Two Tanzanians Slain in Detroit, MI

Two Tanzanians Slain in Detroit, MI

Mzee heshima yako mkuu, na bravo kwa info za hii situaton, isipokuwa wewe, polisi, na wanachi wote hawajui chanzo cha huu unyama, sasa itakuwa ni makosa makubwa kwako ku-dismiss any tetesi at this stage bila ya kujua ukweli, ni lazima kuwe na leads ya aina yoyote ile hata kama ni ya kijinga, katika upelelezi,

halafu ni lazima kuirudia tena na tena ile crime scene, unless wewe unaelewa chanzo, otherwise any lead au tetesi ni valid na inahitaji kufuatiliwa, nilichosikia so far ni kwamba mmoja kati ya marehemu alikuwa involved na mambo ya "Makaratasi", na alikuwa njiani kwenda kuyalipia na kulikuwa na mtu aliyefahamu kuwa kwenye lile gari la marehemu wawili kulikuwa na hela nyingi, na alikuwa aliwafuatilia, kwa hiyo kama ni kweli huenda ni yeye anayehusika na hayo ma-Paper, ninarudia kama ni kweli, na ni moja kati ya lead inayofuatiliwa kwa makini kwa upande wetu, yaani Bongo,

Unless una ukweli au tetesi nyingine ni vyema ukaisema au ikasemwa ili wanaohusika wafanye kazi yao, tunaelewa sensitivity ya hii issue, na tunaheshimu kuwa uko karibu na hii situation, na tunaheshimu all the info ulizozitoa so far, na tunakutakia uvumilivu katika kupambana na the whole issue, na respect kwamba mmoja wa wazee wa hii forum upo karibu,

Halafu sikujua kuwa huko Detroit kuna wabongo wengi sisi tulifikiri ni Texas tu ndio kwenye wengi!

tupatie info hata za tetesi kama unazo, kazi njema Mzee!
 
Mzee ES,
Kama kawaida ya wa-Tanzania anapokufa mtu huwa rumours zinakuwa nyingi sana.Na hapo si rahisi kujua ni kipi ch aukweli na kipi cha uongo.Hata Baba wa Taifa alipofariki kuna watu walizusha maneno mengi sana.Mie nachowaomba ni kwamba tuwe na subira na tuwaachie Police wafanye uchunguzi wao na wakimaliza watatuambia ni nini kilichotokea.
 
Ni kweli mzee wangu, lakini kumbuka kuwa hao polisi ni wazungu tena wa huko Detroit!, sasa lazima na sisi tuwe macho na finality ya uchunguzi wao pia,

na pia in the meantime serikali yetu inalifuatlia hili kwa makini, lakini masikio yetu tunawaachia watu wa huko Ma-Detroit mtupatie news!
 
Mzee Es said:
Mzee heshima yako mkuu, na bravo kwa info za hii situaton, isipokuwa wewe, polisi, na wanachi wote hawajui chanzo cha huu unyama, sasa itakuwa ni makosa makubwa kwako ku-dismiss any tetesi at this stage bila ya kujua ukweli, ni lazima kuwe na leads ya aina yoyote ile hata kama ni ya kijinga, katika upelelezi,

halafu ni lazima kuirudia tena na tena ile crime scene, unless wewe unaelewa chanzo, otherwise any lead au tetesi ni valid na inahitaji kufuatiliwa, nilichosikia so far ni kwamba mmoja kati ya marehemu alikuwa involved na mambo ya "Makaratasi", na alikuwa njiani kwenda kuyalipia na kulikuwa na mtu aliyefahamu kuwa kwenye lile gari la marehemu wawili kulikuwa na hela nyingi, na alikuwa aliwafuatilia, kwa hiyo kama ni kweli huenda ni yeye anayehusika na hayo ma-Paper, ninarudia kama ni kweli, na ni moja kati ya lead inayofuatiliwa kwa makini kwa upande wetu, yaani Bongo,

Unless una ukweli au tetesi nyingine ni vyema ukaisema au ikasemwa ili wanaohusika wafanye kazi yao, tunaelewa sensitivity ya hii issue, na tunaheshimu kuwa uko karibu na hii situation, na tunaheshimu all the info ulizozitoa so far, na tunakutakia uvumilivu katika kupambana na the whole issue, na respect kwamba mmoja wa wazee wa hii forum upo karibu,

Halafu sikujua kuwa huko Detroit kuna wabongo wengi sisi tulifikiri ni Texas tu ndio kwenye wengi!

tupatie info hata za tetesi kama unazo, kazi njema Mzee!

Mzee ES, hiyo ni mojawapo ya maneno yanayosemwa (so it is not excluded) na kuna mambo mengine ambayo hayaeleweki, ni kwa sababu hiyo basi tunataka wapepelezi ndio watuambie rasmi mauaji yaliyotokea vipi na mazingira gani (forensics) na pia nani alihusika na kwa nini (motives) na kuna vielelezo gani vya kuonesha ni huyo amehusika bila ya chembe ya shaka (evidence beyond reasonable doubt). Tunataka kwanza tuhakikishe hawa ndugu zetu wamerudishwa nyumbani, wamewekwa ardhini, ndipo wenye kusema na tutawasikiliza waseme!!!

Kuhusu kuwa na Wabongo hapa.. tupo kaka.. bahati nzuri hatuna drama kama sehemu nyingine na hili la msiba ndio limetumulika.

Nakuambia laiti mngekuwa karibu muone jinsi watu wanashirikiana pamoja, kama jana watu walishiriki futari hapo kwenye msiba na baadaye sala kufanyika ikiongozwa na mtawa..!
 
Mzee wangu kuna mshikaji wangu mmoja huko anaitwa Ali Max, mtoto wa Magomeni yupo?

Anyway poleni sana wazee, na tunawatakia kheri na yote mnayoyapitia katika hiki kipindi, na pia my heart goes kwa washikaji kina the mazulas, George, William, Richard (Ebonight Wooo Jack!), na Mzee Jackson, pamoja na Carter,

Na shukrani kwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia, Mzee Jakaya Kikwete, kwa kuheshimu wananchi na kumtuma muwakilishi wake, Mzee Mtawa,

Inshallah!
 
Mzee ES, kilichotushangaza ni kuwa tangu lini watanzania tunaenda kutoa rambirambi mikono mitupu?
 
Miili ya marehemu Walter Mazula na Vonettha Nkya itawasili nyumbani Tanzania siku ya Jumatano, badala ya Jumatatu kama ilivyotangazwa na Baba wa Marehemu huko nyumbani na kunukuliwa na vyombo vya habari. Kuchelewa huku kumetokana hasa na ratiba ya ndege na maandilizi ya usafiri wenyewe. KLH News itaendelea kuwaletea taarifa kwa kadiri inavyopata!
 
si mzee umesema Rais kamtuma Mzee Mtawa kwa niaba yake kuja kutoa pole (kuchunguza??????) lakini kaja mikono mitupu hanajibu hata moja!! Hivi Rais anafikiri sisi ni watoto tusioweza kufikiri na kugundua when someone is bsing!!
 
Oooh! jamani, Mwenyenzi Mungu awarehemu Walter na Voletha. Walikuwa marafiki kwelikweli, walizaliwa 1979 wamerehemika wote 2006

How comes katika nchi zilizoendelea sehemu kama Michigan (mie sijafika huko) vyombo vya dola hadi leo visielewe kulikoni! bongo kweli tupo gizani kimawasiliano LAKINI huko ambako kuna CCTV kila kona jamani wakifuatilia gari lililokuwa katika nyendo nahakiaka wangesha wapata!

.........................
:U Can't Change The Nature:
 
Mr. Clean.. katika sehemu zilizoendelea Marekani.. Detroit si mojawapo! not in a practical sense anyway... Hivi unajua siku waliyouawa vijana watu wengine wangapi waliuawa usiku huo?... 24! Na hao ni Wamarekani.. now in the greater scheme of things.. where do we fit?
 
Kuna watu wengi ambao wangependa kupata nafasi ya kuja na kutoa heshima zao za mwisho kwa ndugu zetu Walter na Vonettha. Hivyo basi Bw. Ayubu Mfinanga, mratibu wa shughuli hizi na mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio Michigan anatueleza utaratibu ulivyo. Kwa heshima ya ndugu zetu Bendera ya Taifa letu itainuliwa katika tovuti ya KLH News kwa mwisho wa juma hili zima.

http://mwanakijiji.podomatic.com
 
Mzee Mwanakijiji,
ndugu yangu nimehudhulia kisomo cha marehemu na hakika vijana wamefanya kitu!... loooh mwenyewe domo wazi sii mchezo mdogo vijana wa kitanzania jinsi wanavyoweza kujituma...Bila kusubiri msaada wa watawala.
Nimejaribu kukutafuta dakika za mwisho pale msibani lakini sikufanikiwa lakini hata hivyo nimeaacha salaam zangu. Najua ulinishtukia, kuna wakati ulinipigia chapuo sii laa kutazama bali kujiuliza kama huyu ndiye mzee wetu babu ubishi wa Bcstimes?
Shukran nyingi sana ziwafikie wabongo woote popote walipo kwa michango yao ya hali na mali pamoja na umaskini yamewezekana!
Jamani UMOJA sii kitu cha kufanyia mzaha kabisa!.....Inalipa sana. Hapo Detroit vijana Wabongo wameacha record na mfano kwa jumuiya za waafrika wote! Na hii imenipa hakika kwamba kama kutakuja tokea mabadiliko Tanzania basi sii kizazi changu ila hiki kinachofuata umri wa 20 -35.
 
Mkandara,
Umesema kweli kabisa kuhusu our generation na changes.I think our generation itafanya big things huko nyumbani.Nimesikitishwa sana na ubalozi na serikali ya Kikwete kutosaidia hata kidogo kifedha kwenye huu msiba.Nilifikiri kwa vile Rais alikuwepo huku angeguswa na huu msiba lakini naona aliendelea kukata mbuga tu na hata hakuwapigia simu wafiwa.Ukisikiliza hiyo interview na Bwana Mfinanga utasikia hayo yote.
 
Radio Butiama,
Wakati Ukim - interview, nilikuwa naye ndani ya gari lake!
 
Ok! Kumbe mnafahamiana.Bw Ayub Mfinanga kwa kweli ameonyesha leadership ya hali ya juu na anahitaji pongezi kubwa.
 
Mara nyingi huwa nashindwa kumuelewa JK lakini safari hii nimemshusha hadhi kabisa.Yaani ameweza kuondoka US bila hata kwenda kuwapa pole wafiwa?He wasnt that busy na naamini kama angetaka basi angeweza kabisa kufika huko Detroit.Probably ata-turn up kwenye mazishi Dar lakini kwangu hiyo itakuwa ni sehemu ya harakati zake za kujitafutia umaarufu Bongo huku akitupuuza wabongo tulio huku nje
 
Back
Top Bottom