Washauri anayotokea yanaonyesha aina ya washauri alio nao. Katika hili, waziri Chikawe alitakiwa kufuatilia masuala yote ya kisheria na kuhakikisha kuwa yanawekwa sawa. inaelekea huyu bwana mkubwa hajafanya hivyo na ndio maana masuala yanaibuka kila kukicha. kama hao mawakili wangekuwa wametaarifiwa na kuhusishwa katika mazungumzo tangu awali, sidhani kama wangekuja na madai hayoHvi Presidaa hana washauri???????????!
Du watu mliona mbali!, hii ni five years ago!.Kifupi swala la IPTL tunalifufua sisi, ni shirika ambalo tayari limekwisha ingia ktk liquidation process hivyo kuwapa tender ni kufufua mradi uliokufa. Wanachogombania sasa hivi ni KISU tu, ulaji huooo wanauona unakuja ...It will cost us huge!..
Du watu mliona mbali!, hii ni five years ago!.
Pasco.
Tatizo la wadanganyika mkuu wangu huyaona mambo yalipokwisha tokea, hatuna vision wala hawaoni mbali zaidi ya marefu ya kiganja cha mikono yao yaani pale tu wanapoweza kufikia. Na hata hii hutuba ya rais jana, nilijua atakuja na kamba gani maana inayoshitakiwa ni serikali yake sio Muhongo wala Tibaijuka bali mkataba mzima wa IPTL na PAP acha mbali wizi wa fedha za Escrow. Sasa rais atakapo kubali makosa yalifanyika ina maana serikali yake ndio iloingia mkataba haramu na hili la PAP ilikuwa ktk kupozea kero nzima ya IPTL kama ilivyotokea kwa mitambo ya Richmond (Dowans) kuchukuliwa na Symbion, sii yamezimwa? japo uharamu upo palepale..Du watu mliona mbali!, hii ni five years ago!.
Pasco.
Tatizo la wadanganyika mkuu wangu huyaona mambo yalipokwisha tokea, hatuna vision wala hawaoni mbali zaidi ya marefu ya kiganja cha mikono yao yaani pale tu wanapoweza kufikia. Na hata hii hutuba ya rais jana, nilijua atakuja na kamba gani maana inayoshitakiwa ni serikali yake sio Muhongo wala Tibaijuka bali mkataba mzima wa IPTL na PAP acha mbali wizi wa fedha za Escrow. Sasa rais atakapo kubali makosa yalifanyika ina maana serikali yake ndio iloingia mkataba haramu na hili la PAP ilikuwa ktk kupozea kero nzima ya IPTL kama ilivyotokea kwa mitambo ya Richmond (Dowans) kuchukuliwa na Symbion, sii yamezimwa? japo uharamu upo palepale..
ukweli ni upi basi, miradi yote ya uzalishaji umeme ambayo ni miundombinu ilitakiwa kuwa chini ya serikali (Tanesco) na usambazaji wake ndio ufanywe na mashirika binafsi wakati serikali iki control bei ya uzalishaji kutokana na gas yetu (faida hii ni ya baadaye) lakini kina sisi tumekubali kuwa gas ni ya wageni na hata uzalishaji umeme ni wa wageni inatugharimu na itatugharimu zaidi japo guaranture wa miradi hiyo yote ni serikali sio wawekezaji... tutapona kweli?
Mkuu shukran sana kwa kukumbuka haya maana tuliyazungumzia humu humu JF na watu wakampongeza sana Rutabanzibwa, mimi mmoja wao lakini alipohamishwa na kupelekwa wizara ya ardhi sijui ya ndani hakuna Mdanganyika hata mmoja alosimama na kumtetea ama kupinga. Leo hii wala hakuna anayejua huyu Mzalendo yuko wapi ama amekwama wapi..
Mkuu Mkandara,
Sisi Watanzani ni mijitu mijinga ajabu!, kosa la Tibaijuka sio kupokea pesa bali ni kitendo cha kujulikana alipokea pesa!.
Hili lidudu IPTL linajulikana fika tangu lilipoanza ni kwa rushwa mwanzo mwisho!. Wakati linafanyiwa lobbying, aliyekuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Patrick Rutabanzibwa, aligoma kupokea rushwa, akaletewa bulungutu la minoti mpaka nyumbani kwake, kwa vile tangu mwanzo alikataa, this time wakamtaim katoka, 'Mzee wa Kazi' akabisha hodi, house boy akafungua, akakabidhiwa mzigo siku ya 24 December, kesho yake ni Krismas!. Ujumbe huo ukaletwa kama 'zawadi' ya Krismas, ukaambatanishwa na kadi ya Krismas!, na kusainiwa na Bwana Mtoa Sadaka!", akitegemea demand za sikukuu na muambo wa January, lazima atashukuru!. Rutabanzibwa aliporudi nyumbani akakabidhiwa zigo lile!.
Kwa jinsi ile ile alivyokabidhiwa, tarehe 27, akalibeba zigo lile vile vile lilivyo na kulirudisha kwa 'mwenyewe". TISS walijua kila kitu, TAKUKURU walijua kila kitu, serikali ilijua kila kitu, they were all well taken care off, why only Tibaijuka?!.
Aliyekuwa Mkuu wa nchi alipokea ile zawadi ya Krismasi, Waziri wake pia alipokea!. 'Mtoa Zawadi' akawaarifu 'wakubwa", Rutabanzibwa alikataa zadi na kuirudisha, na yeye ndiye kikwazo pekee anayekwamisha 'mradi!', huwezi amini kilichotokea!, Rutabanzibwa aliondolewa, na mradi ukapitishwa!. Jee mnamjua waziri wake ilikuwa nani?!.
Nasema Watanzani ni mijitu mijinga, tunapigia kelele tujisenti twa escrow, ambayo sio chanzo ni matokeo tuu!, malipo hayo ya IPTL ynayobishaniwa ni kiwango cha capacity charges tuu, mkumbuke IPTL bado inameza mabilioni kadhaa ya utility kila siku iendayo kwa Mungu!, nobody cares!.
Turudi kwenye mgao wa Escrow, PAP amegawa 'sadaka' kubwa kubwa nene nene, kwa 'wanene' kupitia Stabic Bank, kwa vile majina hayajatajwa, then its ok!. JR amegawa sadaka kubwa kubwa nene nene, kwa 'wanene' kupitia account yake iliyoko Uholanzi, majina yapo na viwango vipo, na wanajulikana!, ila kwa vile hawajatajwa, Watanzania mazuzu tunashangilia Tibaijuka amewajibishwa!.
Nahisi sio wengi wanaojua kuwa IPTL/PAP bado inaidai Tanesco nyingi kuliko fedha zote zilizokuwemo escrow!, na kwa vile bado IPTL inazalisha umeme, deni hilo linaongezeka siku hadi siku, na malipo yake yatafanyika direct kutoka Tanesco into IPTL/PAP kimya kimya!, and life goes on!, nobody cares!, watu wanashangilia ujinga kwa kuangalia tulipoangukia baada ya kujikwaa, badala ya kuangalia tulipojikwaa!.
Pasco.