Hivi ndivyoo walivyomaanishaa acha uhuni.
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dorothy Mwanyika, awasimamishe kazi wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi ya Wilaya ya Karagwe na Kibaha kutokana na kulalamikiwa na wananchi kupokea rushwa.Lukuvi amewataja wenyeviti hao kuwa ni Rugate Assey wa Karagwe na Jerome Njiwa wa Kibaha.Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dodoma, Waziri Lukuvi alisema katika kutatua migogoro ya ardhi, wizara imeunda mabaraza ya ardhi na nyumba ya wilaya 97 kwa ajili ya kushu-ghulikia utatuzi wa migogoro ya ardhi kwa mujibu wa Sheria ya Mahakama na Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi Sura 216.“Nimekuwa nikipokea tuhuma kuhusu utendaji wa wenyeviti wa mabaraza ya ardhi na nyumba ya wilaya hususani mabaraza ya Wilaya ya Karagwe na Kibaha.“Kwa mamlaka niliyonayo, namwagiza Katibu Mkuu kuanzia leo (jana), kuwasimamisha kazi hao wenyeviti ili kupisha uchunguzi.“Waliosimamishwa ni Rugate Assey, Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ya Karagwe na Jerome Njiwa Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ya Kibaha.“Tuhuma ni kwamba wamelalamikiwa na watu wengi kwamba wanapokea rushwa,” Waziri Lukuvi alisema.I