya chama kwa kile kilichodaiwa kuwa alikuwa "mungu mtu" ndani ya chama.

Alichokifanya ktk mkutano mkuu wa chama uliofanyika Guru, Uganda mwaka huo ni kuamuru zichapwe kadi tofauti na zile za kawaida ili wale ambao 'hawamfurahishi' wakose nafasi ya kupiga kura.

Alifanikiwa njama zake hizo na hatimaye akachaguliwa tena kuwa rais na mwisho akaamuru katiba ibadilishwe na yeye awe anamteua katibu mkuu wa chama.

Mwaka 1967 waliokuwa wabunge machachari wa TANU, Eli Anangisye, Mwafitwange na akina Chonge na wenzao walifukuzwa uanachama ndani ya TANU kwa kile tu kilichodaiwa "mwenyekiti" (mwl. Nyerere) na sekretarieti kuu ya TANU kuwaona wabunge hao wanaenda kinyume na "MATAKWA" ya chama.

Dhambi ya kusema tofauti na wanayonena wenzao ikawatafuna wabunge wale.

Mwaka 1997 aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Agustine Mrema aliunda zengwe la maksudi kwa lengo la kutaka kuwa mungu mtu ndani ya chama.

Ktk mkutano wa kamati kuu uliofanyika mjini Tanga tarehe mei 14, 1997 Mrema aliawaomba wajumbe wa mkutano "WAMSAIDIE" kumwondoa katibu mkuu bwana Mabere Marando ktk nafasi yake kwa vile Marando anaunda zengwe akishirikiana na katibu mkuu wa CCM(wakati huo Laurent Gama) ili "WAMMALIZE" bwana Mrema.

Kwa bahati mbaya na aibu kubwa mkutano ule ulivurugika siku ile. Mrema alienda mbali zaidi pale tarehe 7/mei/1997 alipowaita baadhi ya wajumbe kutoka Zanzibar na kuwahonga ili "wamsaidie" kumtoa bwana Marando.

Lakini jinamizi hilo lilikuwa mwendelezo tu kwani miezi michache nyuma bwana Prince Bagenda, katibu mkuu na Mashaka Nindi(chimoto), naibu katibu mkuu walijiuzulu nafasi zao kwa vile "MWENYEKITI ALIKUWA MUNGU MTU".

Miezi michache nyuma NCCR-Mageuzi chini ya "sultani" Wake James Mbatia iliwafukuza uandacha mbunge wa kigoma kusini David Mafulila, mgombea wa urais kupitia chama hicho mwaka 2010 bwana Rungwe Hashim na wenzao kwa vile tu "mwenyekiti" aliamini kuna njama zinafanywa "ili yeye ang'oke na yeye kwa vile ndio mwenye chama akawang'oa wasio na chama".

Ni mwendelezo ule ule wa ubabe wa wenyeviti wa vyama.

Miaka ya 2000 mwanzoni bwana Erasto Tumbo alifukuzwa UDP kwa vile tu alienenda tofauti na "mwenyekiti" wake. Kijana wa watu akaondoka huku akiipenda UDP lakini akimchukia na kumdharau mwenyekiti dikteta.

Miezi michache tena iliyopita bundi huyo alitua CUF, chama ambacho wengi wanaamini kuna usultani mbichi. Mbunge wa Wawi na na aliyewahi kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Hamad Rashidi alifukuzwa uanachama.

Kikubwa kinachoaminiwa Hamad kufukuzwa ni kwenda tofauti na Seif kwa kuonesha nia ya kugombea ukatibu mkuu ili mwaka 2015 agombee urais visiwani.

Seif akamwona Rashid ni adui yake na anahatarisha "USALAMA WAKE" akaunda kazengwe ka kumwondoa mwenzie na akafanikiwa.

Maalim Seif na Hamad rashidi wana historia zinazolingana na ni marafiki wa muda mrefu. Kwani wote walifukuzwa kutoka CCM kwa kile tu walichobainika kuwa ni "vinyonga" .

Leo mwenzake akamfanya kafara. Ama kweli viongozi wa kiafrika ni "walevi".

Sasa niwaulize ndugu zangu kwa mifano hiyo ya juu kuna haja ya kuwalaumu CHADEMA? Kuna haja ya kumlaumu Mbowe au Slaa kuwa ni miungu watu? Kuna haja ya kulaumu kuwa viongozi wa CHADEMA wanapendeleana?

Hizi siasa za umwinyi zimeenea kote barani Afrika. Ni mwendelezo wa kile "wakubwa" wanachoamini ni kulinda nidhamu ndani ya chama.

Je tuendelee kupiga makelele au tuache ikijengwa nidhamu ya chama?

Mimi binafsi sina chama(nitangaze parsonal interest mapema) ila nina kaupenzi kwa mbali na CHADEMA.

Ila kwa hili naomba tujadili kwa kina ili tujiridhishe sote.

Nawasilisha!

Analysis nzuri hii, japo nina mashaka panaweza kuwa na majumuisho ya mkato sana katika maeneo fulanifulani. Mfano ni katika kudhani kila palipotokea mgongano kati ya kundi na kiongozi mkuu wa chama husika basi sababu lazima ilikuwa ulinzi binafsi wa nafasi ya kiongozi mkuu.

Ile analysis ya Obote sina tatizo sana nayo. Hizi nyingine nina mashaka nazo. Hasa kuhusu Nyerere na kina Anangisye na kina Mwakitwange.

Vyama vyote vya siasa vinakuwa na Memorandum and Articles of Association zao. Ziite katiba ukitaka. Tungechambua kila mgogoro katika hivi vyama na kupima migogoro hiyo kwa kutumia kipimo cha hizo katiba, sera na makubaliano mengine ndani ya chama, nina hakika migogoro mingine chanzo chake si uchu wa uungu mtu kama unavyotaka tuamini ndiyo sababu kila mahali.

Baada ya maelezo haya, ningependa kukubaliana nawe katika msimamo wa msingi wa hoja yako: kwamba uungu mtu katika taasisi yoyote si kitu kizuri, bila kujali ni taasisi ya kisiasa, taasisi ya kiserikali, au hata kama ni taasisi ya kibiashara. hilo huwa linafuta creativity katika taasisi na kudumaza mchango kutoka kwa watu wengine.

Nadharia ya uungu mtu katika taasisi yoyote ni kitu cha kupiga vita, lakini tusifanye hivi kwa kulazimisha kwamba tatizo hili ndio lilikuwa kiini cha migogoro yote katika vyama vya siasa Tanzania. Upo uwezekano wa wivu na tamaa za nafasi za juu katika vyama hivi miongoni mwa watu walokuwapo kwenye nafasi za chini. Nalo hili tusilifumbie macho.
 
Nidhamu ni muhimu sana. Na hapa lazima muweze kutofautisha nidhamu na ukambi/mtandao, cdm inahitaji nidhamu. Hivi watu kama wakina mwampanda ,Juliana Shonza ukiwaondoa kwenye chama ni kuwaonea? watu kama wakina shibuda??? Kuna tofauti kubwa kati ya mtandao na nidhamu,na mtambue msafara wa mamba na kenge wamo!!!!!!!!!!!
 
Mleta hoja, ndani ya taasisi yoyote NIDHAMU ni jambo la msingi. Mifano yako ya Uganda, TANU, NCCR, UDP, CUF hairandani kabisa na kichwa cha habari. Ujue kabisa ndan ya vyama vyote makini, zipo kanuni zinazotoa adhabu kawa zitakiukwa ikiwemo kufukuzwa mfano Katiba ya CHADEMA Ibara ya 5. ukisoma utaona "Taratibu za kuwa, na kupoteza uwanachama" ukilijua hilo hata iweje huwez kuhukumiwa. Ila kama utagundua hila za viongoz na ukapata ushahidi, zipo hatua kudeal na hilo. Ila kwa ufupi hoja yako ni dhaifu, mwambie mod aiondoe. CDM ni "THE STONGEST INST..." Adios...
 
duh lumbumby kweli wameamua safari hii. uwenda kuna tender pale ya kupost jamii forums kila baada ya dk 10 habari ya chadema . kweli chadema inawanyima usingizi kiama 2015.
 
Back
Top Bottom