mapinduzi daima
JF-Expert Member
- Sep 30, 2013
- 1,724
- 2,709
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Bi. Nikki Haley amejiuzulu wadhifa wake hivi punde.
Taarifa rasmi kutoka Ikulu ya White House zinatabanisha hapa katika viunga vya UN, kuwa Rais Donald Trump amekubali barua ya kujiuzulu ya Balozi Nikki Haley.
Ndani ya dk 15 hadi 30 kutoka sasa, Rais Trump na Balozi Haley watakuwa na Press Conference katika Ikulu ya White House...
Sababu ya kujiuzulu kwa Balozi Haley bado haijatajwa rasmi
Balozi Haley alikuwa anatajwa kama raising star katika chama cha Republican na anatajwa kuwania Urais baada ya kipindi cha Rais Trump kuisha.
Wasaalaaam...
==========
Rais Donald Trump ameridhia kujiuzulu kwa Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa (UN), Nikki Haley.
Vyombo vya habari vya nchini humo vimeeleza kuwa kujiuzulu kwa balozi huyo ambaye ni Gavana wa zamani wa jimbo la South Carolina, kumefanyika ghafla.
Hata hivyo, Ikulu ya Marekani (White House) mpaka sasa haijaeleza chochote kuhusiana na taarifa za kujiuzulu kwa Haley ingawa ilithibitisha Rais Trump kuwa na kikoa naye.
Haley aliteuliwa kuwa Balozi wa Kudumu wa Marakeni katika UN Januari mwaka 2017.
Kujizulu kwake kumekuja baada ya kutumikia kwa muda nafasi ya Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa muda wa mwezi mmoja.
Aprili mwaka huu, alikwazana na White House baada ya kudaiwa na wasaidizi wa Trump kwamba alitangaza hatua nyingine ya vikwazo dhidi ya Russia kabla ya wakati.