Gorgeousmimi
JF-Expert Member
- Jun 21, 2010
- 9,296
- 7,713
IN GOD WE TRUST BUT IN HUMANS WE INVESTIGATE FURTHER! lol!
^^
Kuna dhana mbili mimi49 ulizoelezea hapo, UAMINIFU na KUSAMEHEANA
..
Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100% juu ya tafsiri yako ya uaminifu japo umei-attach sana na personality yako ya uaminifu na ukweli..
Hebu tujadili kidogo uaminifu ktk mtazamo wangu ambao naweza kusema ninajisikia mi ni mwaminifu ikiwa "..ni tayari kueleza mawazo yangu, namna ninavyojisikia na mipango yangu. Ninafanya hivyo bila kuficha, siepi kupambana na matatizo. Sijaribu kujionyesha ni mtu bora zaidi kuliko mwenzangu wala sijaribu kujivuna. Sijaribu kuficha makosa yangu wala kuyakuza niweze kuvuta huruma ya watu, nipo tayari kuheshimu hisia na mtazamo wa mwenzangu hasa pale tunapotofautiana na inaponilazimu kuziba ufa na mtu ili kuepusha kujenga ukuta mzima nipo tayari kufanya hivyo kwa upendo na nia njema maana natambua binadamu hatulingani.."
Kwangu mimi huo ni uaminifu kwa nafsi yangu na wenzangu
Tuanzie hapo kwanza kabla ya dhana ya kusameheana
^^
hii penine ndio miongoni mwa mijadala inayovuta hisia za watu wengi.
nionavyo mimi;
sisi kama wanadamu wenye utashi tunawajibika kuishi kwa imani na uaminifu kwa wale tunaoamua kushirkiana nao katika maisha yetu,wakiwa marafika au hata wapenzi udhaifu wa mtu mwingine usipunguze thamani ya utu wako,kwa mafono mtu kupoteza imani na mapenzi kwa vile tu kasilitiwa na mapenzi,hii si sahihi haijalishi imesababisha maumivu kiasi gani kwako.
maisha yetu sis yawe ni kama chuo cha kujifunza kutoka kwenye hali duni kwenda kwenye hali bora zaidi,lakini ukweli wa mambo kila siku tunajifunza kutoka kwenye hali bora kwenda kwenye hali duni.
kama mtu umesalitiwa na mwenzio litumie hilo tukio kama funzo la kukujenga na kukuimarisha kuwa binadamu bora zaidi.
dhana hii haipingani na ukweli kwamba usaliti na vingine vinavyofanana na hivyo vinauniza.
dhana ya kusamehe pia ni ya msingi ni ngumu kusamehe lakini ni bora na afya zaidi kuwa na moyo wa msamaha kuliko wa malipizi na visasi.
nimalizie kwa kusema hivi ubora,na uimara wa mtu unapimwa kwa kiwango cha uwezo wa mtu kuwa mwaminifu na mwenye moyo wa kusamehe haijalishi anapitia ugumu kiasi gani.
Ni kweli unapomuamini mtu maanake upo tayari kumueleza chochote bila kusita lakini iwapo mtu huyo huyo unaemuamini anapokuja kukugeuka na kukupa uongo SO CHEAP bila ya hata guilty consious utamueka fungu gani kiumbe huyo?Achilia mbali hivo,kukiri kosa lake hakubali na ana pride kwamba I GOT AWAY WITH THIS?Utajengaje moyo wa kumuamini yoyote tena?
^^
Kuna dhana mbili mimi49 ulizoelezea hapo, UAMINIFU na KUSAMEHEANA
..
Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100% juu ya tafsiri yako ya uaminifu japo umei-attach sana na personality yako ya uaminifu na ukweli..
Hebu tujadili kidogo uaminifu ktk mtazamo wangu ambao naweza kusema ninajisikia mi ni mwaminifu ikiwa "..ni tayari kueleza mawazo yangu, namna ninavyojisikia na mipango yangu. Ninafanya hivyo bila kuficha, siepi kupambana na matatizo. Sijaribu kujionyesha ni mtu bora zaidi kuliko mwenzangu wala sijaribu kujivuna. Sijaribu kuficha makosa yangu wala kuyakuza niweze kuvuta huruma ya watu, nipo tayari kuheshimu hisia na mtazamo wa mwenzangu hasa pale tunapotofautiana na inaponilazimu kuziba ufa na mtu ili kuepusha kujenga ukuta mzima nipo tayari kufanya hivyo kwa upendo na nia njema maana natambua binadamu hatulingani.."
Kwangu mimi huo ni uaminifu kwa nafsi yangu na wenzangu
Tuanzie hapo kwanza kabla ya dhana ya kusameheana
^^
Habari ndefu!!
nashukuru Himidini!^^
Blessed nimependa ufafanuzi wako, naomba nidadisi ulipoishia, ..nini kifuate baada ya kusamehe..?
^^
Wakumwamini ni "Binadamu aliyekufa tu" wengine ni kuvumiliana sio kuaminiana la sivyo ni presha tupu
Utakuaje kwenye uhusiano bila kumuamini mwenza wako?huo uhusiano utakuwa umejengwa kwa misingi gani?
Hivi Himidini inapotokea unakua mwaminifu kwa mtu na unamweleza kila hatua unayopitia halafu haitilii maanani utajisikiaje ama kumchukuliaje?
Na mtu huyo huyo anakua hakuambii yanayomuhusu utalichukuliaje hilo?
nashukuru Himidini!
inatokana na aina ya uhusiano uliopo na nafasi ya muomba msamaha!
kwa mfano kama ni wapenzi na kuna usaliti,na mkosaji akaomba msamha na kama yuko tayari kuendelea na uhisiano ni jambo la kuamua hapo pia.
kusamehe ni kuishinda nafsi(miongoni mwa mitihani migumu zaidi)
na kuweza kuishinda nafsi ya mwenzako(hapa na maanisha hivi kutokuangalia udhaifu na mapungufu ya mwenzio kuhakkiisha unauona uhodari na ukamilifu wake na siku moja kumfanya auone ukamilifu wake na auishi i.e kila mmoja ana ukamilifu ndani yake na anaweza kuuishi sasa msamaha unaweza kuchochea hali hiyo),sio nadharia inawezekana japo ni ngumu,tukiishi hivi maisha yetu yatabadilika ,n maisha hayatua ya majuto kamwe
Kutokana na jibu lako sishangai kwanini mahusiano mengi ya siku hizi hayadumu!Misingi hiyo hiyo ya kudanganyana, ndio njia pekee ya kujiepusha na stress za maisha ya kisasa haya. pamoja na ukweli kuwa kuishi maisha ya namna hiyo inapunguza ile ladha yote ya mahusiano ila ndio njia pekee ya kujiokoa. Dont expect anything and yet expect everything baasiiiii maisha yanasonga.