Viporo vinazidi kuongezeka, wakati mtu anafikiria ni lini uboreshaji wa daftari la wapiga kura utafanyika, kichwani ana utoaji wa vitambulisho vya uraia. Hapo kuna taasisi mbili tofauti, nida na tume ya uchaguzi ambazo hazishirikiani, moja inaenda kushoto na nyingine inaende kulia.Nida wana karibu miaka miwili tangu waanze zoezi hilo lakini sina hakika kama watakuwa washamaliza angalau wilaya kumi. Mwezi wa kumi ni uchaguzi wa serikali za mitaa, daftari halijaboreshwa na huku wanasema vitambulisho tulivyonavyo mwaka huu havitatumika, lazima vitolewe vipya, Wale waliopata bahati na kupatiwa vitambulisho vya uraia wanaambiwa hivyo havitatumika kwenye uchaguzi. Kuliko kuua ndege wawili kwa jiwe moja ili kupunguza gharama wao wanataka kila taasisi ifanye kazi kivyake, tutafika kweli. Hiki kitambulisho cha uraia ambacho hakinipi nafasi ya kupiga kura kazi yake ni nini hasa. Nchi hii bwana, mtu mmoja anakuwa na vitambulisho zaidi ya kumi, anakuwa na kitambulisho cha: kupiga kura, uraia, CRDB banki, NMB banki, cha kazi, cha kumwekea mtu dhamana mahakamani, cha bima, cha harusi, cha kuingilia mkutanoni, cha kumaliza darasa la saba, sekondari na chuo, cha kumiliki gari na pikipiki. Taarifa katika vitambulisho vyote hivi ingeweza kupatikana katika kimbulisho kimoja tu cha uraia. Nchi hii bwana ni bora liende.