Uamuzi kesi namba 456 ya kuzuia uchunguzi wa Jeshi la Polisi inayowakabili wanahisa JamiiForums kutolewa Februari 22, 2019

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Februari 22, 2019 kutoa uamuzi katika kesi ya kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi inayomkabili mkurugenzi mtendaji wa mtandao wa Jamii Forum, Maxence Melo na mwenzake Micke William.

Siku hiyo mahakama itatoa uamuzi kama washtakiwa hao wana kesi ya kujibu au la.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu Januari 28, 2019 na hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Salumu Ally wakati shauri hili lilipokuja kwa ajili ya uamuzi.

Hatua hiyo imefikia baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wa mashahidi wanne waliotoa mahakamani hapo dhidi ya washtakiwa hao.

Awali, wakili wa Serikali Elizabeth Mkunde amedai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili kutolewa uamuzi kama washtakiwa wana kesi ya kujibu au la, lakini hakimu anayesikiliza shauri hilo amepata udhuru na hayupo mahakamani.

Baada ya maelezo hayo, hakimu Ally ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 22, 2019, kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maamuzi.

Miongoni mwa waliotoa ushahidi katika kesi hiyo ni ofisa mkuu wa upelelezi kanda Maalum ya Dar es Salaam, SSP Ramadhan Kindai (42), ambaye aliieleza mahakama hiyo kuwa yeye ndiye aliyetoa amri ya kukamatwa kwa Melo (40) na Mushi baada ya kushindwa kutoa taarifa sahihi kuhusu habari iliyochapishwa kwenye mtandao wa JamiiForum.

SSP Kindai amedai kuwa waliomba kampuni hiyo taarifa kutokana na shauri lililofunguliwa na Usama Mohammed ambapo walihitaji kufanya uchunguzi wa kina kuhusu taarifa zilizochapishwa kwenye mtandao huo.

Shahidi huyo alidai Februari 19, 2016, mteja wao Mohammed ambaye ni ofisa msimamizi wa mauzo ya rejareja wa kampuni ya Oil com, alifika katika Ofisi ya mkuu wa upelelezi na kutoa malalamiko kwamba Februari 13, 2016, alisoma kwenye mtandao wa Jamii Forum ambapo ilidaiwa kampuni hiyo imekwepa kodi bandarini na wanaiibia Serikali.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 456, 2016, washtakiwa wanadaiwa kuzuia jeshi la polisi kufanya uchunguzi, kinyume na sheria namba 22 (2) ya sheria ya makosa ya mtandano namba 14 ya mwaka 2015.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Aprili Mosi, 2016 na Desemba 13, 2016 katika maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni.

Kujua kinachoendelea kwenye kesi nyingine soma;
 
Duh, itabidi nikaishi mpakani mwa nchi jirani ili kikinuka tu nisepe.
 
Mungu ibariki Jamiiforums.

Ata hawa asilimia ndogo ya wa Tz wanaopata kinachoendelea serikalini kupitia JF watakwenda kukikosa na kubaki kizazi bubu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawana kesi ya kujibu, maandishi yetu ni mali yao lakini maandishi yetu siyo mawazo yao, wala hatujadiliani nao wakati tinaandika.

Vivyo wao kutakiwa kumtoa muandishi ni JF hawahusiki na taarifa hiyo, labda wanataka kutafuta sababu kuifuta otherwise na hakika hawatakuwa na kesi ya kujibu.
 
Back
Top Bottom