Uasi wanukia CHADEMA

Uasi wanukia CHADEMA

Dr. Ndimu

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2012
Posts
717
Reaction score
146
Katika gazeti la Fahamu la januari 22 kuna habari inayosema zaidi ya asilimia 60 ya wabunge wa CHADEMA wanaweza kuachia ngazi baada ya uchaguzi wa ndani wa chama hicho endapo mbowe ataendelea kuwagawa ktk mbio za urais 2015.

Yameandikwa mengi lakin imeelezwa pia wabunge wakikaa kikao ktk hoteli moja magomeni na kujadili kauli ya Mbowe kumpigia upatu Dk. Slaa na kufikia conclusion kuwa ina madhara ya kukigawa chama.

Na mbunge mmoja aliweka bayana kwa mwandishi kuwa demokrasia isipozingatiwa watafanya uamuzi mzito ikiwa ni pamoja na kujienguaili kulinda heshima zao na wapigakura wao. Mambo yanazidi kupamba moto CHADEMA, mtafika kweli 2015?
 
Waache watoke, kuna wanaCDM zaidi ya millioni wenye sifa zaidi ya hao na wanauchungu na nchi yetu.
 
Ktk gazeti la Fahamu la januari 22 kuna habari inayosema zaidi ya asilimia 60 ya wabunge wa cdm wanaweza kuachia ngazi baada ya uchaguzi wa ndani wa chama hicho endapo mbowe ataendelea kuwagawa ktk mbio za urais 2015.yameandikwa mengi lakin imeelezwa pia wabunge wakikaa kikao ktk hoteli moja magomenina kujadili kauli ya mbowe kumpigia upatu dk.slaa na kufikia conclution kuwa ina madhara ya kukigawa chama. Na mbunge mmoja aliweka bayana kwa mwandishi kuwa demokrasia isipozingatiwa watafanya uamuzi mzito ikiwa ni pamoja na kujienguaili kulinda heshima zao na wapigakura wao. Mambo yanazidi kupamba moto cdm, mtafika kweli 2015?
Ningefurahi sana kama ZZK angeondoka na panya wake jana/juzi.
Ningefurahi sana kama SHIBUDA angekimbia bila kufukuzwa toka mwaka jana!!
Let them GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!! Traitors!!
 
chadema ina watu wengi sana zaidi ya milioni 4.majimbo hayazidi 400.tutagombea wengine.WAONDOKE TU.
 
Chadema siyo Wabunge, Chadema ni Umma wa Watanzania ambao ndio wengi. Imani yetu Watanzania haiko juu ya mtu yeyote ila juu ya Chadema kama Chama.
 
Bila kuiandika CDM gazeti halijauzwa. Uzuri ni kwamba Brand recognition inaongezeka hope by 2015 hakuna kiumbe ndani ya hii ambaye hataifaham CDM na hivyo kuipa kura yake.

Waambie hao wabunge kuwa NO INDIVIDUAL IS BIGGER THAN CHADEMA
 
Heshima na harakati za kujikomboa na umasikini kipi ni bora??? kama watajali heshima za kisiasa kuliko maslahi ya taifa letuu huo ni ujinga...... Tatizo la akili ndogo zinajua unafki ndo utaharibu cdm...
 
Ningefurahi sana kama ZZK angeondoka na panya wake jana/juzi.
Ningefurahi sana kama SHIBUDA angekimbia bila kufukuzwa toka mwaka jana!!
Let them GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!! Traitors!!

hapa tatizo shule tu
 
Naona leo mnabadilik,nyie si ndio mnaowasifia hapa hata wakifanyaga upuuzi,mesikia wanataka kuondoka leo mnawaona si kitu,taftane na mzisawazishe changamoto badala ya kuminya demokrasia mana matatiyo yake mnayaona.shauri enu
 
chadema ina watu wengi sana zaidi ya milioni 4.majimbo hayazidi 400.tutagombea wengine.WAONDOKE TU.
yaani mna wanachama wachache kiasi hicho bado tu mnashabikia makundi na kufukuzana?
 
magazeti mengine bana... sasa fahamu ndo gazeti gani!!? au wamelifupisha linaitwa mtindio wa Fahamu! aargh?? mhariri wake wake lazima awe mgulu mchemba!
 
Lisemwalo lipo kama halipo laja

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Vigogo wote wa CCM kuanzia Wassira walishatabiri kwamba CDM kitakufa kabla 2015. Sasa hao wabung 60 wa CDM watakaoasi 2015, wataasi chama gani wakati CDM kitakuwa TAYARI KIMESHAKUFA?! Sijawahi kusikia marehemu wAKIASI marehemu wenzake.

Ukiwa muongo basi lazima pia uwe na kumbukumbu
 
Back
Top Bottom