Bwai
JF-Expert Member
- Aug 2, 2011
- 721
- 488
Hello! Brothers and sisters, hope mnaendelea na wkend vizuri. Imekuwa mda sasa hatujawa pamoja, ila naamini hakuna kilichoharibika na wadau wa MMU mnaendelea na majukumu ya ujenzi wa jamii yetu. Nimekuja na tatizo, nina very best friend of mine amejiunga na jeshi baada tu ya kuhitimu elimu ya juu, bado yupo depo. Alichonisimulia ndicho ambacho kimenilazimu kuja MMU kuwa ombeni ushauri. Alichonisimulia ni kama ifuatavyo: Rafiki yangu ana mpenzi wake wa mda mrefu na anampenda kweli ila tatizo ni kuwa demu wake hataki jamaa kuwa mwanajeshi, na hii inatokana na parception aliyonayo kuhusu wanajeshi ya kuwa ni wakatili, wazinzi, wababe n.k. Ki ukweli mimi rafiki yake nimejitwisha mzigo wa kwenda kumshauri kipenzi cha rafiki yangu us you know rafiki ni zaidi ya ndugu, najipanga niende nikaongee naye ana kwa ana. Kati ya ninayomwamini huyu rafiki yangu ni kuwa si wa mambo ambayo yeye anayadhania, kutokana na hilo ndo maana nimekubali kumsaidia rafiki yangu. Please ushauri wenu ni muhimu wadau.