watu wengi hawajui tatizo letu ni nini? kuna kiwango kikubwa cha fedha kwenye mzunguko kuliko ilivyotakiwa hii ni sababu ya kutoweza kutawala kiwango cha fedha kwani kuna noti za aina mbili na wahusika wameacha fedha nyingi katika mzunguko kuliko kiwango kinachotakiwa
Godwine,
Nafikiri wewe ndio hujui tatizo liko wapi katika sarafu ya nchi hii. Kusema kuwa kiwango cha pesa kiko katika kiwango kingi katika mzunguko pekee ndio sababu ya kushuka sarafu nakukatalia kwasababu serikali muda maalum wa kuzitoa pesa katika mzunguko. Huo muda tukaja kuambiwa umeondolewa kwasababu zile pesa zilizoletwa mpya zina walakin sijui serikali ina msimamo gani sasa katika sarafu za zamani na sarafu za sasa. Na ikiwa mzunguko wa fedha ni mkubwa serikalini kwanini basi benki kuu inaendelea kuuza treasury bonds na bills zake kwa bei ya chini badala ya kupandisha bei ya Tbills and bonds at high prices ili kupandisha interest rate on loans nchini na kupunguza kiwango cha pesa katika mzunguko. Vile vile kuna njia mbali mbali BOT inaweza kusaidia mzunguko wa pesa kupungua na BOT wameshindwa kuzuia kuanguka kwa shillingi nchini.
Sababu za kushuka sarafu ya Tanzania kwa ninavyoona mie:-
a. Kuzidi ama kuongezeka kwa matumizi ya foreign currency nchini. Tanzania ndio nchi inayoongoza East Africa kwa watumiaji wake account katika benki za biashara zinazomilikiwa in foreign currencies. Dollar inatumika kama sarafu ya kulipia bidhaa mbali mbali kama kodi ya majengo, school fees, TRA, na kadhalika. Demand ya fedha za nje ikipanda basi demand ya sarafu yako ya madafu itashuka na ndio hali halisi ya kinachoendelea nchini. Watu wanamiliki dollars kuliko Tshs na matokeo yake shillingi inakosa mwelekeo.
b. Kupandisha mshahara bila kuangalia kiwango cha ukuaji wa uchumi. Mishahara imekuwa ikipanda na kusababisha purchasing power iongezeke na kuongeza mzunguko wa fedha katika nchi. Serikali imekuwa ikipandisha mishahara kiholela pasina kuangalia athari zake katika uchumi na sarafu ya nchi. Watu wakiwa na hela nyingi mfukoni gharama za maisha zinapanda, gharama za maisha zikipanda gharama za uzalishaji zinapanda. Vyote hivi vikipanda matokeo ni sarafu inaporomoka kwani mahitaji ya pesa yanakuwa machache ila upatikanaji wa fedha unakuwa mkubwa na matokeo tunayaona kwani mkate sasa unaweza kununua mpaka Tshs 2000 kutoka Tshs 250 by average.
c. Ufisadi nao umechangia kuporomoka kwa sarafu yetu kwasababu pesa zinazoibiwa zinasafirishwa nje ya nchi. Mfano thamani ya Shilling miaka 2004-2005 iliporomoka kwa kiwango kikubwa (chukua Excel Sheet ya BOT uangalie mwenyewe). Pesa zinazosafirishwa nje ya nchi zinabadilishwa na Tshs na matokeo bei ya fedha za kigeni inapanda.
d. Kukosekana kwa sheria ya kuzuia speculative behavior kutoka kwa currency traders, business personell na benki za biashara. Kama umeangalia tofauti ya bei ya USD BOt na Commercial banks utagundua kuna dalili ya speculations inafanyika kwa baadhi ya wadau wa sekta husika. Mfano jana thamani ya British pound BOT ilikuwa 2670 wakati NBC walikuwa wanauza 2780 na CRDB wakiuza 2735. Difference hii ni kubwa na inaumiza kwa baadhi ya wafanyabiashara. Mfano mtu kama Bakhressa akitaka kununua £1,000,000 kutoka CRDB atalipa Tshs 2,735,000, 000 na NBC atalipa Tshs 2, 780,000,000 na benki za biashara zitalipa Tshs 2,670,000,000 kuna tofauti ya karibu millioni 100 benki za biashara zinapata kutokana na kulangua bei ya sarafu ya kigeni. Ukienda bureau de change ndio kabisa kwanza utakuta wanazipoteza katika mzunguko kupandisha bei ya fedha za kigeni na ukizipata utauziwa bei ghali. Hizi tabia ni hatari kwani kutokana na speculation hii anayeumia ni mtumiaji kwani bakhressa atauza kwa bei ya juu kurudisha gharama zake na matokeo mfumuko wa bei.
Kinachotakiwa kufanyike jitihada za haraka kuikoa sarafu wapunguze mzunguko wa fedha kama unavyoshauri ila vile vile wapunguze matumizi ya fedha za kigeni nchini mwetu. Kulipwa watu mishahara in foreign currencies, school fees kulipwa in foreign currencies, nyumba unalipia kodi kwa foreign currencies vyote ni hatari kwani thamani ya shillingi inaonekana haina maana. Vyenginevyo tuvumilie tu na tumsikilize gavana wetu anayesema sarafu kushuka ina faida wakati hata kiatu hatuuzi nje ya nchi. Bidhaa tunazouza nje ya nchi hatuna hata sauti ya kupanga bei mwishoe tunaumizwa na sarafu dhaifu na mapato dhaifu. Nilikuwapo!!!