Tz mabigwa wa kubadilisha kanuni/sheria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tz mabigwa wa kubadilisha kanuni/sheria

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kwaroz, Feb 11, 2011.

 1. Kwaroz

  Kwaroz Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Naona watu wengi sana wanachanganya mambo, wapinzani si wamoja na hawana sababu za kuwa wamoja kama wangekuwa wamoja basi wangekuwa na chama kimoja cha upinzani kikiwa na vision na mission moja, lakini hilo halipo kila chama kina vision na mission yake. Sioni haja ya CCM kuwachonganisha wapinzani kwa kigezo kwamba wao ni wamoja na lengolao nililelile kutaka kuendelea kutawala kwa kuwachanganya wote.

  Hoja si uchoyo kwa kuwa mabunge karibu yote ya commonwealth wanakambi rasmi ya upinzani na kama chama kinaomba kujiunga ni hiari ya chama husika kukubali au kukataa na sio kushinikizwa na kanuni kwa kuwa kila chama kina mwongozo wake na ilani yake. kwa mfano chadema wanasema wanatoa elimu bure kuanzia chini mpaka form six lakini vyama vingine vinamlengo tofauti juu ya hilo, CCM walishasema haiwezekani na vyama vingine walisema kuboresha elimu yote kiujumla sasa ni sababu zipi zinawafanya hivi vyama kuwa tofauti na sababu ipi itafanya hivi vyama kuwa pamoja ni hakuna. mfano kuna chama cha kutetea mazingira cha ujerumani, cha uingereze na vingine vingi, hata siku moja haviwezi kuwa sawa na kushirikiana isipokuwa pale tu kama ilivyotokea Israel na Uk pale waliposhindwa kutengeneza serikali kama chama kimoja kwa kuona watakosa kura ya kufanya maamuzi hivyo chama kilichopata ushindi kulazimika kuomba chama kingine kuungana nacho na si kulazimisha kubadili kanuni na kuwafanya kuwa wamoja hilo haliwezekani hata siku moja.

  Kwa sasa Tanzania haijulikani tunafuata mfumo upi wa utawala maana njia rahisi ni kubadili kanuni na wanasahau ni kwanini kanuni ziliwekwa kuna jambo lilisababisha zikawepo je leo hii hizo sababu za msingi za kufanya hivyo hazipo, zimeenda wapi au tulijiwekea tu bila kuwa na sababu ya msingi? Nchi yetu imeshuhudia mambo ya kipumbavu kama haya na ndio maana hata leo katiba inaonekana haina maana kwa kuwa njia rahisi ni kuondoa kifungu kwa kifungu ili kurahisisha mambo. Kwa mgombea binafsi tuliamua kuondoa kifungu, kupinga matokeo ya kura za uraisi tuliamua pia kuondoa na kubadilisha kifungu, kwa sasa tumeingia kwenye kanuni za Bunge tumeamua kubadili kanuni sasa sijui sisi tunamatatizo gani wanaCCM kwanini tusiheshimu utaratibu tunaojiwekea? nadhani ipo siku kikomo cha uraisi hicho kifungu kitaondolewa tena au kubadilishwa na kuwa hakuna muda wakikomo na tumekuwa ni sawa na watu waliokula nyama ya mtu hatuachi kuondoa vifungu vinavyotukwaza ili kulinda au kutetea maslai ya watu.

  Kwa sasa Bunge letu limekuwa Bunge la vituko sana hata mtu anayeangalia anashindwa kuelewa wabunge wanafanya nini ndani ya chombo hicho, wabunge wapo sokoni, hapana, wapo stend ya basi au steshen hapana maana huko ndio hakuna utaratibu kila mtu na shughuli zake na mtazamo wake labda kuna sehemu tumekosea turudi nyuma na kujirekebisha maana mwaka huu si mwaka wa lelemama ni mwaka wa Jubilee Mungu atasema kwa njia zake wale viongozi sio sagi wajiangalie maana kuna jambo kubwa Mungu atafanya.

  Mungu Ibariki Tanzania, Mungi Ibariki Afrika
   
Loading...