Anfortyunaitl nina wasi wasi sana na mkakati wa Baraka. Binafsi, simpendi Mitt lakini kuna dalili za kutisha kuwa kuelekea siku ya uchaguzi Baraka atakosa oksijeni kabisa; si kwa sababu ya uhodari wa Mitt, bali kwa sababu ya uzembe wa Baraka mwenyewe kushindwa ku-atikyuleit mafanikio ya utawala wake na kumwacha akiwa ovashaw'd na spins za akina Mitt. Miaka minne ya Baraka ina mafanikio makubwa sana kuliko miaka minane ya Bush.
Ndugu Hofstede unanitia matumaini tu lakini bado nina wasiwasi sana; nitasubiri matokeo. Ninapenda sana Baraka aingie kipindi cha pili kwa sababu ameshamaliza kusafisha uchafu, kipindi hicho kitakuwa kizuri sana iwapo kinaonekana ni maendeleo ya sera zile zile. Mabadiliko ya uongozi yatasababisha kipindi kijacho kiwe cha kuanza sera nyingine, na mambo yanatayumba na yanaweza kuwa mabaya zaidi.
Mimi wasiwasi wangu ni kuwa Obama ameisha safisha njia na kama wamarekani watamnyima ridhaa ya kipindi cha pili ni dhahiri kuwa credit zitaenda kwa atakayekuwa madarakani just by sitting and watching. Maana Romey hana ajenga inayoeleweka he is everywhere anapoona kunaweza kumpatia ushindi yeye anaelekea tu.
I hope wamarekani si wajinga kiasi hicho, DNC itaweka wazi hili na huenda tutashuhudia gap kubwa sana baada ya convention. GOP wameamua kwenda rogue kwa kuazisha uwongo dhidi ya Obama na kuufanya ukweli ila nina hakika kuwa uchagui huu mpaka sasa Obama ana upper hand, unless miezi hii miwili itokee recession nyingine kama ya 2008