TZ economy to surpass Kenya, forecast shows. Hongera Kikwete!


Hivi ni kitu gani nyie mnakipinga hasa hizi figures za uchumi kukua za uongo, kiwango cha uwekezaji nchini ni cha uongo? Mapato ya nchi kuongezeka ni ya uongo au mna jengine mnalolipinga? Hembu tupeni basi figures zenu nyie kuwa uchumi haukui tujifunze? Vile vile sijazungumzia income distribution nchini kwani unalolieleza kuhusu sukari na gharama ya maisha hata Kenya they face a similar problem, Uganda pia. India is the 9th LARGEST ECONOMY IN THE WORLD but 70% of the population in India are living with less than 1$ a day kama Tanzania. Mmejiuliza kwanini? Lakini India tunawasifu Tanzania mnawabeza mna wivu nyie loh!!!!
 

Ingesaidia wewe kama ungekuja na kutuelezea government home initiated programmes ambazo zimezaa matunda na sio kuja kutujengea economical zones halafu kujakutuletea wamalasia waje kuwekeza. Tunataka uje utuambie sera za serikali ambazo zipo aimed fully kuwanufaisha watanzania kwa upande mkubwa na si hadithi za shule na vyuo vilivyojengwa kupitia donors conditions. Uchumu unakuwa kwa kuwa tunagawa kila kitu hovyo hovyo lakini si kwa sera za watu kuona mabadiliko kule alipo mjomba wangu mzee Mkandawire, uko mjomba noma tukianza kusikia hata sasa jamaa mlo mmoja tu si kasheshe la vile hapo sasa tunaweza kumsifia JK. Lakini si kwa gdp figure hizo azilishi watu kaka.
 

Hongera! Kweli bila CHADEMA kusumbua na vurugu zao uchumi wetu ungekuwa kwa 10%. Vurugu za CHADEMA zimerudisha uchumi kwa 3%, hiki ni chama hatari sana kwa maendeleo ya Tanzania.

Swali ni vipi tufanye ili tuwaengue kisiasa ili tufanikishe lengo letu la kuipiku Kenya? Chama hiki kinatafuta point kwa serikali kushindwa kiuchumi na sio chama kinachosaidia kukuza uchumi.

Uchaguzi wa 2015 tuwaengue hawa watu hatari.
 
Nilidhani unazungumzia CCM!
 
Nani amekuambia Kenya wako constant but Tanzania uchumi wake unakuwa kwa kasi, unapanuka kwa kasi na vile vile foreign investors wanawekeza kwa wingi nchini kuliko Kenya. Kama hufahamu uliza ndugu sio kubeza tu.
Mkuu, hao unaowaita foreign investors wanakuja kwa wingi Tz zaidi ya Kenya wanasaidia nini economy ya nchi zaidi ya kusomba utajiri, sitaki kupinga huo utabiri ila nadhani utatimia tu kama kutakuwa na change of policy kwenye sekta zote ikiwa pamoja na kuangaliwa upya kwa kodi...nchi haijengwi kwa kodi za wafanyakazi pekee
 

@Mdondoaji, Hivi unaelewa ni kwa nini wananchi wanalalamika maisha magumu lakini serikali ikisaidiwa na wewe mnahuburi kuwa GDP inakuwa?
Madini na Telecommunication ndio zinaongoza kwa kuchangia kwenye ukuaji wa GDP.Tatizo kubwa (hasa kwenye madini) serikali inaambulia tupu - Capital outflow ni kubwa sana. Pili hakuna linkage kati ya madini kwa na local economy. Unakuta wana-outsource karibu kila kitu sisi tunabakia kuuza nyanya. Kwa hiyo huu uchumi utaendelea kuwa wa kinadharia kwa watanzania weng, sadly!
 
kila soko linaye hata kama ni mmoja so sishangai wewe kuwa hapa, nwy ni mwisho wa mwaka na kila mtu anaonyesha bidii yake ili ongezeko liwe kubwa, mwisho nashindwa kuelewa kwa nini bongo tunashindana sana na kenya wakati wao wenyewe wana matatizo kibao...kwa hiyo gdp ya TZ ikiwa juu zaidi ya kenya na bado tunapata mlo mmoja kwa siku bado utasifia magamba...kwa kweli itakuwa vigumu sana kuipiku kenya kwa kutegemea akili za watu kama wewe
 

United Kingdom is the fifth largest economy in the World behind 1. USA, 2. China, 3.Japan, 4. Germany. Unahabari uchumi wa UK 60% unategemea sekta ya huduma kama Telecommunication, Banking, Food and Tourism?? What is wrong with that? Anyway nafahamu kuna matatizo katika uchumi unaotegemea service sector but niwaulize swali uchumi tanzania unakua au haukui nini hasa tatizo lenu katika economic performance ya JK? Tuzungumzie kwanza GDP halafu tuhamie katika structure ya GDP na matatizo yake.
 

Kama umezaliwa jana ni vigumu kuelewa, lakini kama una umri wangu nitakushangaa kuuliza swali hilo. Fuatilia historia.

Kifupi, Kenya haikuwa miongoni mwa nchi Tano za mstari wa mbele ktk ukombozi wa Afrika. kwa hiyo waliweza kufanya biashara na S afrika na nchi nyingine wakati wote wa harakati. Kenya imekuwa sikio la Uingereza, Israel, Marekani na nchi zote za Ulaya toka uhuru mpaka leo hivyo kufaidika na mikopo mingi na kuuza bidhaa zao huko kwa muda mrefu.

Hizo ni sababu chache tu za kuzitaja ambazo kama mwana uchumi unaelewa impact yake. Rejea South na North Korea kuhusu mahusiano na uchumi.
 
Nilidhani unazungumzia CCM!

Ni CHADEMA wala sijakosea. Mnatuharibia sana nchi yetu.

Kwa watoa hoja wengine wa CHADEMA wameshaanza kuzungumzia VITA TANZANIA, mkimzingizia LOWASA Eti ndie anayetabiri vita TANZANIA.

Mnajua thamani ya vita nyie, ile ya UGANDA imetuacha chali mnataka vita nyingine.

Libya inadaiwa $480 bilioni, mnaonaje ndio taarifa nzuri hizo. Achani ujinga tuachieni nchi yetu.
 
Hatudanganyiki. Haiwezikani kwamba tunaipiku Kenya as if wao wamelala tu. Hiyo ni vice versa.

Tanzania has got the potential to be aguably one of the largest if not the largest economy in Africa.Emphasis here being potential.
potential is very much like talent if you don't develop it,it would never be fully expressed.
If we r serious about economic growth that is not all about data but actual translation in improved living conditions for the citizens,then we must take concrete steps to develope those potentials.

1.Invest in improved and quality education.
2.Power generation
3.Sustainable political system
4.Qualitative health care delivery
5.Infrastructural development.
6.Security





GDP does not measure economic strength, only the size of the economy. It is generally positively correlated to economic strength but the strength of correlation varies from country to country depending on their population growth, spread of wealth etc. There is no single neo-classical method for measuring economic strength, but there are various indicators that inform analysts of the strength of the economy.

It depends on the country in question's method of calculating consumer spending. Consumer spending is the variable in the GDP equation for which population may be factored in. The effect of wrong population figures on GDP is somewhat nuanced in developing countries where Consumer Spending will only make up a small percentage of GDP - less than 20%.

Compared with Yankee where 70% of GDP is from Consumer Spending, the effect of having wrong census figures in Tanzania is not pronounced. It only becomes pronounced when we calculate GDP per capita, where our overinflated census figures reduces our GDP per capita putting us at the bottom of any development index.
 
tutabaki kuambiwa uchumi unakua lakini hatuoni afadhali yeyote

Hawa CHADEMA wanatafsiri mbaya sana ya neno 'UCHUMI KUKUA'. Inabidi waelimishwe maana ya neno hilo duniani.

Wewe kijana hebu sikia, unajua Duniani CHINA ni ya pili kwa ukubwa wa uchumi. Wananchi wake ndio unaowaona Manzese na wametawanyika nchi nzima. Hivi unajiuliza kama uchumi kwao umepanda na wanashika nafasi ya pili kwanini wahangaike huko manzese. Hii ni kwa vile wanaelewa ni nini maana ya uchumi kupanda kwa nchi masikini. Halikathalika Urusi.

Hii ni longterm program, matokeo yake kwa mwananchi wa kawaida si sawa na kufanya biashara asubuhi na kupata mapato jioni.

Nyie CHADEMA NI WATU WA BIASHARA KWANINI MNAJIFANYA KAMA HAMUELEWI? Kazi kweli kweli vijichama vya KIUKOO.
 

Stop being over-jubilant for nothing my dear!
 
Kuipita Kenya kiuchumi haina maana kwamba uchumi wetu ni mzuri......... Kujiringanisha na Kenya ni kujidumaza kiakili......maana ninavyoijua kenya is an ailing state..... halafu sisi tunasema eti tutaipita...... ni upupu huo..... hiyo si akili..... bali ni matope......
Binafsi ningeona labda tunakaribia nchi ya Botswana, Namibia au hata South Africa kwa kusimamia vizuri maliasili zetu...... walau ningepongeza .....

Labda niulize....... kuizidi Kenya kwa GDP kuna TIJA kiasi gani kwa mwananchi ambaye anahitaji matibabu bora, elimu bora, maji safi, barabara, pembejeo za kilimo, masoko ya mazao, ajira n.k.....
 
Mdondoaji,

..wanasema tutawapita Kenya by 2030, which is 19 yrs away!! in my opinion that is not good enough.

..vilevile mchango wa sekta za kilimo,uvuvi,ufugaji,na manufacturing, utakuwa kiasi gani ktk growth hiyo?

..growth yoyote ile ambayo haigusi sekta hizo nilizozieleza hapo juu inaweza kuwa "laana" na tishio la amani kwa nchi yetu.

..kama ni growth/neema basi ni vizuri ikaonekana across the board, na umasikini nao ni hivyo hivyo.

..hii amani unayoiona Tanzania ni kwasababu wengi wanaamini kila mmoja wetu ni masikini, that we are all in the same boat.

..sasa masikini kule vijijini wakizinduka na kuona kwamba kuna wenzao ni matajiri wa kutupwa, tena at the expense ya wao masikini, basi nchi haitatawalika wala kukalika.
 
tuachanane na ndoto za alinacha, twatambaa wenzetu wakimbia
 
Kwa nini tunajivunia kwa kuipita Kenya? kwani ktk rank za economic growth Kenya ni namba ngapi?
yawezekana twajisifu kumpita mgonjwa mwenzetu kunywa uji?
Ningempongeza rais kama uchumi wetu ungekuwa walau 75% ya uchumi wa Africa Kusini by 2030.
 
Suruma!
hukuelewa response yangu kwa mdonoaji!! isome tena!!
kuhusu cooked data probably you are rite! especially when it comes to Americans protected their interests [migodi na mipango ya muda wa kati kwa TZ] they will praise even democracy!!!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…