Peter Mwaihola
JF-Expert Member
- Jun 23, 2022
- 289
- 489
TUJENGE HOJA HAPA
Kwenye harakati za kisiasa inaelezwa kuwa kadri harakati zinavyopamba moto ndivyo wanaharakati hupitia wakati mgumu ikiwemo kuwekwa kizuizini wakati mwingine hata kupoteza maisha kwa sababu hakuna dora inayokubali mageuzi kwa wepesi pasipo kuyalinda kwanza.
Zimbabwe alikwepo mwanaharakati na mwanasiasa Morgan Tshangirai akafariki kwa utata, Ukienda Uganda utasikia habari za nguli wa vita vya msituni mwanasiasa mkongwe Kiiza Besidye ambaye anasota lupango kwa masaibu ya kuipinga serikali ya Museveni.
Tukisalia hapo hapo Uganda mwana mama Stella Nyanzi ni miongoni mwa wanawake waliopitia mateso, dhulma na vikwazo kwa sababu ya kupigania megeuzi ya kiutawala nchini Uganda.
Nchini Afrika Kusini yupo Julius Malema kiongozi mkuu wa chama cha Economic Freedom Fighters, EFF. Malema ni mwiba mkali wenye msimamo wa kijamaa unaochoma kwenye makalio ya Serikali ya Rais Cyril Ramaphosa na chama kiongozi cha ANC.
Malema amepitia misukosuko mingi ya mashtaka mbalimbali za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha lakini bado anadunda kiasi cha kumchefua hadi Rais wa Marekani Donald Trump juu ya mtazamo wake mkali dhidi ya watu weupe wa Afrika Kusini.
Sio Afrika tu ambako wanaharakati hupitia kwenye tanuri la moto hata kwingineko duniani mambo ni ya moto.
Alexei Navalny mwanaharakati na mpinga ufisadi na rushwa nchini Urusi alishikiliwa hadi umauti ulimpopata akiwa gerezani 2024.
Navalny hakuwa gaidi wala mhaini alianzisha taasisi ya kupinga rushwa, Anti-corruption Foundation hata hivyo hakupendwa kabisa na mamlaka za nchi hiyo akafungwa kifungo chenye utata.
Historia ya maisha ya wanaharakati mashuhuri duniani kama Martin Luther King Jr, Malcom X, Nelson Mandela na wengine ni ushahidi tosha kuwa harakati za mageuzi sio kazi rahisi inahitaji moyo na kujitoa sadaka.
© Peter Mwaihola