U-CCM ndani ya CUF na NCCR Mageuzi

EJM_

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,836
2,090
Hivi karibuni kumekuwa na migogoro mingi kwenye vyama hivi viwili kiasi cha kutaka kufukuzana ama kufukuzana kabisa kwa baadhi ya wabunge. Nimekuwa nafakari kidogo kuhusu sababu hasa ya migogoro hii, je ni kweli hawa watu wamepotoka ndani ya vyama vyao au ni U-CCM ndani ya vyama hivi?

Tangu CUF wamekuwa na muafaka na CCM kule Zanzibar, status ya chama hicho hasa kwa upande wa Bara imeporomoka kwa kiasi kikubwa sana (Hii inathibitishwa na maelezo ya Mtatiro wakati akiongelea kuhusu uchaguzi wa Igunga aliposema CUF imeshindwa kwa kuonekana kuwa CCM B) lakini pia ideology za baadhi ya viongozi wa chama hiki sasa zimeanza kutofautiana kwa kiasi kikubwa kiasi cha kupelekea migogoro inayoendelea sasa.

NCCR Mageuzi nao wameonekana kutokuwa na mwelekeo ila kinachonitatiza ni kuona wale wabunge wao ambao kwa mtizamo wa watu kama sisi huku nje wanaonekana kuichachafya sana serikali ya CCM (Kafulila) sasa wanaundiwa zengwe la kuondolewa chamani.

Dah labda mtu anisaidie why now? na kwanini hawa tu?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom