Marekani (MCC) wametunyima shilingi trilioni moja (1) kwa sababu zao wanazozijua (na sio marudio ya uchaguzi Zanzibar wala sheria za mitandao. Mengi yamekwisha zungumzwa mitandaoni sina haja ya kuyanukuu).
Sasa tufanyeje?
1. Tuendelee tu kuwa na uhusiano mwema na Marekani na mataifa mengine duniani. Tusiwakashifu MCC. Wana sababu zao na wanatekeleza majukumu yao. Sisi ilikuwa tupokee fadhila zao tu, wametunyima basi hakuna nongwa - haina haja ya kuwashutumu au kuwakejeli.
2. MUHIMU - Tusisitishe mipango tuliyokuwa nayo ambayo ingelipiwa na MCC-2. Tunaweza kutafuta wasimamizi wengine (mfano, sio SYMBION) wa kuendeleza hii miradi bali isisimame. Kuna wananchi wengi wamekaa mkao wa kula wakisubiri umeme na maji - tusiwaangushe.
Sasa fedha zitatoka wapi?
Sasa hivi tunakusanya (TRA) kati ya trilioni 1.2 hadi 1.4 kwa mwezi kutokana na kodi. Hii ni takribani 30-40% ya kodi iliokuwa inakusanywa kabla ya utawala wa awamu ya 5. MCC-2 imetunyima trilioni moja (1) tu katika awamu yake hii ya pili.
Tukifungua akaunti maalum (labda tuiite "KIBOKO YA MCC" ) na tukaweka asilimia 8 tu ya kusanyo la TRA la kila mwezi (ambazo ni Tsh bilioni 108) basi baada ya mwaka mmoja tutakuwa tumetimiza fedha tulionyimwa na MCC. Hapa tutakuwa tumeidhibiti miradi yote tuliotegemea kufadhiliwa, bila kupumuliwa shingoni, na MCC.
Mwalimu Nyerere alisema: "IT CAN BE DONE, PLAY YOUR PART !!"